Hivi kweli hakuna watanzania wenye sifa na ujuzi wa kibiashara wa kuiongoza TAZARA?

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
Nimesikitika sana kusikia kwamba wizara ya miundo mbinu ya Tanzania na wale wa Zambia wako china kujaribu kutafuta menejimenti ya kuendesha shirika.

Najiuliza swali moja, hivi kweli ktk watanzania milioni 36 hakuna wasomi wazuri wa kuweza kuiendesha TAZARA? Mbona Dk. Charles Kimei ameweza kuiendesha CRDB mpaka sasa ni benki bora Tanzania?

Tatizo la Tanzania nafikiri siyo wataalamu ila ni wanasiasa kuingilia maamuzi ya kitaalam. Sasa wanaJF sijui tufanye nini ili watawala wetu wawe na akili ya kutumia wataalam wetu na wasiwaingilie ktk maamuzi??
 
Hivi mbona hoja zenye maana siku hizi zinadoda jf?? au umakini umepungua siku hizi??
 
MKUU KWA UPANDE WANGU NAWEZA KUSEMA HAKUNA

SWALI KAMA HILI NILILIONA NIKIWA NNJE NASOMA LIKIULIZWA

KUHUSU ATCL..NILIKUWA WA KWANZA KUSAPOTI KUNA WATANZANIA WENYE UWEZO NA KULAANI SAA WASOUTH AFRIKA LEO HII NASEMA BORA MAKABURU..WALIOINGIA WAZAWA WAMEKULA HADI PESA ZA SPARE ZA NDEGE WANAKOSA KUNAVIONGOZI TENA HAPO????

WAACHENI TULETEWE HAO HAO WAZUNGU,WAHINDI,WAARABU WATUFUNDISHE KUISHI KWENYE UONGOZI KWA ADABU...WATANZANIA WENGI WALAFI ,WANAFIKI WANATAMAA....ONA

BOT;KILA MTANZANIA LIMWAMINI GAVANA WA BOT KWA UWADILIFU TUPO TULIOPINGA KUTEULIWA KWAKE TUKISEMA KAMA UCHAFU WA BALALI ALIUFANYA YEYE AKIWA NAIBU GAVANA ANATUHAKIKISHAJE AKUSHIRIKI;AU MCHANGA WA MACHO??
LEO HII GAVANA HUYU ANATHUBUTU KUTANGAZA MBELE YA WATANZANIA PUMBA ZAKE KWAMBA NYUMBA YAKE KWELI INAGARIMU BILLION 1,ANYWAY WATANZANIA HII HELA NI

1,000,000,000 YAANI SUFURI SITA HUYU BWANA ANAKUBALI KUJENGEWA NYUMA YA BILLION 1,HAWA MAnaibu gavana wanajengewa za sh ngapi???
uhuni mutpu
 
Tatizo sio watu wenye uwezo...tatizo ni kukosa uzalendo na tamaa ya kula hata kisicho cha kwako mwishowe makampuni yote yanafirisika
 
Ni mara elfu tumuajiri Mtu mwenye uwezo with no string Attached to run these companies.
hata kama atakuwa ni mjerumani sawa tu as long as he/she delivers.hata mie nimechoka na watanzania.umasikini wetu na uchu wa kuwa matajiri overnight ndio unatuponza,hata uwezo wetu unashindwa kuonekana.

si vibaya tukapewa vyeo vya kiutendaji-kama vile unaibu,etc ili tupokee amri kutoka kwa wakuu wetu watakaokuwa sio watanzania.hapo kazi zitaenda
 
Nimetolea mfano wa CRDB, mbona inaendeshwa na wazawa na ina mafanikio? Ni nini kinashindikana ktk mashirika nyeti kama TRC/TRL, ATCL, TAZARA n.k.?
 
Nadhani tatizo hapa ni protocol za serikali hizi mbili. kama unavyofahamu reli hii ni mali ya nchi mbili na nadhani walikubaliana hapo mwanzo kuwa makao makuu yawe tz lakini mdingi awe toka zambia
 
Nadhani tatizo hapa ni protocol za serikali hizi mbili. kama unavyofahamu reli hii ni mali ya nchi mbili na nadhani walikubaliana hapo mwanzo kuwa makao makuu yawe tz lakini mdingi awe toka zambia

Mkuu hoja yangu sijui kama umeisoma na kuielewa. Suala hapa ni kuwa mawaziri wa zambia na TZ wanakwenda china kutafuta menejimenti ya kuendesha shirika, swali ni je, hakuna watanzania au wazambia wa kuweza kuweka menejimenti thabiti yenye ufanisi? au siasa huwa zinaingilia mambo ktk mashirika yetu??
 
Nafikiri watanzania wamechoka kuwekewa MD toka Zambia....wanataka kipengele hicho kibadilike wajua JKN alikuwa fair kupita maelezo....jamaa tangu waanze kuwa MD kila siku wanatuburuza tu....watanzania wazalendo wapo ila wachache sana hata Zambia wapo pia wachache!!
 
Back
Top Bottom