Hivi kwanini CCM huwa wanapendwa sehemu zisizokuwa na maendeleo?

lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,496
1,035
Ndugu zangu naomba kuuliza ni kwanini maeneo mengi hasa vijijini wanaipenda sana ccm ilhali maeneo yanayowazunguka ni maskini wa kutupwa mliotembea mikoani nadhani hali halisi mnaijua yaani kuna maeneo kuanzia tuapate uhuru maji ya bomba hawajawahi kuyaona wala kuyanywa umeme ndio kabisaaa mbingu na ardhi ukienda kwenye huduma za afya ndio usiongee tukija kwenye elimu watu wanasomea chini ya mbuyu au kwa kifupi elimu sio lazima lakini hawa watu wanaipenda ccm balaa ni nini kinachowasukuma kuwa wakereketwa namna hii au ndio kutojitambua?
 
Kama ulikuwa hujui, huo ndiyo mtaji mkubwa kwa CCM. Huko ndiyo wanapopata kura za kumwaga, maana watu wa huko ni rahisi kuhongeka na kudanganyika. Ulishawahi kujiuliza hata siku moja, ni kwanini CCM hawapendi kutoa elimu ya uraia????
 
Ndugu zangu naomba kuuliza ni kwanini maeneo mengi hasa vijijini wanaipenda sana ccm ilhali maeneo yanayowazunguka ni maskini wa kutupwa mliotembea mikoani nadhani hali halisi mnaijua yaani kuna maeneo kuanzia tuapate uhuru maji ya bomba hawajawahi kuyaona wala kuyanywa umeme ndio kabisaaa mbingu na ardhi ukienda kwenye huduma za afya ndio usiongee tukija kwenye elimu watu wanasomea chini ya mbuyu au kwa kifupi elimu sio lazima lakini hawa watu wanaipenda ccm balaa ni nini kinachowasukuma kuwa wakereketwa namna hii au ndio kutojitambua?
kwenye miji yote ya maendeleo ccm haipendwi hila sehemu ambozo maendeleo hakuna ndio ccm inapendwa hii ni kwa sababu sehemu zisizokuwa na maendeleo watu wengi ni masikini sana hivyo wakipewa kiasi kidogo cha fedha hata kama sh.5000 kwao ni kubwa sana na ndio maana ccm hawapendi sana kupeleka maendeleo vijijini wanajua wazi ndio kwenye mtaji wao
 
Duh hii kali Dar Ilala CCM, Morogoro CCM na sehemu nyingi tu. Halafu wewe ni mkenya. Kichwa cha thread kimekutambulisha. Operation kimbunga unakuhusu.
 
Duh hii kali Dar Ilala CCM, Morogoro CCM na sehemu nyingi tu. Halafu wewe ni mkenya. Kichwa cha thread kimekutambulisha. Operation kimbunga unakuhusu.

Nataka nikuambie kitu laiti kama kiongozi wakati anaapishwa na kuapa kwa kutumia vitabu vitakatifu bila hata chembe ya hofu ya MUNGU angalikuwa MWENYEZI MUNGU angalikuwa anatoa hukumu za papo kwa hapo sura za viongozi wengi wa ccm tusingekuwa nazo sasa hivi .
 
Umasikini wa watanzania wa vijijini ndio mtaji wa kisiasa wa CCM!!

ccm.jpg
 
Ccm wanawarubuni ndg zetu kule vjijini, hata mawasiliano hakuna, radio hazishiki, tv ndo hizo wamezima... Kwa hiyo ukombozi utachelewa tu!

Hata suala la kuzima mitambo ya analoji na kuleta digital ni njia moja wapo yakutaka wananchi wa huko vijijini wasipate habari...

Hebu fikiria wanazima anaoji huko vijijini wakati wengine hata hiyo analoji hawajabahatika kuwa nayo!
 
ndugu zangu naomba kuuliza ni kwanini maeneo mengi hasa vijijini wanaipenda sana ccm ilhali maeneo yanayowazunguka ni maskini wa kutupwa mliotembea mikoani nadhani hali halisi mnaijua yaani kuna maeneo kuanzia tuapate uhuru maji ya bomba hawajawahi kuyaona wala kuyanywa umeme ndio kabisaaa mbingu na ardhi ukienda kwenye huduma za afya ndio usiongee tukija kwenye elimu watu wanasomea chini ya mbuyu au kwa kifupi elimu sio lazima lakini hawa watu wanaipenda ccm balaa ni nini kinachowasukuma kuwa wakereketwa namna hii au ndio kutojitambua?
ni ujinga wa watu wanaletewa mwanga wanakataa, kisa wamezoea giza,ndio kilichotokea kalenga,watu bado hawajitambui,nadhani shule pia ,au wamekunywa maji ya bendera na kujifanya hawanazo kichwani.
 
CCM wanapendwa kwenye vijijini kwa kuwa huko bado wako kwenye ujima, pia wanapendwa maeneo waliyofanikiwa kupanda mbegu ya udini
 
Kwa taarifa yenu hizi zero zinazozalishwa form 4 ni mpango wa CCM ili watu wasijitambue
 
Back
Top Bottom