Katika project management mradi una fail hata kabla haujaanza. Muda ule unapoisha inakuwa ni kujidhihirisha tu. Ile barabara iliyokuwepo haijamaliza miaka 20 inakwanguliwa na kuwekwa nyingine yenye mapungufu mengi tu ni failure mbaya na hasara kwa taifa. Walipashwa kujenga fly overs , kuchimba chini na kuweka madaraja kwenye junctions. Mfano ubungo, mwenge, tazara, fire, magomeni-flyovers. Tabata, buguruni, akiba, Kamata na kwingineko kwenye ukorofi upande mmoja ukachimbwa magari yapite chini na upande mwingine liwepo daraja magari yapite juu. Hili nalo limetushinda baada ya kujitawala kwa zaidi ya miaka 50!🙈siku zote huwa nasikitishwa sanaa na watanzania kwa kuwa na majibu mepesi kwa critical issues. Nyumba ya Maskini huwa haiishi kujengwa. hata Mradi haujaisha tayari tumelalamika haijatolewa tathmini ya kitaalamu tayari tumejitwika utaalamu na ujuaji kibaooo jamani hebu muwaache wataalamu wamalize kazi yao ndio tuje tuanze kuwaambia kasoro kutokana na output yao. inasikitisha project iko at 55% watu tushalalamika sana na kinachosikitisha hizi barabara hata miaka 3 hazijamaliza ila ukizitazama ni kama za miaka 5 uchafu matofali kubomoka yaani ili mradi tu yote hii ni sababu ya kukosa ustaarabu tu. hata tujenge flyovers tuweke reli nzuri na kila kizuri kama hatutokuwa wastaarabu sisi wenyewe matatizo yetu hayatoisha. sote mashahidi uvunjanji wa taratibu za undeshaji vyombo vya moto unavyochangia foleni tena kiasi kikubwa ila tunaona udogo wa barabara kama a big issue. tumejengewa uwanja mzuriiii lakini watu wanavunja viti wanaharibu miundombinu mwisho wa siku watakuja wanalalamika hapa uwanja hauna ubora. hebu hata hivi vidogo tulivyonavyo tuvitumie kwa utaratibu na ustaarabu. tusipo badirika wenyewe hata ijengwe flyovers sijui treni ya Umeme hamna kituu. na tujifunze kuwa wavumilivu subili kitu kikamilike then uliza wataalamu ni kwanini output imekuwa tofauti na ulivyotegemea