Hizi ndizo sababu za magari kusombwa na maji kipindi cha mvua

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Matukio ya magari kusombwa na maji na kusababisha maafa makubwa kwa watu kupoteza maisha, yamekuwa yakiripotiwa kwa wingi nchini, tukio bichi likiwa ni lile la familia moja kupoteza maisha baada ya gari aina ya Toyota Noah, kusombwa na maji katika eneo la Malula King’ori wilayani Arumeru na kusababisha vifo vya watu watatu.

Watu wengi, wakiwemo madereva, hawaelewi sayansi iliyojificha kwenye maji yanayotembea, hususan maji ya mafuriko na vyombo vya moto kama magari na kusababisha matukio ya aina hiyo yaendelee kutokea.

Wahandisi wa Chuo Kikuu cha New South Wales (UNSW), wamefanya utafiti kuhusu sababu za magari kusombwa na maji ya mafuriko, na kuja na majibu yafuatayo:
Matairi ya magari au pikipiki, huwa yanajazwa upepo ndani yake na kwa kawaida, kitu chenye hewa ndani kinapoingizwa kwenye maji, hugeuka na kuwa boya hivyo kuelea. Hii husababisha hata gari kubwa na lenye mizigo, kusombwa kirahisi kwa sababu uzito wake huwa umebebwa na matairi ambayo huelea kirahisi kwenye maji.

Magari mengi ya kisasa, yameundwa kuzuia maji au hewa isiingie ndani kutokea nje, kwa kitaalamu airtight. Hali hii hufanya magari kuwa na uzito mwepesi yawapo juu ya maji kwa sababu kama ilivyoelezwa, kitu chochote ambacho kinakuwa na hewa ndani, huwa chepesi kuelea ndani ya maji au kwa kitaalamu Bouyant.

Maji yanayotembea, hata kama ni kidogo huwa na nguvu kubwa ambayo wengi huidharau.

Mkuu wa Shule ya Uhandisi ya Chuo Kikuu cha New South Wales, Grantley Smith amenukuliwa akisema, utafiti umeonesha kwamba mita moja ya ujazo ya maji yanayotembea, huwa na uzito unaoweza kufikia kilogram 1000 (sawa na tani moja).

Smith ameeleza kuwa gari lenye uzito wa tani 2.5 likiingia kwenye maji yanayotembea yenye kina cha sentimita 95, linaweza kusukumwa kwa mkono na kusogea.

Je, ulikuwa unayafahamu haya? Jilinde wewe na uwapendao kwa kuepuka kuendesha gari au chombo chochote cha moto kwenye maji yanayotembea.
stori: hope sylus
 
Back
Top Bottom