Hivi wasukuma ugali lazima?

kukuna

Member
May 26, 2010
73
1
mambo wachangiaji wa jf,mi nna swali hivi hawa wenzetu wasukuma wakija kukutembelea mpaka uwasongee ugali ata kama saa za lunch zimeisha? vijisambusa,vikacholi vikaranga na soda kwao havipandi watakusema ah huyu shemeji mchoyo ukienda kumtembelea hakupikii!!!!ninyumbulisheni anti yangu kaolewa na msukuma ajionea mauza uza kutwa wageni na mizigo yao na wanataka wasongewe ugali.
 
Ukiona shangazi yako anahangaika mshauri aachike halafu umtafutie kabila wasio taka ugali maana wakati anaolewa si aliyajua hayo. Au wewe hutaki wageni?
 
hata wakurya pia,si wanawake si wanaume wote wanapenda ugali...!!!
ukikaa nao mchana jioni ugali,mpaka unakinai!lol
 
Oyaaa, acheni kupayuka hapa.

Huyo Shangazi anafahamu RAHA anazozipata baadaye usiku kutoka kwa Ngosha aliyekula ugali.

Siyo mtu kala vimikate na sambusa na anaanza shughuli nzito ya usiku. Mwisho mnaishia kunywa Red bulls na mapombe makali.
Kuleni Ugali na matokeo yake wake zenu watayaona.
 
Bila kula ugali mtu utakula nin eti; huwa nashangaa kuona watu wengine wanakula vitu vya ajabu kabisa. Wengine wanafanya wali eti ni chakula huku hicho ni kisusio tu kabla ya mlo kamili wa ugali.
 
Carbohydates, inajenga mwili na kuongeza nguvu, kwa kutengeneza energy ya mwili..na carbohydrates,inapatikana kwenye vyakula vya wanga,sukari n.k...maize meal is excellent energy provider, husaidia sana shughuli zote zinazohitaji nguvu..

....nguvu kazi...
 
kwani kuna tofauti kati ya wanga unaopatikana kwenye ugali na kwenye wali?
 
Carbohydates, inajenga mwili na kuongeza nguvu, kwa kutengeneza energy ya mwili..na carbohydrates,inapatikana kwenye vyakula vya wanga,sukari n.k...maize meal is excellent energy provider, husaidia sana shughuli zote zinazohitaji nguvu..

....nguvu kazi...

Ndugu, carbohydrate haijengi mwili bana. Kujenga mwili ni kazi ya protini
 
mambo wachangiaji wa jf,mi nna swali hivi hawa wenzetu wasukuma wakija kukutembelea mpaka uwasongee ugali ata kama saa za lunch zimeisha? vijisambusa,vikacholi vikaranga na soda kwao havipandi watakusema ah huyu shemeji mchoyo ukienda kumtembelea hakupikii!!!!ninyumbulisheni anti yangu kaolewa na msukuma ajionea mauza uza kutwa wageni na mizigo yao na wanataka wasongewe ugali.

Kaolewe na Mdindi kama unataka vikachori na visambusa!
 
Kitu ugali bwana, naufagilia sana tena ukaliwa na mlenda we acha 2, kitu pizza hata kwa koo langu haiwezi pita sijui kwa nini iyo siipendi
 
hahaha watani wangu hawa bana lazima Nguna tena iwe ile ngumu na si laini laini hivi, mwambie siku akosee awachanganyie na ulezi kidogo, wakienda Toilet shughuli yake wataipata fresh next time wakija hawatadai tena ugali hahahahahaha
 
..hee naona wasukuma wamechachamaa na hii sredi...
..sema mmezoeshwa kula maugali tangia watoto,
...kusema mnakula maugali ili muhimidi tendo la ndoa,is absolute rubbish...
...mbona mambo yenu kitandani hayasifiki kihiiiivyo...:doh:
 
Mi sio msukuma lakini nikila wali hayafiki hata masaa mawili nahisi njaa,mambo yote ugali/samaki,chapati/rosti au ndizi iliyopikwa na nyama nyingi.
 
Vyakula vyote vya kibongo tisa 10 ugali na kama ukiupatia mboga nzuri labda mchicha wa nazi, au kisamvu cha nazi, bamia na samaki wa kukaanga au nyama choma na pilipili kwa wingi ahhhhh! acheni jamani ugali una raha yake ambayo haifanani na chakula chochote cha kibongo.
 
mambo wachangiaji wa jf,mi nna swali hivi hawa wenzetu wasukuma wakija kukutembelea mpaka uwasongee ugali ata kama saa za lunch zimeisha? vijisambusa,vikacholi vikaranga na soda kwao havipandi watakusema ah huyu shemeji mchoyo ukienda kumtembelea hakupikii!!!!ninyumbulisheni anti yangu kaolewa na msukuma ajionea mauza uza kutwa wageni na mizigo yao na wanataka wasongewe ugali.
...oww hoooo wao si na wageni? basi wale watakacho kikuta bana.... halafu mie wala sijali watakayo ya sema... nyumba ya kwangu jiko langu wao ni wageni watakula ntakachokipika....
 
weweee lete mada zenye mantiki, ugali kwanza sana tu, unaleta habari za vikacholi, sambusa na kalrimati, hapa siyo zenji wala hao jamaa siyo kuchikuchi, kazi kwenda mbele. ndo maana mijamaa imekwenda juu na ina misuli ya kufa mtu, ukitaka mshauri aende akaolewe na wala bagia, dengu lakini kazi yake ataipata maana itakuwa full mdebwedo
 
Back
Top Bottom