Hizi ndiyo silaha za Jwaneng Galaxy zitakazoziangamiza Simba SC

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,747
1/ Mtendaji mkuu wa Jwaneng Galaxy (Senzo) Hii ni silaha kubwa sana (nyuklia) kwa maana Senzo anawajua Simba sc nje ndani Alishawahi kufanya kazi Simba na Yanga pia kwa hiyo anajua fitina /michezo ya ligi yetu na utundu wa wakongwe wa kariakoo.

Senzo ndiyo CEO wa ligi ya Botswana na ni mipngoni mwa viongozi watakao kuwa na furaha kuona timu (Jwaneng Galaxy) inashinda /kusonga mbele katika uongozi wake.

Na Kuna uwezekano mkubwa Senzo ndiyo atakua ametoa wazo la kupeleka mchezo katika kiwanja Cha nje ya mji.

2/ Wachezaji wa Jwaneng Galaxy wanacheza kwa kujituma Kama wanavyopewa maelekezo na kocha wao.

Niliwatazama Jwaneng Galaxy walipokua wanacheza na Orlando pirates kiufupi Jwaneng Galaxy hawana mastaa katika kikosi Chao yaani ni underdog wenye nidhamu ya Hali ya juu na wanacheza kwa discipline kubwa sana kama kocha anavyowapa maelekezo.

Kwa uchezeshaji wao wamemtoa Orlando pirates na wydad tena akiwa nyumbani kwake.

Kwa uchezaji wao Simba sc itakua na wakati mgumu sana.

3/Presha ya Simba sc wakati huu, kisaikolojia Simba sc HAWAPO sawa kutokana na kelele za mashabiki na ujio mpya wa kocha.

Kwahiyo Kama Simba Sc wasipo control saikolojia Yao ni advantage kubwa sana kwa Jwaneng Galaxy na kuchukua point 3 muhimu.

Nawasilisha hoja.
 
ninacho jua senzo ni CEO Wa ligi ya Botswana ,hayo mengine ni chuki za kike tu.
Any way mimba changa hua zinausumbufu sana ndimu zinasaidia
Yaani huyo jamaa ni utopolo mpaka anapitiliza kwa umbumbu.
 
Back
Top Bottom