Hizbullah: Ndege yetu ya upelelezi imeingia na kutoka salama katika ardhi za Palestina zinazokaliwa na Wazayuni

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Hizbullah: Ndege yetu ya upelelezi imeingia na kutoka salama katika ardhi za Palestina zinazokaliwa na Wazayuni

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon ya Hizbullah imetangaza kuwa ndege yake moja isiyo na rubani aina ya "Hassan" imeingia hadi ndani ya anga ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopewa jina la Israel kwa ajili ya kufanya upelelezi.

Duru za habari ziliripoti jana Ijumaa kuwa, sauti za ving'ora vya hali ya hatari zilizisikika katika vitongoji vya Kizayuni karibu na mpaka wa Lebanon hususan katika eneo la Al Jalil.

Televisheni ya al-Mayadeen ilitangaza jana kuwa, Hizbullah ya Lebanon imeeleza katika taarifa kwamba ndege yake moja ya droni aina ya "Hassan" ( ya kulienzi jina la Shahidi Hassan al-Laqqis) ilipaa ndani kabisa ya anga ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa muda wa dakika 40 na katika umbali wa kilomita 70; na kwamba baada ya kutekeleza operesheni ya upelelezi wa kutosha ilirejea kituoni kwake nchini Lebanon salama usalimini.

Katika taarifa yake hiyo, Hizbullah imesisitiza kuwa licha ya kuwepo silaha na zana za ugunduzi za adui, ndege hiyo isiyo na rubani ilifanikiwa kurudi salama baada ya kukamilisha kazi yake.

Hayo yameripotiwa katika hali ambayo, jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel limekiri rasmi katika taarifa kwamba, licha ya silaha na zana zote za ugunduzi lilizonazo, likiwemo kuba la chuma, ndege za kivita na helikopta halikuweza kuigundua droni hiyo iliyotokea ardhi ya Lebanon.

Kufanikiwa ndege hiyo isiyo na rubani ya Hizbullah kuingia hadi ndani kabisa ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kumethibitisha kwa mara nyingine tena ufanisi duni wa mtambo wa ulinzi wa anga wa utawala haramu wa Israel ujulikanao kama Kuba la Chuma.../

1645373543652.jpg
 
Wahuni wameona drone isiyo na madhara waka kausha. Angekuwepo binadamu ingekuwa lawama mida hii. You have to play smart, si kila muda ni violence.
 
Waliiona haina madhara na c ajabu waliijam na kuilisha false data achana kabisa na mossad
 
Vita baina ya hawa watu ipo kuanzia kwenye propaganda hadi vitendo...

Inaweza ikawa ndio au isiwe ndio pia, muda ndio utaongea
 
Mtoa mada ana story mbaya kuhusu Israel. Hata Uzi upo kipropaganda sana
 
Back
Top Bottom