Hivi Marekani inataka niamini kwamba imewashindwa Wasomali hawa?

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Wote tunaifahamu marekani jinsi ilivyo na ubabe na nguvu kijeshi.Kama ilivamia Iraq na nchi nyingine nyingi, kulikoni leo imeshindwa kuwamalizia mbali wasomali hawa wenye AK 47s.NATO nayo,nchi za jumuiya ya Ulaya vipi?Yaani wanataka tuamini kwamba wamewashindwa wasomali hawa?Nauliza hivyo kwa sababu hawa ndio wenye papara ya kila jambo.Hapana sio mjinga kiasi hicho.Hapa pana ajenda ya siri,ajenda ambayo matokeo yake halisi tutayaona hapo baadae.Tutakacho ona sasa ni matokeo ya muda mfupi tu,kupanda kwa bei ya mafuta,watu kuwa na wasiwasi kwa sababu ya kutokuwa na hakika ya maisha ya siku za usoni nk.nk. Kama tutakuwa hai tutashuhudia.This is conspiracy in a grand scale!Inawezekana kabisa kwamba haya maharamia yako kwenye payroll ya Wamarekani na wanapewa kila msaada na Wamarekani.
 
Kwa nini nchi za Kiafrika zisiende kuingilia kati na kuwashika hawa maharamia, na kwa nini mpaka tusubiri nchi za magharibi?
 
Kwa nini nchi za Kiafrika zisiende kuingilia kati na kuwashika hawa maharamia, na kwa nini mpaka tusubiri nchi za magharibi?

Mkuu ujui kwamba waafrika tumelemaa kwa misaada?Yani sisi kila kitu tunataka tufanyiwe tu!
 
Hakuna haja ya kuiita Marekani,maana kuiita Marekani ni sawa na kujidhalilisha,je kweli nchi zetu hizi wataweza kukabiliana na WASOMALI labda ingekuwa COMORO
 
....Americans walijaribu wakaishia kuwa targets,kuna msomali kaniambia huko ni kama jungle,mwenye gun ndio ana survive,na hawataki serikali wala nini maana kuna factions huko zinalima na kusupply bangi/unga dunia nzima,wengine wame control fishing coast unawapa pesa unapata mavuno yako,wengine wanacontrol upande mwingine wa ocean na kuruhusu makampuni ya magharibi kuja kumwaga chemicals zao kwa pesa nyingi sana,terrorist camps nako ndio mazoezi,they are making millions na hawataki kusikia any form of govt....ila nasikia wanauwana wenyewe kwa wenyewe ile mbaya,acha wamalizane labda ndio namna ya kumaliza Somali crisis!
 
what your talking is true 100% nilipata kuishi somalia mwaka mmoja na nusu, hiyo ndio hali halisi kabisa. Somalia haitakuja kuwa na amani hata siku moja
 
Back
Top Bottom