Hivi serikali hii imelogwa?

MkimbizwaMbio

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
868
331
Taarifa kwa vyombo vya Habari

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inafuatilia kwa ukaribu taarifa kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Southwark mjini London, Uingereza kuiamuru Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza kulipa faini ya Paundi za kiingereza laki tano 500,000 kwa kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi za kihasibu kuhusu fedha zilizolipwa na kampuni ya BAE Systems kwa Mfanyabiashara Shailesh Vithlani wa Tanzania miaka mitano iliyopita.

Serikali ya Tanzania,kupitia Ubalozi wetu nchini Uingereza imeomba taarifa rasmi kutoka Serikali ya Uingereza kuhusu uamuzi huo. Serikali inasubiri kwa hamu kubwa kurejeshwa kwa bakaa ya Dola Milioni 30 za Kimarekani kama ilivyokuwa katika makubaliano kati ya Idara ya Serious Fraud (SFO) na Kampuni ya BAE Systems baada ya kuondoa faini ya kiasi cha Paundi Laki tano za Kiingereza ambazo kampuni ya BAE Systems imeamuriwa kuilipa Mahakama ya Southwark mjini London.

Mara baada ya kupata taarifa rasmi, Serikali ta Tanzania itachukua hatua muafaka ikiwa ni pamoja ni pamoja na urejeshwaji wa kiasi cha fedha kinachotakiwa kurejeshwa Tanzania kulingana na makubaliano kati ya SFO na Kampuni ya BAE Systems.

Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

22 Desemba, 2010
========================
Serikali imeshindwa kutoa tamko ni vipi itawachukulia hatua wale waliohusika na wizi huu badala yake inafuatilia pesa. Hatukuwa hata na wakili wa TZ kufuatilia kesi ile.
 
kufuatilia fedha sio kosa labda kama na wewe umelogwa. wakati tunajuliza maswali ya kukabiliana na wahusika fedha yetu ni muhimu
 
kufuatilia fedha sio kosa labda kama na wewe umelogwa. wakati tunajuliza maswali ya kukabiliana na wahusika fedha yetu ni muhimu

Uhalali wa kufuatilia fedha hii unautoa wapi wakati hutaki hata kuwachukulia hatua walioipoteza. Hamna hata aibu, Khaaa!!! Mnajiuliza? Acha kichekesho. Mnafanya kazi kwa kujiuliza? Hamna taratibu za kufuata ambazo zipo kisheria?. Ebu toa mfano mmoja wa kujiuliza.
 
toka lini wakachukuliwa hatua? hyo inakushangaza nini wangapi hawajachukuliwa hatua na pesa hazijarudishwa? walete pesa hapa mzee
 
CCM ina wenyewe!!kama mshiko alipata mkulu unategemea nini hapo??lazima kimya kitaendelea kuwa kimya!!
 
kufuatilia fedha sio kosa labda kama na wewe umelogwa. wakati tunajuliza maswali ya kukabiliana na wahusika fedha yetu ni muhimu

Utaendaje kudai hela wakati wahusika unasema hawana makosa? na wapo tuwanatamba mitaani
 
kufuatilia fedha sio kosa labda kama na wewe umelogwa. wakati tunajuliza maswali ya kukabiliana na wahusika fedha yetu ni muhimu

Ni muhimu kutibu chanzo cha tatizo kuliko kukimbizana na matokeo. Kwani kuna ugumu gani kuwachukulia hatua watu waliohusika?
 
kufuatilia fedha sio kosa labda kama na wewe umelogwa. wakati tunajuliza maswali ya kukabiliana na wahusika fedha yetu ni muhimu

Mkubwa nafikiri wewe ndo umelogwa ukalogeka haswa!!! Hicho kinachofanyika ni kama kupurura majani tu na kuliacha shina bila hata kuligusa!! Ili iweje??? Kesho lichipuke tena sivyo????? Muda wa watanzania kudanganyika ulishakwisha!!!!! Hadanganyiki mtu hapa na hizo "smoke screen" zenu????
 
kwani na nyie mnajiita kuwa mna serikali? ipi?
labda subirini 2015 mtapata
 
Back
Top Bottom