Hivi Kiswahili ni kigumu hivi au watu tuna matatizo ya uelewa? Je, neno 'Udhaifu wa Bunge' ni sawa na 'Bunge Dhaifu'? CAG hajasema Bunge dhaifu

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,

Wakati tukiendelea kuisubiria hiyo tarehe 21/1/19 ifike, hakuna ubaya kama Watanzania tutaelimishana kidogo ni nini haswa CAG alichokisema kuhusu Bunge letu wakati akiwa nchini Marekani hadi watu kuhamaki, kukasirika, hadi kupandisha jazba na kuanza kuitana kwa kutishina kwa pingu?.

Kusema la ukweli, kumbe lugha ya Kiswahili ni kigumu kuliko wengi mnavyodhania, lakini pia ukiachia ugumu wa lugha ya Kiwahili, pia uwezo wa uelewa, comprehension pia ni tatizo kubwa katika elimu yetu. Unaweza usiamini, kama tukifuatilia pass rates za viongozi wetu wakuu wa taasisi mbali mbali wakiwemo wakuu wa mihimili walipata gredi gani katika somo la Kiswahili enzi zao walipokuwa
shule za msingi na sekondari, unaweza kushangaa!, hivyo natoa wito kwa viongozi wetu, hata kama unazungumza Kiswahili vizuri na unajijua kuwa unajua Kiswahili, lakini ukisikia mtu katamka neno fulani au jambo fulani ukahamaki, ni vema, ukamsikiliza tena kwa kituo na kwa umakini zaidi na ikibidi ukajiridhisha kwanza kwa kutumia watalaam wa lugha hiyo, kabla ya kuchukua hatua kama kuitisha press conferences za hamaki na jazba na kutishia watu kwa pingu!.

Hili ni bandiko la Swali, "Hivi Kiswahili ni Kigumu Hivi, Au Watu Wanamatatizo ya Uelewa?. Jee Neno "Udhaifu wa Bunge", Ni Sawa na "Bunge Dhaifu"?. CAG Hajasema Popote Bunge Dhaifu, Sasa Ameitiwa Nini Dodoma?!.

Naomba kwanza nikuwekee Clip ya CAG akihojiwa na Arnold Kayanda wa UN ili usikie wewe mwenyewe CAG alichokisema,


Kisha nakuwekea neno kwa neno
" Hilo ni jambo ambalo kimsingi ni kazi ya Bunge, kama tunatoa Ripoti zinaonyesha kuna ubadhirifu, halafu hatua hazichukuliwi, huo kwangu mimi ni udhaifu wa Bunge, Bunge linatakiwa lisimamie kuhakikisha kuwa pahali penye matatizo, basi hatua zinachukuliwa, sisi kazi yetu ni kutoa ripoti tuu, nahuo udhaifu, nafikiri ni jambo la kusikitisha, lakini jambo ambalo tunaamini, muda sii mrefu huenda litarekebishika" Mwisho wa kunukuu.

Sasa tujadiliane, jee kusema neno "Udhaifu wa Bunge" ni sawa na kusema neno "Bunge Dhaifu" kwa lugha adhimu ya Kiswahili?.


Neno "Udhaifu wa Bunge" unamaana gani?.
Neno "Bunge Dhaifu" lina maana gani?.

Twende Pamoja.
Neno "Udhaifu wa Bunge" na "Bunge Dhaifu" ni maneno mawili yenye maana mbili tofauti
Mtu akisema neno "udhaifu wa Bunge", anamaanisha ni katika baadhi tuu ya maeneo, hii ikimaanisha Bunge linaweza kuwa ni very strong katika maeneo mengine yote, lakini likawa ni dhaifu katika eneo moja specific tuu, la kushughulikia ripoti ya CAG. Na CAG, Prof. Asad alikuwa very specific kuwa Bunge limeonyesha udhaifu katika kushughulikia madhaifu yaliyobainishwa katika ripoti ya CAG, which is very true, wala hili halihitaji rocket science kubaini kilichosemwa na CAG ni ukweli mtupu.

Neno "Bunge Dhaifu" linamaanisha ni Bunge lote ni dhaifu. Mtu akisema "Bunge dhaifu", hapo kweli atakuwa amelidhalilisha Bunge na Spika au mtu mwingine yoyote, atakuwa ana haki ya kukasirika kuwa Bunge limedhalilishwa, limemedharauliwa, kwa sababu kauli hii inamaanisha Bunge lote ni dhaifu, hakuna jambo lolote la maana linachofanya, kitu ambacho sii kweli, Bunge letu ni imara sana, kila siku linajadili bajeti na kupitisha, linajadili miswada ya sheria na kuipitisha kuwa sheria, kamati za Bunge za kisekta kila siku ziko busy kazini kuisimamia serikali.

Sasa katika muktadha huo, ni wapi CAG ameliita Bunge Dhaifu?.
Na Jee kusema Bunge lina udhaifu katika maeneo fulani, hili ni kosa?. Bunge letu limekuwa ni Bunge malaika in such a way haliwezi kuwa na udhaifu wowote?. Ikitokea ni kweli Bunge limeonyesha udhaifu katika kushughulikia ripoti ya CAG, na ukauzungumzia udhaifu huu in public, kweli hili ni kosa la kuitiwa Kamati ya Bunge kwa kutishana kwa pingu?. Hoja kuu ya msingi sana kabisa ya alichokisema CAG kuhusu Bunge letu, jee ni kweli?.

Kuwa na udhaifu fulani ni jambo la kawaida mfano mimi nilipokuwa UDSM nilipata A somo la Prof. Shivji lakini nili supp somo la Dr. Tulia na ku carry somo la Prof. Kabudi. Kuniita nina udhaifu eneo fulani ni halali yangu.

CAG kasema "Bunge lina udhaifu", Spika kaelewa ni "Bunge dhaifu" kosa la CAG ni lipi?. Yaani CAG anaitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwa kulidhalilisha Bunge kwa kuliita "Bunge Dhaifu" wakati in reality CAG hajatamka "Bunge Dhaifu", bali "Udhaifu wa Bunge"

Yaani Bunge linamuita CAG kuhojiwa kwa kulidhalilisha Bunge, kumbe tatizo ni issues ndogo tuu ya misunderstanding, ya uelewa wa Spika, nashauri CAG aende tuu Dodoma akawaeleweshe hawa jamaa.

Mhe. Spika alikuwa Naibu Spika Bunge la Makinda, na alishuhudia jinsi Bunge lile lilivyoshughulikia Ripoti ya CAG, ajilinganishe na Bunge lake sasa limefanya nini kwenye kushughulikia ripoti ya CAG, halafu akiambiwa ukweli Bunge limeonyesha udhaifu, kitu ambacho ni kweli kabisa, hili kweli ni jambo la kukasirikia hadi kuita watu Dodoma kwa kuwatishia kwa pingu?.

Tanzania jamani ni yetu sote, ni ya Watanzania, sio Tanzania ya mtu fulani pekee, au Tanzania ni ya chama fulani pekee, au Tanzania ya taasisi fulani pekee, serikali yetu ni serikali ya Tanzania kwa Watanzania, Mahakama zetu ni Mahakama za Tanzania kwa Watanzania na Bunge letu ni Bunge la Tanzania kwa Watanzania, vitu vingine, tutangulize mbele maslahi ya taifa kwanza, tuache umimi, tuitangulize Tanzania mbele.

Namalizia kwa hili swali "Hivi Kiswahili ni Kigumu Hivi, Au Watu Wanamatatizo ya Uelewa?. Jee Neno "Udhaifu wa Bunge", Ni Sawa na "Bunge Dhaifu"?. CAG Hajasema Bunge Dhaifu! bali ameeleza udhaifu wa Bunge katika eneo moja, kitu ambacho ni ukweli kabisa, Jee wewe umeelewa nini kuhusu alichokisema CAG?. Kama alichokisema ni kitu cha ukweli kabisa, swali ni Jee huko Dodoma ameitiwa nini?!, na kama ataitika wito huu wa kiamri amri, ambao ni kinyume cha katiba, Jee inategemewa atakwenda kuomba msamaha kwa kuusema ukweli huu, uliowaudhi wakuu wa mhimili?.

Ila kabla ya kuhitimisha, naomba kutoa angalizo la "The Boss is Always Right" hivyo pamoja na ukweli wa udhaifu wa Bunge letu, msije kushangaa msema kweli ndio akaja kuadhibiwa kwa kuusema ukweli, halafu mdhaifu akashangiliwa kwa kuonyeshea yeye sio dhaifu!.

Nawatakia Jumanne Njema.

Paskali.
Update 03/04/2019
Hatimaye imethibitishwa pasipo shaka kuwa ni kweli Kiswahili ni kigumu, pale ambapo msema kweli anaadhibiwa, kwa kosa dogo la tafsiri sahihi ya lugha ya Kiswahili kwa katamka neno "udhaifu wa Bunge", likapokelewa amesema "Bunge Dhaifu", na sasa anaadhibiwa.
P.
 
Mkuu nakumbuka uliitwa kule kwenye kamati ya maadili nasikia mambo si mchezo, hapa yule jamaa mfupi anaweza kukupangia ratiba tena kwa kuwa umelitukana bunge na kulidhalilisha kwa kusema halielewi kiswahili.:D
 
Mkuu hata angesema Bunge ni dhaifu wao ni viongozi ilitakiwa wakae waangalie mapungufu yao na si kujiona miungu watu kuwa hawakosei wakati CAG kawakumbusha mimi nafanya kazi yangu hivi na wao kazi yao ni kuisimamia Serikali cha ajabu anaeambiwa asimamie Serikali kisa yupo karibu na Zuma anatisha watu kwa pingu na Zuma yupo kimya ina maana ni mpango walioupanga pamoja kutokana na madudu aliyonayo Zuma ili yafichwe Wananchi wasiyajue..
Na Zuma atakaa kimya atatumia watu wake wa Chini kumharibia CAG.
Tanzania mkitaka iendelee ni kuwa na Spika ambae atoki chama chochote na kazi aombe kwa CV zao sio kama sasa mkipata Wabunge wote ziro wanamchagua ziro mwenzao kuendesha vikao vya Bunge kila kukicha tutafungua sheria za Nchi na katiba vinasemaje huku wengine wakiondoka na Madini bure kabisa ambavyo ndio vilitakiwa visimamiwe na kujadiliwa haswa...
 
Nahisi kuna mengi nyuma ya pazia, hilo la udhaifu ni "jina tu la igizo".

Udhaifu ni sifa tu unaweza irekebisha au kuiondoa wala si tusi. Waungwana hukaa pembeni na kuyamaliza mapungufu yao bila munkari. La, kuna la ziada.

CAG ni mtu mstaarabu na mweledi wa kazi yake. Kuyasema yale hadharani tujue yamemkwaza. Mwitikio wa Spika si wa kushtusha sana ana 'mori'. Hata hivyo nguvu na vitisho alivyotumia vina ujumbe nyuma ya pazia.

Drama hii ikiendelea si ajabu mkasikia Prof akajiuzulu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuliko kutumia hela nyingi kuitisha kamati na kuilipa nashauri kila anayeitwa kamati ya maadili wanakutana uwanja wa Taifa yeye na Ndugai halafu wanachapana bakora za kichwa kwa zamu atakayezimia hoja yake inatupwa kapuni.

Na tukio liwe live.
 
Back
Top Bottom