Hivi mradi wa DARTS aliubuni nani? Was it the best/cheaper option

Huu ni mradi wa wakubwa ndo maana hata Magufuli hapigi kelele kwenye huu mradi japokuwa una makosa Mengi ya wazi,kwa mfano hii barabara ni nyembamba na endapo utaongozana na lori kwenye kona itabidi uliachie lipite otherwise utapata hasara,siku moja nilimuuliza injinia mmoja wa wizara ya ujenzi kwa nini mnaziba hii mifereji mikubwa ya maji kwenye barabara kubwa kama ya morogoro road na mkaweka makaravati ambayo kwanza ni ngumu kwa nchi zetu kufanya kazi vizuri kutokana na uchafu mwingi kwa hiyo kila wakati inaweza ikawa inaziba,akaniambia hii barabara imetungiwa sheria kabisa kwa hiyo kila kitu kipo binded anasema wakati inaanza kutengeneza waliomba service road zote zitolewe matuta ili magari yapite kiurahisi lakini mkandarasi aligoma kwa sababu sheria inamlinda na wizara haiwezi fanya chochote,,,kwa hiyo walitunga sheria hiyo ya barabara makusudi ili iwalinde wale vizuri.
 
Nimevutiwa na mwamko wa wengi kutaka kujua kama huu mradi utasaidia kupunguza msongamano. Hii ni topic pana na ni vizuri kuwa wengi mnatoa maoni yanayotoka moyoni na kwa nia njema. Kinachokosekana ni maoni a wataalamu wanaoijuia writeup ya huo mradi. Nianze kwa kukiri kuwa mimi pia sijaiona proposal ya huo mradi ila natoa maoni yangu tu kuongezea ya wachangiaji waliopita.

Ni vizuri tufahamu kuwa performance ya barabara yoyote inategemea factors tatu kubwa: roadway (geometric), traffic, and environmental conditions. Kama mbili zikibakia constant na moja kati ya hizo inabadilika, kwa mfano mvua ikanyesha (one of the environmental conditions), basi performance ya barabara itakuwa poor. Likewise, kama barabara ni ya wima (tangent), ukabadilisha sehemu yake ukaweka a sharp curve, au barabara iwe na mashimo (roadway factors), basi performance itapungua hata kama traffic and environmental conditions zitabaki constant. Sijaona michoro ya huo mradi ila ninafikiri kuwa watakuwa wameongeza at least one lane for BRT kwa hiyo one of the important geometric factors imeongezeka. Kuna wadau wanaongelea kupunguzwa kwa upana wa individual lanes ila nafikiri anamaanisha lane ya BRT sio pana. Kutegemea na design speed hawahitaji ziwe nene sana kwa sababu zimetenganishwa na normal traffic kutumia a barrier, preferably, a raised curb (sina uhakika sababu sijaona michoro).

Sasa tuje kwenye swali la msingi, je itapuguza foleni? Ni vizuri tukajua kuwa kupungua au kuongezeka kwa congestion ni swala la demand and supply. Hili la congestion ni complex na kulijibu kwa sentensi chache na fupi ni kutolitendea haki. Ukiangalia barabara moja peke yake, say, Kimara to Kivukoni, tuanze kwa kuangalia demand in terms of trips badala ya magari. Wapo wengi waliopo kwenye lower na middle class ambao hawatumii mabasi kwa sababu ya karaa za usafiri huo ulivyo. Kama mabasi yatakuwa na ratiba zinazoeleweka na yawe mazuri, kwa wengi wanaoenda ofisini au shuleni na kutokuwa na secondary trips, lower na middle class wengi watafanya modal migration from automobile to transit based for most of their trips. Kama ninaishi Kimara na kuna park-and-ride facility nzuri kwenye vituo vikubwa, kama time savings and fuel savings ni significant, nitabadilisha mode of transportation kirahisi. Watu wengi wakitumia mabasi hayo kwenda kazini, congestion itapungua kweye hizo barabara, hususani kwenye AM and PM peak kama watumiaji wa barabara nyingine hawatahaia hapo. Tatizo ni kuwa baadhi ya wanaoenda mjini kutumia barabara za mabibo through Kigogo au wanaokatiza Sinza kwenda Mwenge, wanaweza kuhamia Morogoro road (path of the least resistance). Ila watakaoamua kutumia transit watafika mapema kuliko wanaoendesha magari yao. Ikumbukwe kuwa kutakuwa na routes za express pia ambazo hazisimami kila kituo.

Naomba niwaulize swali. Kama hayo mabasi yakiwa mazuri sana na quality of service iwe nzuri na yawe efficient, hamuoni kuwa vipanya na madaladala mengine yatatoweka taratibu kwenye hizo routes? Madaladala yakitoweka au hata yakipungua morogoro road (change in traffic conditions) kwenye normal lane, traffic stream ita improve sana, hata automobiles zitatembea vizuri. Ukiondoa mabasi madogo u replace na makubwa yanayofuata sharia, na ukumbuke yatakuwa na prepaid cards option ambayo itafanya ridership iwe stable, traffic will improve.

Naomba pia nisisahau kusema kuwa BRT ni part of solution na sio the whole package. Ring roads zitasaidia sana kupunguza foleni za Dar. Hata hizo flyovers mnazozisema zinapunguza foleni kwenye junctions ila kukiwa na bottleneck downstream, utashangaa foleni itakuwa mbaya zaidi ya mataa, ila itachukua muda kulielezea hilo kwa urefu.

Kuna mmoja wetu hapa amesema kuwa kuna mhandisi wa wizara ya ujenzi amemweleza kuwa hata Magufuli hawezi kubadilisha chochote kwenye huu mradi. Tuache maneno ya mitaani. Magufuli hana ruhusa ya kubadilisha ujenzi wa barabara yeyote, yeye ni mwanasiasa, barabara inajengwa na wajenzi, si wanasiasa. Yeye kama mwanasiasa anasimamia policy, anaweza kupiga mkwara kama wako behind schedule au quality is visibly poor. Magufuli hawezi kubadilisha upana wa barabara kama unavyoelezea. In fact, hata contractor hawezi kubadilisha kilichopo kwenye mchoro, ni gharama sana kufanya design modification wakati wa ujenzi. Huu ujenzi wa hii BRT sio mrahisi kama nitakavyoelezea kwenye aya ifuatayo.

Kama una nyumba uliijenga wakati umeanza maisha, baadaye mambo yamekukubali unataka kuifanya iwe ya kisasa, uweke choo cha ndani, bathtub, ubadilishe interior and exterior design iwe kama nyumba za kileo zinazojengwa Mbweni, Ununio au Bahari beach, utakubaliana na mimi kuwa sio kazi rahisi na pia haitakuwa exactly the same. Kuna restrictions kwa sababu unachofanya ni retrofitting. The original design did not consider kuwa baadaye utakuwa na hela na kutaka nyumba yenye amenities za kisasa zaidi. Hicho ndicho kinachofanyika kwenye mradi wa mabasi yaendayo kasi ya Dar kwa sababu mabasi yaendayo kasi hayakuwa part of the original plan. Kuna constraints nyingi mno kubwa ikiwa right-of-way.

Sitaki kuwachosha na hoja zangu naomba niishie hapo kwa leo. Ninachowashauri tu ni kama unamfaamu mtu anayefanya kazi kwenye huu mradi muwaombe waje kuchangia hoja na tuwaulize maswali. Pia ijulikane kuwa huu ni moja ya miradi michache ya aina hii barani Africa na kama ukiwa executed vizuri una potential of proof of concept na wengi watakuja kujufunza kwetu.

Title ina swali, was it the best/cheaper option? Cheaper option, for this size of infrastructure project, don't go for a cheaper option, pursue the most effective and feasible option. Was it the best option? it is hard to tell!

Samahani kwa typos, for some reasons editor ya JF inanisumbua.


Asanteni.
 
Katika project management mradi una fail hata kabla haujaanza. Muda ule unapoisha inakuwa ni kujidhihirisha tu. Ile barabara iliyokuwepo haijamaliza miaka 20 inakwanguliwa na kuwekwa nyingine yenye mapungufu mengi tu ni failure mbaya na hasara kwa taifa. Walipashwa kujenga fly overs , kuchimba chini na kuweka madaraja kwenye junctions. Mfano ubungo, mwenge, tazara, fire, magomeni-flyovers. Tabata, buguruni, akiba, Kamata na kwingineko kwenye ukorofi upande mmoja ukachimbwa magari yapite chini na upande mwingine liwepo daraja magari yapite juu. Hili nalo limetushinda baada ya kujitawala kwa zaidi ya miaka 50!🙈

Wachimbe chini na chemchem za Dar? Si kila eneo linafaa kwa underground roads, surface water yenyewe yanakusumbueni huko chini mtaweka ngalawa?
 
Nasdaz, nini kinakufanya useme watu watafika mapema kazini au kwenye destinations zao? Unataka kuniambia mabasi ya DART yakifika kwenye makutano yataruhusiwa yapite kwanza magari mengine yasubirie? Umeshaelezwa mara nyingi kwamba tatizo la foleni Dar sio uwingi wa magari bali ufinyu wa barabara. Watu wanalazimika kutmia barabara moja pekee moro road kuingia mjini. Bara bara ya Mbezi- Tegeta mbona ipo tayari ni kuwekwa lami tu na hahitaji kubomoa nyumaba za watu? Ya mbezi kinyerzi mpka aiport mbona nayo ni lami tu! Ni ni hasa kimeifanya serikali mpka leo haijaona umuhimu wa kuborehs ahizo barabara? Kuhusu mjini kati km magomeni, karume, kifupi barabara zote ndani ya jiji zinatakiwa kuwa na fly ofer kwenye junctions. hakuna option nyingine.

Hii habari ya kusema DART lengo lake sio kupunguza foleni ni mbinu tu za kutaka kukwepa hoja. Hii la kusema lengo la dart sio kupunguza foleni limeanza kuzungumzwa baada ya watu kuhoji ni vipi huu mradi utakabiliana na kupunguza foleni kama junctions zitabaki zilivyo? Ukweli ni kwamba haya mbasi nayo yatajipanga kwenye foleni kusubiri trafiki aruhusu upande wao na sidhani kwamba kutakuwa na upendeleo! Feeder roads zipo nyingi tu ambazo ni mashimo tupu zingewekwa kwanza katika hali nzuri tatizo lingepungua kwa kiasi kikubwa. Unaposema kujenga feeder roads mpya ni gharama kwa sbabu inabidi watu wengi walipwe fidia ni kama unataka kusem huu mradi haukuhusisha watu kubomolewa nyumba zao na kulipwa fidia? Tatizo la huu mradi ni wa gharama kubwa ambao impact yake itakuwa ndogo. hayo mahela yangeweza kufanya kitu kizuri zaidi kukabiliana na taitizo la usafiri dar.

unajua BUS LANES zinavyotumika?? kama unajua usingeuliza hili swali.
 
Kwa kutazama tu huu mradi wamekosea sana. Mimì nilitarajia angalau wangeongeza barabara mbili pembeni kumbe la.
Na pia reli walizotumia kujenga hivi vituo ukizitandaza kwenye hiyo barabara ya zege zinatosha kabisa kinachobaki hapo ni kununua tu vichwa vidogo vya treni.
Tungewaomba Hata wale matajiri wetu wa viwanda vya juis na na soda aliotuambia Muhongo watununulie then warejeshewe kidogokidogo nadhan wasingeshindwa
 
siku zote huwa nasikitishwa sanaa na watanzania kwa kuwa na majibu mepesi kwa critical issues. Nyumba ya Maskini huwa haiishi kujengwa. hata Mradi haujaisha tayari tumelalamika haijatolewa tathmini ya kitaalamu tayari tumejitwika utaalamu na ujuaji kibaooo jamani hebu muwaache wataalamu wamalize kazi yao ndio tuje tuanze kuwaambia kasoro kutokana na output yao. inasikitisha project iko at 55% watu tushalalamika sana na kinachosikitisha hizi barabara hata miaka 3 hazijamaliza ila ukizitazama ni kama za miaka 5 uchafu matofali kubomoka yaani ili mradi tu yote hii ni sababu ya kukosa ustaarabu tu. hata tujenge flyovers tuweke reli nzuri na kila kizuri kama hatutokuwa wastaarabu sisi wenyewe matatizo yetu hayatoisha. sote mashahidi uvunjanji wa taratibu za undeshaji vyombo vya moto unavyochangia foleni tena kiasi kikubwa ila tunaona udogo wa barabara kama a big issue. tumejengewa uwanja mzuriiii lakini watu wanavunja viti wanaharibu miundombinu mwisho wa siku watakuja wanalalamika hapa uwanja hauna ubora. hebu hata hivi vidogo tulivyonavyo tuvitumie kwa utaratibu na ustaarabu. tusipo badirika wenyewe hata ijengwe flyovers sijui treni ya Umeme hamna kituu. na tujifunze kuwa wavumilivu subili kitu kikamilike then uliza wataalamu ni kwanini output imekuwa tofauti na ulivyotegemea

HUU MRADI HAUNA SULUHISHO LOLOTE HAPO DAR HALI ITAKUWA MBAYA SANA BAADA YA kufunguliwa maana watalazimisha kusimamisha magari pande zingine na kuruhusu yanayopita barabara iliyotengenezwa ili wajiridhishe kuwa wamefanikiwa
 
Mleta mada asante sana. Ni kweli huu mradi umeanguka kabla haujaisha. Mosi ni wembamba wa barabara na ujenzi unaobana magari kama ngombe wanapita kwenye josho, yaani ukibugi mambo Kimara kutoka nje au kugeuza ni mpaka Ubungo mataa. Jee gari zilizoopata ajali au zilizoharibika zitatolewaje?? Pili kuna maeneo ambayo mradi huu umeyatayarisha kuwa ya mauaji, mfano ule mwingiliano wa barabara pale Magomeni kwa Sheikh Yahya, mambo ni zig zag. Tatu ile kona yenye herufi S pale kimara mwisho kuelekea Mbezi, malori mengi yatajibwaga kule bondeni. Ziada ya hayo, eneo lote kuanzia junction ya NSSF pale Technical College hadi Posta ya Zamani hadi Ferry ni mchanganyiko maalumu. In conclusion, mradi huu ulianzia kwenye jibu (percent ya rushwa) kurudi kinyume nyume kwenda kwenye swali (Gharama ziweje). Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!

Hapo kwenye red umenichekeshaje?

Kwenye blue - you have said it all!

Huu mradi ni mzuri lakini haukutakiwa ufanyike sasa kabla, kwa mfano barabara ya Mandela na Morogoro haijapanuliwa kuwa na lanes tatu hadi angalau Mlandizi au kuhamisha malori ya mizigo nje ya mji. Kuimarisha barabara za pembezoni kama Mbagala-Airport, Majumba 6-Mbezi, Tangi Bovu - Morogoro road, n.k. Miradi hii mingine haina maslahi kama huu wa DART ndiyo maana umefanywa wa kwanza, tunaambiwa process za kupata operators zitakuwa transparent, lakini je ni wapi ambapo process haziko transparent na kwa nini IPTL, TICTS, dege la rahisi, etc zilipitishwa na nani hajui kuwa rushwa ilifanikisha madili hayo?
Wanasema pale Magomeni pekee kutakuwa na abiria 17,000 kwa saa hebu fanya mahesabu ya masaa 6 tu kwa siku utaona namna hii ilivyo biashara kubwa, na kibaya zaidi ni kuwa hizi nauli wao ndio wataamua baada ya kuridhika na ulaji wao (kuna watu wataniambia kuwa kutakuwa na bodi za kulinda walaji, je mbona Tanesco/Dawasco bado tunalipa service charge??)
 
Nimekuwa nikitafakari namna ambavyo nchi yangu inaendeshwa naomba kuwashirikisha GT wenzangu juu ya potential white elephant iliyotengenezwa kwenye DARTS.
- Je ni kweli DARTS ilikuwa ndiyo best option (in terms of cost, efficiency and priority)ya kupunguza msongamano Dar?
- Je hizi nyumba za kusubiria wasafiri zilikuwa zina ulazima wa kujengwa kwa gharama kama ilivyofanyika sasa
- Je namna ambayo barabara zimejengwa itapunguza foleni kweli?

Kwa maoni yangu (I stand to be corrected), DARTS haitapunguza msongamano na huenda ikaongeza, na kama kweli mradi huu ulijadiliwa kwa mapana yanayostahili then kuna umuhimu wa watu waliodhani huu ndio mwarobaini wa msongamano wa magari Dar(ni muhimu kuwafahamu ili tuweze kujiridhisha na weledi wao, au hata IQ zao)

Kama ningekuwa mimi ningeanza na kujenga fly overs kwanza, then barabara za pembezoni kwanza na kama pesa bado ipo ningeimalisha usafiri wa reli ndani ya jiji la Dar pamoja na kuimalisha uchukuzi wa mizigo kutokea bandari ya Dar kwa kuweka dry port kubwa Ruvu au Mlandizi.
Ukiziwekea lami barabara za Kinyerezi-Mbezi Lousi, Makongo Juu-Goba, Tangi Bovu-Morogoro Rd, Mbagala-Kipawa/Banana/Ukonga utapunguza msongamano kwenye barabara ndani ya jiji la Dar kwa kiwango kikubwa na kwa gharama ndogo kuliko huu wendawazimu wa DARTS.

Ulichoandika mkuu ni cha msingi, kuanzia hoja za maswali na namna ulivyoangalia baadhi ya barabara ambazo zingeweza kuimarishwa kwa minajiri ya kupunguza msongamano.
Binafsi natatizwa sana na nini ilikuw lengo kuu la mradi husika,na Je ? kulikuwa na utafiti kujua hitaji la huo mradi ? aliyefanya utafiti huo alikuwa ni Mtanzania au Mzungu? Je michoro ya Barabara na usanifu wake ulifanywa na Watanzania au na wazungu walituletea kwa utekelezaji tu ?
Kiini cha maswali yangu ni namna ambavyo mradi ulivyotekelezwa pasi na kuangalia mazingira yanayozunguka mradi, kiasi cha kuondoa kabisa mfumo wa kimawasiliano kwa njia ya barabara kwenye maeneo mengi ambayo yamepitiwa na mradi huo.
Lakini pia; kwangu napata shida kuamini kwamba huyu msanifu wa Mradi,aliwezaje kutengeneza vituo na madaraja ya Gharama kubwa namna ile wakati ambapo ingewezekana kuweka vituo vya gharama ya kawaida na kuimarisha maeneo mengine ya mradi hasa kwa waenda kwa miguu na waendesha Baiskeli ?
Kitendo cha kuweka madaraja ambayo kimsingi ni ubadhirifu tu, ghorofa mbili ili waenda kwa miguu wavuke barabara ? kwa nini isingewekwa tunnels watu wavuke barabara kwa kupita chini ambapo clearance ni kama mita 2 tu. Nilifikiri investiment iliyokuwa imewekwa kwenye daraja la manzese ingetufundisha kwamba kunahitajika namna nyingine ambayo ni bei nafuu kuliko kujenga madaraja ya gharama kubwa sana wakati ingewezekana kuvusha watu kwa gharama nafuu ili kuimarisha barabara hizo sehemu nyingine Muhimu kwa utatuzi wa kupunguza msongamano.
Napata shida sana kutafakari,mfano; pale ubungo ambapo kuna mtawanyiko kwa magari ama yatokayo mijini kulelekea Kimara,Mandela rd,sam nujoma rd. hakuna kilichofanyika kwa minajiri ya kupunguza msongamano pale,nilitegemea kungekuwa na lane ndefu za kuondoa magari yenye kuelekea pembeni iwe ni kwenda mandela au sam Nujoma na kwa kutokea pande zote. Mfano kungekuwa na lane inayopasukia kuanzia mteremko wa ubungo maji kwa ajili ya magari yanayoelekea mwenge,na nyingine kwa magari yanayo elekea mandella rd kutokea morogoro rd ili kubaki na clear lane ya magari yanayoendelea na Moro rd kuelekea manzese,vivyo hivyo kwa pande zingine,pale pangeongezeka lane 4 kila upande kuondoa msongamano pale Ubungo mataa. kilichofanyika hakitapunguza msongamano kwa kuwa hata kama utaruhusu magari ya moja kwa moja,kama mbele kuna magari ya kwenda mwenge ni lazima yatazuia.na hata kama yatenda pamoja kama pale Tazara,bado kuna delay kwa magari yanayochepuka kuzuia yanayokwenda moja kwa moja. Ingekuwa ni vema magari ya uelekeo tofauti yawekewe njia yake japo kwa km 1.

Mradi umetekelezwa kwa kiwango kikubwa pasipo kuangalia mazingira yanayozunguka mradi huo.
 
Nimekuwa nikitafakari namna ambavyo nchi yangu inaendeshwa naomba kuwashirikisha GT wenzangu juu ya potential white elephant iliyotengenezwa kwenye DARTS.
- Je ni kweli DARTS ilikuwa ndiyo best option (in terms of cost, efficiency and priority)ya kupunguza msongamano Dar?
- Je hizi nyumba za kusubiria wasafiri zilikuwa zina ulazima wa kujengwa kwa gharama kama ilivyofanyika sasa
- Je namna ambayo barabara zimejengwa itapunguza foleni kweli?

Kwa maoni yangu (I stand to be corrected), DARTS haitapunguza msongamano na huenda ikaongeza, na kama kweli mradi huu ulijadiliwa kwa mapana yanayostahili then kuna umuhimu wa watu waliodhani huu ndio mwarobaini wa msongamano wa magari Dar(ni muhimu kuwafahamu ili tuweze kujiridhisha na weledi wao, au hata IQ zao)

Kama ningekuwa mimi ningeanza na kujenga fly overs kwanza, then barabara za pembezoni kwanza na kama pesa bado ipo ningeimalisha usafiri wa reli ndani ya jiji la Dar pamoja na kuimalisha uchukuzi wa mizigo kutokea bandari ya Dar kwa kuweka dry port kubwa Ruvu au Mlandizi.
Ukiziwekea lami barabara za Kinyerezi-Mbezi Lousi, Makongo Juu-Goba, Tangi Bovu-Morogoro Rd, Mbagala-Kipawa/Banana/Ukonga utapunguza msongamano kwenye barabara ndani ya jiji la Dar kwa kiwango kikubwa na kwa gharama ndogo kuliko huu wendawazimu wa DARTS.

Mkuu,

Ninakushukuru sana kwa kuanzisha mada hii nzuri kabisa ya maendeleo ya nchi yetu!

Kwanza hivi tujiulize tatizo la foleni linasabishwa na nini hasa?

Tatizo la foleni linasababishwa na mambo mawili!
Mosi,ni kwamba barabara zote za michepuko ni mbaya hivyo magari yoote yanang'ang'ania njia kuu kufika kule yanakoelekea.

Pili,junction point haziruhusu magari kupita bila kusubiriana hivyo uelekeo mmoja unasubiria uelekeo mwingine uruhusu magari kwa muda Fulani na wenyewe ndio uruhusiwe(mataa)!

Je haya mambo mawili yametatuliwa kwenye huu mradi mpya!Jibu ni HAPANA!

Ni kweli kabisa gharama za ujenzi wa barabara hizi ni kubwa kuliko gharama ambazo zingetumika kutengeneza barabara ambazo zingesaidia kupunguza foleni.Kwani magari mengi yanapita njia kuu kwa sababu njia za mchepuko hazipitiki na ni mbovu kupindukia!Kwa hiyo kwa uhalisia gharama ambazo wangetumia kutengeneza barabara za mchepuko na madaraja machache(flyovers) kama ubungo,buguruni na magomeni,kwa hakika zisingekuwa kubwa kama hizi wanazojaribu kutumia sasa.

Watu wanasema kujenga flyovers ni gharama!SI KWELI!

Hivi unagharamika nini kuchimba morogoro road mita 8 chini kwenye kila junction ili kuruhusu magari yanayopita upande mmoja yasisubiri upande mwingine?

Mfano mdogo ni zile daraja ambazo treni zinapita kwa sie tunaoenda mikoani ambazo zinaruhusu magari na treni kupita kwa wakati mmoja!

Hivi ni gharama kiasi gani mtu atatumia kujenga daraja hizo?Hata mtu binafsi(tajiri) anaweza kuzijenga ,sembuse serikali!!!?

Kwa hiyo ningependa nikuhakikishie sio tu huu mradi ni kupoteza muda Bali pia ni kutengeneza bomu la foleni jijini ambalo litakuwa la kusimuliwa vizazi na vizazi!!!!
 
unajua BUS LANES zinavyotumika?? kama unajua usingeuliza hili swali.

Hapa tunaoneshana ujuaji au tunaelimishana? Nieleimishe basi. Wabongo bwana? Mimi nauliza swali nipate ufafanuzi badala ya kutoa ufafanuzi km unao unanipachika swali? Da haya bwana!
 
Nkwesa Makambo
Umejenga hoja nzuri sana na za msingi kwenye namna ya kupunguza foleni kwenye makutano - nimeipenda ile ya kutengeneza lane kwa mfano pale ubungo itokayo Kimara kwa magari yaendayo Mandela, lakini vile vile kuna option imetolewa na Deony juu ya namna ya kutengeneza fly over, hivi kwa mfano kama ikiwa badala ya fly over tukitengeza underground tunnels za kuvusha magari haiwezi kuwa nafuu zaidi?
 
Huu ni mradi wa wakubwa ndo maana hata Magufuli hapigi kelele kwenye huu mradi japokuwa una makosa Mengi ya wazi,kwa mfano hii barabara ni nyembamba na endapo utaongozana na lori kwenye kona itabidi uliachie lipite otherwise utapata hasara,siku moja nilimuuliza injinia mmoja wa wizara ya ujenzi kwa nini mnaziba hii mifereji mikubwa ya maji kwenye barabara kubwa kama ya morogoro road na mkaweka makaravati ambayo kwanza ni ngumu kwa nchi zetu kufanya kazi vizuri kutokana na uchafu mwingi kwa hiyo kila wakati inaweza ikawa inaziba,akaniambia hii barabara imetungiwa sheria kabisa kwa hiyo kila kitu kipo binded anasema wakati inaanza kutengeneza waliomba service road zote zitolewe matuta ili magari yapite kiurahisi lakini mkandarasi aligoma kwa sababu sheria inamlinda na wizara haiwezi fanya chochote,,,kwa hiyo walitunga sheria hiyo ya barabara makusudi ili iwalinde wale vizuri.
1. Kwanini Magufuri hapigi kelele?
Jibu ni kwamba mradi wa DART haupo chini ya Wizara ya Ujenzi bali upo chini ya ama Tamisemi au City Council kwahiyo Magufuri hapo hauhusiki!
2. Kwanini barabara ni nyembamba! Sijafahamu unazungumzia barabara ipi? Kama ni DART ni kwamba DART ipo chini ya mfumo unaofahamika kama BRT-Bus Rapid Transit! Kuna standards zinazopaswa kufuatwa duniani kote endapo unataka ku-adopt that kind of transport! Kwa mfano, angalia vile vituo... sehemu nyngi duniani utakuta vituo vyake vipo staili ile ile! Sasa linapokuja suala la wembamba wa barabara; moja ya subsystem ya BRT ni one busway... kwamba unajenga barabara ambayo itakuwa inapita gari moja tu bila kupishana! Labda kingine unachoweza kufanya ni kuongeza addition lane(s) kila upande na kama ilivyo kwa original lane, hakuna lane itakayokuwa na upana wa kuwezesha magari kupishana!!
3. Maelezo ya Engineer: Kama nilivyosema hapo juu, unapotaka ku-introduce BRT kwenye nchi yako au mji wako ni lazima uzingatie standards za BRT duniani! So, hawa wana standard zao kuhusu suala zima la barabara zenyewe, vituo, hadi vitu kama mitaro! Vituo kwa mfano... vituo vidogo vinatakiwa kuwa katikati kama ambavyo tunaviona pale Usalama n.k lakini vilevile sehemu ambazo zinakuwa na intersection kubwa unalazimika kujenga vituo vikubwa pembeni kabisa ya barabara... na ndio maana unaona kituo kikubwa pale Ubungo (kutokana na large intersection ya Ubungo Mataa) na Jangwani (kutokana na large intersection ya Morogoro/Kawawa Road!)
 
Mkuu udasa99,
Kwanza kabisa ingawaje umesema hujaona michoro ya DART lakini ulichozungumza ndio hasa kilichopo kwenye mradi huu! Kwanza, tukianza na hilo suala la daladala, lengo sio kupunguza daladala bali kuziondoa kabisa... which means, mradi ukishaanza hapatakuwa tena na daladala kwenye barabara husika! Wamiliki wa daladala wenyewe wanalifahamu jambo hilo na wameshapewa elimu na nini wanatakiwa kufanya to go on with the business! Hawa wanatakiwa kuunda kampuni, kwa wale wasio na uwezo mkubwa, wanaweza ku-join force. Lengo ni kwamba, kampuni hizi nazo ziwe zina-operate through DART lakini sio kwa daladala bali kwa mabasi maalumu yanayokizi vigezo vya DART/BRT!

Kuhusu ratiba maalumu ya mabasi! Unless wakiuke matakwa ya BRT lakini ratiba maalumu lazima iwepo! Kama nilivyosema hapo awali, BRT ni system ambayo eneo fulani la dunia likitaka kutumia mfumo huo basi ni lazima wafuate standards za BRT duniani! Moja ya standard za BRT ni ratiba... kama kituoni unatakiwa kukaa dakika moja, haijalishi kama umepakia au hapana, kama dakika moja imeisha ni lazima uondoke coz' nyuma yao kutakuwa na gari lingine linakuja!

Je, itapunguza foleni? Hii itategemea sana na wananchi wenyewe! Kama ulivyosema, ikiwa watu wata-switch from using private cars to DART, basi foleni inaweza kupungua ingawaje, kama ulivyosema, watu ambao hivi sasa hawatumii Morogoro Rd wanaweza kuhamia na hivyo kutoonekana tofauti! Lakini hata kama watu hawata-opt kuacha magari yao nyumbani bado watakaoathirika ni wao na wale wa DART hawataathirika coz' DART roads ni only kwa mabasi ya DART na hivyo kuondoa uwezekano wa msongamano ambao leo hii unasababishwa na daladala kusimama popote, malori, kupigana bao, kuchomekeana n.k!!

Hilo la Magufuri, si tu kwamba Magufuri ni mwanasiasa lakini pia mradi huu haupo chini ya Wizara ya Ujenzi! Kumbukumbu zimenitoka lakini kama haupo chini ya TAMISEMI basi itakuwa City Council kwa sababu, kimsingi huu si mradi wa barabara bali mradi wa mabasi yaendayo haraka!
 
Last edited by a moderator:
Dart sio white elephant!
Kimsingi nia ya mradi wa BRT ni kupunguza idadi ya gari binafsi zinazongia mjini.....hii inasaidia uchumi (kwa kupunguza matumizi ya mafuta). Usafiri wa umma ukiwa bora watu wengi watapunguza matumizi ya magari binafsi kuingia katikati ya jiji.
Mradi ukianza mtaona ubora wa usafiri wa umma....hii itawashawishi kupunguza kutumia magari binafsi!

Maendeleo halisi ni pale watu wenye vipato vya juu na chini wanapotumia usafiri wa umma bila tabu! Na sio kila mtu kutumia gari binafsi.
 
Dart sio white elephant!
Kimsingi nia ya mradi wa BRT ni kupunguza idadi ya gari binafsi zinazongia mjini.....hii inasaidia uchumi (kwa kupunguza matumizi ya mafuta). Usafiri wa umma ukiwa bora watu wengi watapunguza matumizi ya magari binafsi kuingia katikati ya jiji.
Mradi ukianza mtaona ubora wa usafiri wa umma....hii itawashawishi kupunguza kutumia magari binafsi!

Maendeleo halisi ni pale watu wenye vipato vya juu na chini wanapotumia usafiri wa umma bila tabu! Na sio kila mtu kutumia gari binafsi.

Hebu tuweni realistic, utazipunguza vipi gari wakati mizigo bado inachukuliwa Bandarini? Haya malori yatapishana vipi na hizo basi na je watu wanaoshushwa na DART watakwendaje kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na mradi?
DART imekuja ili kutatua tatizo la usafiri jijini Dar na si vinginevyo, na kama haitalitatua tatizo hili basi ni white elephant!
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa huu mradi wa mabasi yaendayo kasi ulipendekezwa kati kati ya miaka ya 90 na ilikuwa uanze kutekelezwa mwaka 1997.

Labda ungetekelezwa ontime pengine leo tungekuwa tunajadili alternative nyingine ya kupunguza foleni.

On the other hand huu mradi utasidia sana wale wasafiri wanaotumia usafiri wa public.
kwakuwa mabasi ya Darts yanatembea katika lane yao, hata kama yanapaswa kusubiri katika junction still hayatosubiri muda mrefu kusubiri taa ya kijani iwake compare na yale yanayosubiri kwenye chain ndeefu.

Haitopunguza foleni hata kwa asilimia 1 isipokuwa itawasaidia sana wanaotumia public transport.
 
Hebu tuweni realistic, utazipunguza vipi gari wakati mizigo bado inachukuliwa Bandarini? Haya malori yatapishana vipi na hizo basi na je watu wanaoshushwa na DART watakwendaje kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na mradi?
DART imekuja ili kutatua tatizo la usafiri jijini Dar na si vinginevyo, na kama haitalitatua tatizo hili basi ni white elephant!

Naona kwa makusudi hujaona kwamba nimeandika magari binafsi......
Sehemu kubwa ya magari yanayoingia mjini ni magari binafsi .....na inasababishwa na ugumu wa usafiri wa umma.

Hebu fikiri zaidi ya foleni ya ubungo......vipi kuhusu sehemu za kupaki magari mjini? Kwa mfano magari yakipita kwa urahisi ubungo, magomeni inakuaje? Vipi kuhusu selander na fire? Kote kutakua na fly overs? Huoni siku flyover ya ubungo ikianza basi foleni itahamia magomeni, fire na selander?
Sio rahisi tatizo la foleni likaisha dar kwa aina moja ya suluhisho....kuna njia nyingi za kupunguza msongamano dar, kati ya hizo nataja baadhi:
1. Kuboresha usafiri wa umma (brt ni mojawapo)
2. Kuboresha mipango miji (mji wa dar uko mno sehemu moja, angalao mlimani city imesaidia kutawanya sehemu za kufanya manunuzi. Tungekua na satelite cities ingesaidia zaidi....natambua kuna mipango ya kupanga na kujenga hizi cities)
3. Kuboresha miundo mbinu mikubwa (flyovers na barabara bora)
4. Kuboresha miundombinu midogo (njia za michepuko nk).
5. Kuboresha miundo mbinu ya usafirishaji wa mizigo mikubwa (reli na maji zitumike kusafirisha bulk cargo).
 
Back
Top Bottom