Hivi ni kwanini road license isilipiwe kwenye mafuta?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,066
40,725
Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.

=========================================================
UPDATE: (02/06/2017)
Hii ni moja ya michango bora katika Bunge linaloendelea sasa. Hamna gari inayostahili kulipia road licence kama haipo barabarani, cha ajabu wamiliki wenye magari yasiyotembea kwa ubovu ama ajali yangali yanachajiwa road licence na penalty juu na zaidi ya yote hata kama gari langu ni zima ila siko barabarani kwa muda tajwa ya nini nilipie road licence?

Wenye mamlaka jiongezeni kidogo tu, hamna gari itakayokuwa barabarani bila nishati na kadiri mtu atakavyotumia barabara ndivyo jinsi itakovyombidi kununua nishati husika na ndivyo jinsi atakavyolipia barabara na probably kipato cha serikali kitaongezeka zaidi.

Hongera mtoa hoja, hongera wabunge wote mwitikio wenu tumeuona, kazi kwenu serikali!!

=====

Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria inayoagiza tozo ya umiliki wa vyombo vya moto (road license) ili kuondoa kero kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo bungeni leo (Ijumaa) alipojibu swali la Dk Raphael Chegeni aliyetoa pendekezo hilo ili kodi hiyo iendane na matumizi halisi ya vyombo vya moto barabarani.

"Tozo hii ipo kisheria. Serikali imesikia mapendekezo ya wabunge na itaangalia namna nzuri ya kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo," amesema Dk Kijaji.

Wabunge wengi, akiwamo Spika wa Bunge Job Ndugai wamependekeza kufutwa kwa kodi hiyo inayowaathiri zaidi walioegesha magari kwa muda mrefu kutokana na ubovu au ajali.
 
Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Umenena sana hongera
 
Atakaetumia barabara au atakaetumia mafuta mengi ndio atalipa zaidi? Najua unajiuliza kivipi? Ni hivi toyota passo akiweka lita 10 approximately 20,000 atatembea zaidi ya 100km.

Range rover 4.4i V8 akiweka lita 10 atatembea chini ya 60km. Sasa nani katumia barabara zaidi?!
 
Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Una hoja ila matumizi ya mafuta ni zaidi ya vyombo vya moto; kuna generator, chain saw nk.
 
  1. Maafisa wa mapato na usalama barabarani wanapoteza muda mwingi kukagua stika barabarani wakati kama road license ingelipiwa kwenye mafuta wao wangeendelea na majukumu yao ya msingi yenye ulazima wa kufanyika manually, jambo la msingi hapa wangepaswa kusimamia na kuhakikisha kila kituo cha mafuta kinatoa receipt
  2. Yapo magari mengi ambayo hayalipii hiyo road licence kutokana na kufanya kazi pembezoni mwa miji ambako hao wakaguzi hawafiki, na mengine yanatembea usiku wakati hao maafisa hawako barabarani
  3. Kuna magari ya serikali yalishauzwa lakini bado yana namba za serikali, hayalipiwi road license na bado yanafanya kazi mitaani, mfano mmoja tu nilipata kuona lori moja lina namba za serikali na mlangoni limeandikwa Shule ya Sekondari Mazengo, japo sina uhakika kama hiyo shule bado ipo
  4. Kwa utaratibu wa kulipia kwenye mafuta mapato yangeongezeka kwasababu, kila chombo cha usafiri na mitambo kama matrekta yangechangia pato la taifa, kwa sasa hivi, bodaboda na bajaji hazilipii kabisa, na zipo nyingi na zinatumia barabara kwa kiasi kikubwa,
 
Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Wazo zuri sana bro lkn bei ya mafuta haitabiriki, soko lapanda na kushuka duaniani
Anyway tuwangoje EWURA wachangie humu
 
Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Ukisema road licence ilipiwe kwenye mafuta maanaake kwenye magari ya biashara ni kwamba road licence itakuwa inalipwa na walaji kama ni gari ya abiria hao abiria ndo watakaolipa hiyo road licence na kama ni gari ya mizigo mtumiaji wa hiyo mizigo ndo atakuja kulipa hiyo road licence.
Mfano mtu hana hata uwezo wa kununua baiskeli lakini akienda kununua nyanya ya kupikia anawekewa na gharama za mafuta(road licence) yaliyosafirishia hiyo nyanya.
Pia kumbuka kuna generators, mashine za kupump maji, mashine za kusaga mahindi huko vijijini e.t.c

Mimi naona hiyo itakuwa ni njia ya wenye vyombo vya biashara kuhamishia hizo gharama kwa mwananchi wa kawaida directly, manaake sasa hivi inawezekana bado mwananchi wa kawaida ndo analipia ila indirectly.
 
Labda pendekeza namna mbadala ya kulifanya hilo kwakuwa hivi sasa serikali inapoteza mapato mengi sana kwenye huo mfumo, kwa siku za nyuma ni sawa vyombo vya moto vilikuwa vichache na ilikuwa rahisi kuvibana na vikalipa lakini kwa sasa hivi vipo vingi na siyo vyote vinalipa, isipokuwa vile tu vinavyofika mijini na kutumia barabara kuu ndivyo vinalipa, jiulize kama serikali ingekusanya fedha ya road license kutoka kwenye pikipiki na bajaji ni fedha kiasi gani ingepatikana,

Anyway wafanya biashara wanafidia kilakitu kwa walaji wao, sidhani kama athari yake itaonekana kuwa kubwa kiasi hicho kwa kulipia road license kwenye mafuta , kinachopendekezwa ni mfumo wa kulipa unahamishwa kutoka upelekaji wa fedha bank kwenye akaunti za TRA na kuifanya kodi hiyo ijikusanye yenyewe kama ilivyo kwenye miamala ya simu na huduma zingine
 
Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Bila shaka yo yote hii ni hoja murua sana waziri wa fedha anapaswa kuizingatia katika bajeti ijayo!!
 
Nabadooo.mkapande.mwendokasi hizo passoodooo podokaa mpodoookoo.zote.MPAKA.MPAKA weekend
 
Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Ni njia mojawapo nzuri sana na nchi nyingi inatumia.
 
  1. Maafisa wa mapato na usalama barabarani wanapoteza muda mwingi kukagua stika barabarani wakati kama road license ingelipiwa kwenye mafuta wao wangeendelea na majukumu yao ya msingi yenye ulazima wa kufanyika manually, jambo la msingi hapa wangepaswa kusimamia na kuhakikisha kila kituo cha mafuta kinatoa receipt
  2. Yapo magari mengi ambayo hayalipii hiyo road licence kutokana na kufanya kazi pembezoni mwa miji ambako hao wakaguzi hawafiki, na mengine yanatembea usiku wakati hao maafisa hawako barabarani
  3. Kuna magari ya serikali yalishauzwa lakini bado yana namba za serikali, hayalipiwi road license na bado yanafanya kazi mitaani, mfano mmoja tu nilipata kuona lori moja lina namba za serikali na mlangoni limeandikwa Shule ya Sekondari Mazengo, japo sina uhakika kama hiyo shule bado ipo
  4. Kwa utaratibu wa kulipia kwenye mafuta mapato yangeongezeka kwasababu, kila chombo cha usafiri na mitambo kama matrekta yangechangia pato la taifa, kwa sasa hivi, bodaboda na bajaji hazilipii kabisa, na zipo nyingi na zinatumia barabara kwa kiasi kikubwa,
Swadakta!
 
Ni kweli kabisa na ndio njia iliyotumika miaka ya nyuma, INA maana serikikali itapata mapato mengi kuliko ilivyo sasa. Kila chombo kitachangia, pikipiki, generators, tractors, chain saw, boats, na kadha wa kadha. Sijui ni nani wa kumpa pendekezo hilo lipitishwe.
 
Kunakosekana link kati ya wadau na vyombo husika, labda ingekuwa rahisi kama kungekuwa na mijadala ya wazi kwenye vyombo vya habari ili kuizindua serikali juu ya jambo hili, nakumbuka zamani kulikuwa na vituo vya ushuru wa barabara ambavyo havikufanya vizuri, marehemu Kibona akiwa Waziri wa Fedha alikuja na mbinu ya kulipia tozo hiyo kwenye mafuta na ikaonekana kufanya vizuri zaidi,
 
Basi ingetengenezwa kipindi cha malumbano ya hoja na mada iwe hiyo, Na mada iwe hiyo, nadhani ingewafikia wahusika na jambo hilo lingefanyiwa kazi. Lakini sijui tunaanzia wapi kufanikisha jambo hilo.
 
Back
Top Bottom