Hivi unajua kwamba Ugali uliletwa na mabeberu Afrika? Ugali sio chakula asilia

Wazungu hawakuleta ugali bali walileta mahindi... Waafrika ndio wameyageuza mahindi kuwa ugali.. ni ubunifu tu wa kimapishi
 
Unaposema ugali fafanua ni ugali upi, ugali wa nini.

Kuna Ugali wa mahindi ya aina tofauti...
Kuna ugali wa ulezi, mtama, mchele, ndizi, viazi, ngano, mhogo nk
Sisi kigoma tulikuzwa na ugali wa muhogo,nyange na lowe je tuna akili tofauti na wasukuma?
Wapogoro/ wanyakyusa kyela chakula chao kikuu ni mchele je wana akili tofauti na wagogo?
Wakinga hula ugali wa ngano na mikate ya ngano aka mikate ya kikinga, je wana akili kulikp makabila mengine?
 
Weka picha tuone.
Ugali wenye akili huo vit.A
IMG_20210216_130018.jpg
 
Kua specific ugali upo katika category nyingi

Kuna wa muogo, mtama, ngano, ulezi nk

Halafu mbona watoto waliokaa bush wanaakili sana wakati huko wanapiga nguna ambayo haijakobolewa?
 
Sema hivi ugali Wa mahindi siyo chakula ila ugali chakula kama unatumia nafaka nyingine kama muhogo mtama ulezi ngano ndizi viazi n.k ngoja nitoe chanzo cha kula ugali Wa mahindi mahindi siyo zao LA asili ninafaka iliyotengenezwa maabara kwaajili ya kupata chakula cha mifugo,kuna mahindi kwaajili ya farasi kuna mahindi kwaajili ya nguruwe kuna mahindi kwaajili ya ngombe Wa maziwa na mahindi kwaajili ngombe Wa nyama chanzo chakuliwa kwa ugali Wa mahindi kulianzwa na manamba wale waliokuwa wanafanya kazi kwenye mashamba ya ngombe Wa maziwa wenye range za ngombe Wa maziwa walikuwa hawanyonyeshi ndama maziwa walileta mashine za kuzaga unga kwaajili ya ndama walikuwa Napika uji Wa ndama kisha wanaweka maziwa kidogo wananywesha ndama ili asimnyonye mamaye ili maziwa yapatikane mengi na huyo ndama apate protein na wanga KISA cha kula Ugali wale manamba walikuwa wanaona ule uji Wa ndama wanakunywa na kuwapa watoto wale wazungu wakakuta wanakunywa ule uji Wa ndama wakaulizwa ni kitamu wakasema ndiyo hivyo wakaanza kuruhusiwa kutumia badala ya chapati na viazi ,hakuna kabila linaloweza kusema kuwa ugali Wa mahindi ni asili yao laa ila ulezi mtama na mihogo na ndizi huo kuna makabila wana asili ya vyakula hivyo .Kwanini tunasema ugali wa mahindi Sii chakula kwenye kiini cha mahindi kikikauka sana hasa kikianza kuoza kinatengeneza toxic sumu ambayo inapunguza ule uwezo Wa ubongo ila ngano ina kirutubisho kinachokuza ubongo ugali Wa mahindi Sii hata chakula cha mwafrica kati ya nchi zinazokula ugali Wa mahindi hata hazifiki 20 wanaigaiga tu na duniani ugali Sii chakula kama mtu unauwezo haswa kutokuwapa watoto ni vyema usingewapa ila kutokana na ugumu Wa maisha tunakula kama itaweza kuwapa aina za viazi mihogo mtama ulezi mtama ngano soa maharage ndizi ni vyema sana
 
Sisi kigoma tulikuzwa na ugali wa muhogo,nyange na lowe je tuna akili tofauti na wasukuma?
Wapogoro/ wanyakyusa kyela chakula chao kikuu ni mchele je wana akili tofauti na wagogo?
Wakinga hula ugali wa ngano na mikate ya ngano aka mikate ya kikinga, je wana akili kulikp makabila mengine?
TUNA fish,ina omega 3,tatizo watu wa uchumi wa Kati tunanzisha Tax collection task force na kusahau formula nzima ya chakula sahihi Cha uchumi wa kati
 
We nae n mlevi tu..nani kakwambia ugali wanakula Waafrika wote?? Ni africa masharik tu ndo wanakula ugali ww..haswa Tanzania na Kenya... Uganda tu hapo ugali sio kivile wao wanakula ndiz na vyakula vingine kwa wingi.. acha ulevi ww boya
 
Yes mbegu za mahindi orijini yake ni South America huko wamarekani wakaja chukua na ku modified mbegu na kusambaza barani Afrika na kwenginepo dunia
 
Ukistaajabu ya musa utaona ya firauni.

Piga ua utacheza ngoma ya mabeberu tu

Hivi unajua kwamba Ugali uliletwa na mabeberu Afrika?

Someni mahindi waliintroduce kina nani.

Ndio maana ugali umegandisha akili zetu waafrica ugali sio chakula asilia kabisa sio chakula asilia.

Utasikia watu wakiwacheka wasiokula ugali kwamba eti hawana nguvu.....Wakati ukila ugali ndo mbaya zaidi...ndo maana Africa tumeshindwa kuchangamsha bongo zetu kwasababu ya ugali.

Usikute ndo maana hatujui kufikirisha bongo zetu maana before haijawa introduced africa ilikua vizuri sana tulikua tunanyanyuka kwa kasi lakini toka watu waanze kula mhh!ugali sio nzuri hata kidogo.

Utasikia mtu akitamba kwamba yeye ni mwafrika asilia ndo maana anakula ugali na akiona watu wa mabara mengine wasiokula ugali kama watu dhaifu na legelege wewe nani kakuambia?ugali ni product ya mabeberu sio chakula cha asili.
ugali wa mahindi ni chakula cha mifugo
tutumie mtama na ulezi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom