Hivi ni kweli kazi yetu ni kunung'unika tu?

mapambano

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
535
14
Habari za Kitaifa
Mzindakaya ataka wabunge kuacha kunung’unika
Mwandishi Wetu, Dodoma
Daily News; Sunday,April 20, 2008 @00:03

MBUNGE wa Kwela, Chrisant Mzindakaya (CCM), amewataka viongozi na wabunge nchini kuacha kunung’unika kama wafanyavyo wananchi, badala ya kuchukua hatua ya kuondoa matatizo husika.

Akichangia maazimio manne yaliyowasilishwa juzi jioni bungeni ya Wizara ya Miundombinu, Mzindakaya alisema inaonekana wanachosomea viongozi ni shutuma tu na kunung’unika, bila ya kuwa na nini cha kufanya kuondokana na hali hiyo.

“Inaonekana kila mtu ananung’unika. Waziri Mkuu alikwenda pale bandarini akasema kweli hali ni mbaya. Wananchi wanalia; TICTS wanalia; wabunge wanalia; nani atafanya kazi wakati tunalia,” alisema Mzindakaya na kuongeza:

“Viongozi wananung’unika; tulichosomea ni critics, hakuna way forward; wabunge wanalalamika; viongozi wanalalamika. Nani ataiondoa nchi katika matatizo kama kila mtu analalamika. “Kule kwetu kuna mdudu anaitwa tengaruzi; yeye kazi yake ni kuzunguka hapohapo alipo ndani ya maji.

Nasi tumekuwa kama tengaruzi; tunazunguka hapohapo, hatuendi,” alisema mwanasiasa huyo mkongwe. Alisema viongozi wanapaswa kuchunguza kwa nini bandari ya Dar es Salaam imekuwa na msongamano na kupendekeza wabunge na wataalamu kukaa chini na kuchunguza msongamano huo.

Lakini pia alisema tatizo kubwa la Tanzania ni kutokuwa na miundombinu mizuri hasa ya usafirishaji kwa kutumia reli, na kwamba uchumi wa kutegemea barabara, utaiumiza nchi.

Maazimio yaliyofikishwa bungeni na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dk. Maua Daftari kwa niaba ya Wizara ya Miundombinu ni Itifaki ya Marekebisho ya Mkataba ulioanzisha Kamati ya Kudumu ya Kiserikali ya Usafiri wa Baharini mwaka 2006 na Mkataba wa Kuanzisha Wakala wa Uwezeshaji wa Uchukuzi wa Mizigo Ukanda wa Kati wa mwaka 2006.

Mengine ni kuridhia Mkataba wa Shirika la Kimataifa linalosimamia Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) na kuridhia Itifaki ya Mkataba kuhusu Masuala Maalumu yahusuyo vifaa vya ndege vinavyohamishika.

Wabunge wengine pia waliochangia maazimio hayo yaliyoridhiwa na Bunge jana asubuhi, walipendekeza kuimarishwa kwa bandari nyingine za Tanga, Lindi na Mtwara pamoja na miundombinu.

Mbunge wa Muheza, Herbert Mntangi (CCM), alisema wakati umefika wa Watanzania kuamka sasa na kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo kwa kutumia reli na bandari zilizopo.

Mbunge wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga (CCM), alisema Tanzania imejaliwa bandari nzuri, lakini imelala usingizi. “Hatuna injini, hatuna mabehewa, barabara mbovu. Bila ya kuwa na biashara katika usafirishaji, hatutafika,” alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Tandahimba, Juma Njwayo (CCM), aliitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuacha kuweka vikwazo kwamba kutakuwa na upotevu wa mapato kama mizigo itashushwa katika bandari ya Mtwara.

Wazo hilo la Njwayo liliungwa mkono na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi, aliyehoji wafanyakazi wa TRA wanachagua wapi pa kufanya kazi. “Eti mizigo itaporwa, itaibwa. Kwa nini tuliamua kujenga bandari,” alihoji Zambi.
 
Naona serikali na CCM ndio tengaruzi, tena hata tengaruzi ana afadhali maana anazunguka hapo hapo, wao wanarudi nyuma kwa kasi kubwa badala ya kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom