Hivi ni Magufuli alikuwa Katili au Vyama vya Upinzani ndio dhaifu? Mbona Kinana, Membe, Makamba na Sophia Simba wanadunda tu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,145
Kuna tofauti kubwa sana Kati ya Kuonewa na Wewe mwenyewe kuwa muoga

Ndio najiuliza Magufuli alikuwa Katili?

Vyama vya Upinzani Siyo dhaifu?

Viongozi wa Upinzani Siyo Waoga?

Upinzani wa Tanzania Siyo Biashara?

Awamu zilizopita tulishuhudia Watu wakitekwa na walipoachiliwa walirudi vilema pia tulishuhudia Mwangosi akiuawa hadharani na wengine pale Soweto Arusha walipigwa mabomu

Wapemba walihamia Shimoni Mombasa

Awamu ya Magufuli Mo alitekwa na kurudi salama salimini

Mzee Membe alikuwa anatamba atakavyo

Wazee Kinana na Makamba pamoja na zile Sauti lakini mwishoe wao ndio waliombwa radhi na Bashiru

Sasa huo Ukatili ni upi?

Mbowe aliitisha maandamano ya UKUTA Wafuasi wao wakaogopa tofauti na wenzake Kenya akina Raila Odinga
Sasa japo Upinzani Siyo Waoga na dhaifu?
 
Watanzania hawaachi kusema, yule Fisadi, huyo Katili mara anatutesa na huyu anaupiga mwingi kinafiki.

Huwezi kuongoza nchi ya mamilioni ya watu na ukategemea kumuimpress kila mmoja ifike mahali tukubaliane tu hii ndo nchi yetu hatuna pa kwenda zaidi, tutaibiwa, tutakopa hii mikopo ya kausha damu na kugawa malighafi zetu kama riba. Tutaishi na tutaishia tukiwaacha wajukuu zetu wanapambana kurejesha deni
 
Back
Top Bottom