Hivi Tanzania hakuna watu waliosomea mipango miji?

Saskatchewan

Senior Member
Oct 16, 2011
148
21
Kila kukicha utasikia wamachinga wanakwaruzana na serikali kutokana na kufanyia biashara maeneo ambayo hayaruhusiwi. Hii inatokeaje wakati kuna watu wameajiriwa kwa ajili ya kazi hiyo? Kama wapo wanapatikana wapi? Mipango miji wanasababisha matatizo mengi sana yanayorudisha nyuma maendeleo!
 
Ndugu yangu wapo! Ila sijui niseme wapo ofcn kupokea mishahara tu bila kuingia field? Au hawapewi fursa za ku-apply fani yao ipaswavyo? Au kozi waliyoisomea huitumia kwa ishu zao binafsi? So many unanswered questions?
Machinga complex nako dah! Waliopo wanalalamika biashara haziendi... Waliopo nje wanahofia... Sijui ilijengwa kulingana na matakwa ya watu binafsi. Lisemwalo lipo.

Hivi niulize hii style ya siku hizi maghorofa yetu ndio ni mengi laaakiiinii yanafanana kama mabox kila ukutanapo nayo! Mitaa mingine ndio hata gari zikipaki tu shida, parking mjini miradi ya watu binafsi yaani full kero.
 
Wataalam wapo, tatizo maamuzi mengi yanafanywa na wanasiasa ( kina lusinde)
 
Wapo na wengine wengi tu wapo Bize kuijenga Botswana, Ma-city engineers wengi wa miji mikubwa Botswana walikuwa Watanzania
 
kila mwaka ARDHI UNIVERSITY inacheua graduates!..

Wataalamu hawa hakuna anaye wahitaji, kwani huu utaratibu wa bomoa boma unatusaidia kupata heshima Mitaani. Ukijifanya unajua jua kesho hapo ilipo nyumba yako inageuka sehemu wazi ya kuchezea watoto hivyo inafuata ile herufi isiyo maarufu kabisa bongo "X"
 
Wataalam wapo, tatizo maamuzi mengi yanafanywa na wanasiasa ( kina lusinde)
Masaki na O'bay kule waliko uziana nyumba za serikali, wamebadilisha matumizi. Msururu wa maduka, mabaa, ma'apartment marefu ma'supermarket, maofisi na machangu kibao ! Jamaa wapo wanaangalia tuu ! Hizo vurugu zilisababisha Kinje kupigwa ban na mahakama baada yao kugeuza nite klub !
 
Kama wapo hakuna kazi wanayofanya. Wanakula hela za walipa kodi bure tu! Hapa mtaani ninapoishi mkurugenzi wa jij4 ameruhusu soko ambalo ni kero kubwa! Inawezeka vp ukaruhusu soko kwenye makazi ya watu tena barabarani bidhaa zenyewe zinapangwa chini. Ushuru wanaotoza hatuoni unafanya kazi gani! Ningepata nafasi huko mipango miji ningewaondoa mara moja kuondoa kero hii!
 
Back
Top Bottom