February Makamba
JF-Expert Member
- Jan 31, 2020
- 2,115
- 2,822
Venezuela!
Mungu anatumia vitabu/maandishi kufikisha ujumbe wake, iwe kupitia biblia au Quran.
Tatizo la hii njia ni kuwa inategemea utafsiri/enterpretation ya binadamu.
Tatizo la binadamu ni kuwa tunatofautiana uelewa na uwezo wa kutafsiri.
Unaweza kuchukua wanazuoni wawili wote wenye elimu kubwa ya dini, ukawapa kifungu kimoja na kila mtu akatoka na maana tofauti kulingana na uelewa wake.
Hii imesababisha kuwepo madhehebu lukuki, utasikia mara kuna wasabato, waluteri, walokole, wasunni, washia, wayahudi, wapentekoste nk. Nk.
Wengine wameenda mbali mpaka wanaitana wenyewe kwa wenyewe wapagani, makafiri, waliopotea nk. Nk.
Hii imepelekea mpaka vita kwa baadhi ya sehemu kisa tu utofauti wa kutafsiri vifungu vya Mungu.
Wengine wanasema Nguruwe kula ni ruksa na wengine wanasema alaye nguruwe anatenda dhambi na haendi mbinguni.
Sasa Mungu atachukua watu gani? Wanaokula au ambao hawali?
Kama atachukua ambao hawali, je hawa wanaokula kwasababu ya kutafsiri vibaya maandiko yake kutokana na upeo wa kibinadamu wana kosa gani?
Mungu anayejua kila kitu, hakuona kuwa akitumia vitabu atawapotosha binadamu wengi kulingana na utofauti wa upeo wao wa kutafsiri mambo?
Kwanini asingetumia njia bora zaidi kufikisha ujumbe wake? Au hajui hiyo njia? Au hana huo uwezo?
Au hakujua kuwa binadamu watatofautiana kutafsiri?
Na sasa kuna dini na amadhehebu zaidi ya 50, 000 duniani na kila moja linajiona lenyewe ndio lipi sahihi.
Sasa sijui Mungu atachukua lipi, au atachukua yote?
Atachukua wanaoamini Kutunza sabato ya jumamosi tu na wengine wote kuchomwa moto? Au atachukua wanaoamini kunena kwa Lugha na wengine wote kuchomwa moto?