Hivi mkoje nyie?...!

Ah shemeji mie tena? wala sidongoi pale penye ukweli ati. Ninakubaliana nawe kuwa kina mama wengi tuna tabia hii ila kama alivyosema dada Vera huwa kuna sababu behind yaani dada kuna ujumbe anataka kukufikishia but ndo hatujui njia sahihi!

Ila seriously kuna wanaume wanaonuna na usiombe ukakutana naye loh! Utajuta. Mie wangu alikuwa ananuna bila sababu asubuhi hadi usiku akirudi ni kuchuna tu hadi unachoka halafu nite kali ghafla bin vuu unasikia kono linateremshwa hazina!! Sijui wakoje wa namna hii!
Nimecheka saana, du.
 
Umarried men know about women than married men. Thats why they are not married!!
 
Kitu kimoja nilishaaswa.. nisijaribu kumwelewa mwanamke......so I stick to that...
 
MBU= MARRIED BUT UNHAPPY,

mkuu pole sana, kumbe ni kweli kabisa jina lako lilivyo Lol.
 
Mr. Mbu,

Kwa wale walio na wake wanalijua vyema hilo timbwili timbwili la wake zetu, iyo hali wengi wetu hutukuta, me hapo bado sija waelewa kabisa hawa wake zetu, wanafikili kununa ndio silaha yao ya kukufanya uwaogope au urudi nyumbani mapemaaaa! kumbe anapaswa kukuliza tu vizuri mume wangu kulikoni?? na atajibiwa.

Amakweli me hakuna jambo linalo nikela umetoka zako Job unakutana na na hilo timbwili timbwili huwa na juta kwanini nime wahi kuja home, wakuta ukirudi home bado yeye wife anataka umpe attention 100% awe anakusemesha na ikatokia hukumsikiliza ndio hapo unaunogesha ugomvi, sasa me ndie nimetoka job nimekukuta nategemea ndio unipe hiyo attention kwangu nikueleze mawili matatu ivi lakini jamaani wake zetu nao wawe wanatufikiriapo japo kwa muda kuwa mumewe kachoka anatakiwa kuliwazwa nae sio yeye atake kufanyiwa ivyo tuu,

Au utakuta jambo lingine ni pale wote mwafanya kazi ukiwahi rudi wewe utampokea vyema na utakuwa umeisha hata andaa chai ya jioni na mtaongea vyema au akukute nawe uko kwa bad mood utakiona cha mtemakuni naye anaweza kukubadilikia akawa yeye ndie mwenye hasira zaidi yako ati sasa hapo wajiuliza mimi ndio niko vibaya iweje wewe tena unibadilikie??

Au kunajambo jingine wengi wao wakitoka kazini na mkiwa mme pumzika usiku na labda mwaitaji kufanya tendo la ndoa wife wako atakuambia mimi nimechoka hiyo hali ipo toka Monday to Friday mazeee na huwatokea wengi, ati amechoka amefanya kazi nyingi sana au ana stress zake za huko job, siku nawe ukimjibu ivyo utanuniwa na utazushiwa kuwa una nyumba ndogo na maugonvi yanaanzia hapo sasa mimi huwa siwaelewi wao wanapenda tu wawe wanadekezwa tuuuuuuu au??

Si Love is both way jamani????au it a one way love only??
 
...unajua,

kuna wanawake wengine hawana jema wajameni. Mwanaume 8am-5pm ulikuwa unaumizana kichwa na mabosi huko kazini, badala ya kupata farijiko la akili ukirudi nyumbani ndio kwanza unakutana 'maza-hausi' kanuna nuna tu bila sababu...

Ukimuuliza " una nini leo?" anatingisha kichwa tu hakuna lolote...
Ajabu yenyewe 'mingine' utakuta imeudhiwa labda kazini, madonge yao wanakuletea wewe nyumbani. Hata ukijibaraguza na TV au na JF kwenye kona ya jicho unamuona na kila dalili za shari shari tuuu,... hasemi lolote almuradi kaamua 'kukuweka' uncomfortable as if hapo nyumbani unamuwekea usiku...

No wonder wanaume wengi wanaishia Grocery, Pub na sehemu nyinginezo kujiliwaza na marafiki, au farijiko la 'nyumba ndogo'...

Wenye roho ngumu kama mimi ndio inabidi kubanana nao tu hivyo hivyo, akinuna nami nauchuna vile vile...

Nyumba yangu kwanini aifanye 'kituo cha polisi' bana?

Pole mzee... wengine ndo staili zao za kuomba mdinyano...
 
Back
Top Bottom