Hivi mwenye akili timamu atawekeza Tanzania?

BondJamesBond

Member
Jul 6, 2011
85
60
Hii issue ya rushwa, umeme, politics kila sehemu, kodi za kutisha, bandari ambayo ni inefficient, mfumo wa kodi uliokaa kuwakandamiza wafanyabiashara na wawekezaji, mawasiliano duni..etc

hivi kweli mwenye akili timam ataweza kuwekeza pesa zake nchi hii?
 
Why not?
 
Hii issue ya rushwa, umeme, politics kila sehemu, kodi za kutisha, bandari ambayo ni inefficient, mfumo wa kodi uliokaa kuwakandamiza wafanyabiashara na wawekezaji, mawasiliano duni..etchivi kweli mwenye akili timam ataweza kuwekeza pesa zake nchi hii?
Tusilaumu kila kitu we are the one to make things proper,sasa wakulaumiwa ni nani,ni viongozi au ni watanzania?
 
kati ya jana au juzi rais wa kenya kibaki alikutana na jopo la wataalamu wafanye taathimini jinsi gani wanaweza ongeza bandari kwa ajili ya soko jipya la south sudan,watanzania wamelala na sijui kama nundu analijua hilo
 
Hii issue ya rushwa, umeme, politics kila sehemu, kodi za kutisha, bandari ambayo ni inefficient, mfumo wa kodi uliokaa kuwakandamiza wafanyabiashara na wawekezaji, mawasiliano duni..etc

hivi kweli mwenye akili timam ataweza kuwekeza pesa zake nchi hii?

Mkuu kwanini mwekezaji akatae wakati anapata faida kuliko anachikiweka?
Rushwa: tena ndio anashangilia cause bila rushwa huenda asingepata mkataba ambao unam-favor 100%
Umeme: faida aliyopata ni kubwa sana yaani anaweza aka-afford umeme wake mwenyewe
Politics: 10% inamfanya politicians wamlinde
Kodi za kutisha: Kodi kubwa ni kwako wewe wenyewe yaani wanapewa na miaka kadhaa ya bila kodi

Mkuu kwa hayo hapo juu hata kama nisingekuwa mzalendo na nina cash zangu za kutosha nisingesita kuvuna kwenye shamba la bibi
 
Hii issue ya rushwa, umeme, politics kila sehemu, kodi za kutisha, bandari ambayo ni inefficient, mfumo wa kodi uliokaa kuwakandamiza wafanyabiashara na wawekezaji, mawasiliano duni..etc

hivi kweli mwenye akili timam ataweza kuwekeza pesa zake nchi hii?

Ukianalyze yote hayo utagundua kwamba wenye nchi hiyo hawana akili timamu na ni wajinga na wajinga ndiyo waliwao... hivyo mwenye akili timamu anawekeza sababu anajua atakula tu maana wenye nchi ni wajinga.
 
Inji yetu inayoongozwa na sisimu wawekezaji wananufaika mno! Hata wao wanakili hilo
 
Umedadavua vizuri sana
Mkuu kwanini mwekezaji akatae wakati anapata faida kuliko anachikiweka?Rushwa: tena ndio anashangilia cause bila rushwa huenda asingepata mkataba ambao unam-favor 100%Umeme: faida aliyopata ni kubwa sana yaani anaweza aka-afford umeme wake mwenyewePolitics: 10% inamfanya politicians wamlindeKodi za kutisha: Kodi kubwa ni kwako wewe wenyewe yaani wanapewa na miaka kadhaa ya bila kodiMkuu kwa hayo hapo juu hata kama nisingekuwa mzalendo na nina cash zangu za kutosha nisingesita kuvuna kwenye shamba la bibi
 
Ndio.wanawekeza bcoz misamaha ya kodi ni mingi,wananchi wajinga na nirahisi kuwakaghai.then serikali haiwafuatilii.mfano wachina wanawapiga mpaka wakuu wa vituo vya polisi huko babati.
 
Labda kutokee tu Muujiza lakini. Uwekeza nchini mwetu, kwa hali ya hivi sasa, kwa kweli haiwezeka kwa sababu zifuatazo:

1. Kuwekeza gizani haiwezekani.
2. Wananchi wenye motisha iliovurugika hawaundi soko zuri.

3. Kwa kuwa tatizo la umeme umekwepo kwa muda mrefu sasa maana yake ni kwamba ajira zimepotea nyingi hadi sasa hivyo Watanzania hadi sasa hatuna ung'ao wala ushawishi kwa mwekezaji yeyote kwa kuwa KIPATO CHETU HADI HIVI SASA NI YA KUUNGA UNGA tu.
4. Maji kwa viwanda ni tatizo sugu lisilozungumzwa.

5. Mfumuko wa bei unafanya urahisi kununua malighafi kutoka kwetu kuzalishia tu kwingineko na wala si hapa nyumbani.
6. Picha ya serikali yetu hivi sasa tangu kashfa wa WIZI WA WAZI WA KURA Oktoba 2010 na hasira za wananchi dhidi yake hadi hivi sasa ni alama tosha ya kukosekana kwa udhabiti na ushwari wa utawala wa kisiasa nchini - ni bomu ambalo wawekezaji wanaliona kuweza kulipuka wakati wowote hivyo kuwatisha wasiweze kuja kuwekeza.

7. Kushamiri kwa rushwa ni ishara kubwa kwamba GHARAMA YA KUWEKEZA nchini mwetu ni kubwa ajabu bila urasmi wowote wala gharama hizo za kulipa RUSHWA kutoweza kuingizwa katika vitabu vya mahesabu ...

Hii issue ya rushwa, umeme, politics kila sehemu, kodi za kutisha, bandari ambayo ni inefficient, mfumo wa kodi uliokaa kuwakandamiza wafanyabiashara na wawekezaji, mawasiliano duni..etc

hivi kweli mwenye akili timam ataweza kuwekeza pesa zake nchi hii?
 
Watawekeza haswa WAHINDI kwa kuwa unakuja TZ mifuko mitupu unaondoka na utajiri wa kupindukia na kesi kibao za kudai fidia toka serikalini!
 
Back
Top Bottom