Hivi Kweli JK anjua anawaongoza watu gani?

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,770
553
Ndugu zangu wanaJF,

Naomba kufahamu, Hivi JK ni rais wetu kweli mbona mimi napata wasi wasi kutokana mambo ambayo yamekuwa yanajitokeza mara kwa mara;

1. Mfano Rais JK anasema yeye haifahamiu kabisa kampuni ya Richmond/Dowans na hata wamiliki wake hawafahmu kabisa, Lakini huku serikali yake inawafahamu na kuwapa hela nyingi namna ile ili walete mitambo ya kufua umeme. Mimi siamini kabisa kuwa haifahami, JK anaifahamu kampuni hii na kama kweli haifahamu basi amfukuze kazi Ngeleja, AG kwa kuwa wanataka kuilipa kampuni ambayo wao hawaifahamu na rais haifahamu na wananchi hatuifahamu.

2. Siku za hivi karibuni kumekuwa na migomo ya wafanyakazi, wanafunzi na wahadhiri; Rais anasema ni wanasiasa espe. CDM ndio wanawashawishi wanafunzi na wafanyakazi kugoma hivi mbona wafanyakazi na wanafunzi wanagomea mambo ya msingi ambayo wanayasema wazi wazi kwanini yasipatiwe ufumbuzi?
mfano kuna wanafunzi ambao mpaka sasa hawajapewa hela zao huu mwezi wa tatu je wafanyaje zaidi ya kuwaambia walipa kudi wa nchi hii?
Ukimwuliza JK atakwambia yeye hajui kwa nini wanafunzi wanagoma.

3. Kuhusu matatizo yanayoisumbua CCM kama vile Rushwa rais kama mwenyekiti wa CCM anasema atalimaliza kwa kuwaondoa baadhi ya watu kwenye chama ambao tunawafahamu na walijipambanua kama wapambanaji wa Ufisadi akidhani ndio tatizo la mpasuko ndani ya CCM, kumbe tatizo ni kina Rostam, EL, Karamage etc.

Kumbuka waTZ wengi ni masikini, kwa hiyo matatizo yao hayawezi kushughulikiwa na mafisadi kama kina RA, Manji na wengine bali na viongozi wao wanaowapenda kama mwakyembe, sita na wengine.

4. Je rais JK anafahamu anawaogoza kina nani?
 
Mkuu wa kaya anamaliza vibaya uongozi wake.....'' ALIPOINGIA KITINI ALIPOKELEWA KAMA MALAIKA.....LAKINI ANAPOONDOKA KITINI anaelekea atakataliwa KAMA MTUMWA ASIYE NA VAZI LA HARUSI !!!!!!!!!!!!!!1
 
Ndugu zangu wanaJF,

Naomba kufahamu, Hivi JK ni rais wetu kweli mbona mimi napata wasi wasi kutokana mambo ambayo yamekuwa yanajitokeza mara kwa mara;

1. Mfano Rais JK anasema yeye haifahamiu kabisa kampuni ya Richmond/Dowans na hata wamiliki wake hawafahmu kabisa, Lakini huku serikali yake inawafahamu na kuwapa hela nyingi namna ile ili walete mitambo ya kufua umeme. Mimi siamini kabisa kuwa haifahami, JK anaifahamu kampuni hii na kama kweli haifahamu basi amfukuze kazi Ngeleja, AG kwa kuwa wanataka kuilipa kampuni ambayo wao hawaifahamu na rais haifahamu na wananchi hatuifahamu.

2. Siku za hivi karibuni kumekuwa na migomo ya wafanyakazi, wanafunzi na wahadhiri; Rais anasema ni wanasiasa espe. CDM ndio wanawashawishi wanafunzi na wafanyakazi kugoma hivi mbona wafanyakazi na wanafunzi wanagomea mambo ya msingi ambayo wanayasema wazi wazi kwanini yasipatiwe ufumbuzi?
mfano kuna wanafunzi ambao mpaka sasa hawajapewa hela zao huu mwezi wa tatu je wafanyaje zaidi ya kuwaambia walipa kudi wa nchi hii?
Ukimwuliza JK atakwambia yeye hajui kwa nini wanafunzi wanagoma.

3. Kuhusu matatizo yanayoisumbua CCM kama vile Rushwa rais kama mwenyekiti wa CCM anasema atalimaliza kwa kuwaondoa baadhi ya watu kwenye chama ambao tunawafahamu na walijipambanua kama wapambanaji wa Ufisadi akidhani ndio tatizo la mpasuko ndani ya CCM, kumbe tatizo ni kina Rostam, EL, Karamage etc.

Kumbuka waTZ wengi ni masikini, kwa hiyo matatizo yao hayawezi kushughulikiwa na mafisadi kama kina RA, Manji na wengine bali na viongozi wao wanaowapenda kama mwakyembe, sita na wengine.

4. Je rais JK anafahamu anawaogoza kina nani?

Anafahamu anaongoza watu vilaza, majoga na yaliyojaa kusema mageuzi yataondoa amani inayodaiwa kurithiwa huku wakiwa hawajui hata nin maana ya amani
 
Kuna tofauti kati ya kiongozi na mtawala. JK anatawala, hajui hata chembe ya uongozi maskini ya mungu!
 
Kama anaweza kutembelea kwenye nyumba inayotarajiwa kubomolewa unategemea nini?

GO9G3102.JPG
 
Angalia hiyo picha hapo juu, afu tathimini watu aliokaa nao, Je ni wa jamii ipi na wanaheshimu sana mambo gani wanapokua katika hali hyo. Angalia miguuni mwao. Kila siku wanadai tunamwonea kwasababu ni mtu wa jamii fulani, Je hawaoni JK ni mtu tofauti na wao na anawatumia tu kisiasa ili kukwepa uwajibikaji
 
Anajua ndio maana mpaka leo na kesho yupo madarakani, anawafahamu anaowaongoza kua waoga, wajinga na hawewezi kuufyata! Kama si hivyo basi angewaheshimu na kuwatumikia kiuadilifu kwa haki. Angalia vitu vidogo tu wanafunzi vyuo vikuu wanalilia hali ngumu ya maisha wanakula mkon'goto wa FFU. Tujiulize ni vipi wataweza kusoma na kufaulu katika mazingira walionayo? Iwapo watz wataacha woga kwa kisingizio kisiwa cha amani basi jiti la makalio kila kukicha litaendelea kupekecha.
 
JK hahitaji kujua anaongoza watu gani kwani yeye siyo kiongozi, yeye ni mtawala aliyewekwa hapo na NEC wakishirikiana na TISS. Yeye anachojali jee washikaji zake wanapata manufaa ya yeye kuwa hapo alipo? Hayo mengine tunamuonea tu mtoto wa watu, siyo yaliyompeleka ikulu.
 
Kuna tofauti kati ya kiongozi na mtawala. JK anatawala, hajui hata chembe ya uongozi maskini ya mungu!

Mimi nafikiri kwa yanayotokea hata kuwa mtawala hafai, sijui tumweke wpi.
 
Mbona hajavua viatu? Inamaana anachakachua hata kwenye mambo ya msingi ya dhehebu letu? kwanini hawa wazee wetu wasimwambie?
 
Inamaana hata msikitini anaingia na viatu eti kwa sababu ye rais, hakuna hiyo
 
This is leadership
images

Haya waliotuuwa na wanaoendelea kutushikia kamba shingoni hawa...
images
 
Back
Top Bottom