Hivi jamani kwanini wanawake hamna mapenzi ya kweli?

Jamani wana JF nimekuja hapa kwenu kuwaeleza hili swala na pia kuomba ushauri wenu kutokana na hili sakata lililonikuta la kusalitiwa na mpenzi wangu.

Jana usiku wakati nikiwa nafanya kazi zangu mbali mbali niliamua kuingia katika mtandao wa facebook na kuhack account ya facebook ya mpenzi wangu ili kujua kama kweli ananipenda au napoteza mda wangu tu kumpenda mtu ambaye hapendeki. Niliamua kufanya hivyo baada ya kudanganywa password ya e-mail yake kipindi cha nyuma kwa kisingizio eti aliogopa kunipa e-mail yake kwa sababu eti aliwahi kumpa mpenzi wake wa nyuma e-mail yake na matokeo yake mpenzi wake akawa anaitumia e-mail yake kwa kumtuhumu makosa ambayo hajayatenda kwa hiyo aliogopa pengine na mimi ningemfanyia hivyo. Kwa jinsi nilivyompenda niliamua kumsamehe na kuendelea na uhusiano wetu kama kawaida.

Sasa baada ya kufanikiwa kuhack katika account yake ya facebook nilianza moja kwa moja kwa kukagua profile yake, kutizama picha zake na mwishoni niliingia katika inbox yake na kuanza kusoma message zake. Jamani message nilizozikuta huko sitaki hata kusema. I wish kama ningekuwa na uwezo ningewawekea hapa ili na nyinyi mzione. Nilipomueleza na kumtaka aniambie ni kwa nini ameamu kunifanyia hivyo na kuamua kunisaliti na wanaume wengine tena wa facebook akanijibu na kuniambia kuwa eti alifanya vile kwa sababu eti wanaume wote wapo kuumiza tu ila hakumaanisha kila alichokuwa anasema katika message za facebook pia akaniambia kuwa japo aliumizwa ila alipokutana na mimi alinipa moyo wake wote cuz alinipenda sana na aliamini kuwa niko tofauti na wanaume wengine ila kiukweli hana mwanaume mwingine zaidi yangu.

Kitu kingine nilichogundua ni kuwa huyo mpenzi wangu ana e-mail address ila mimi aliniambia e-mail address yake mmoja tu. Mimi nilihisi kuwa anazo mbili na baada ya kugundua hivyo nilimuuliza kuwa e-mail address ........ ni ya kwako??? akaniambia hapana na ya kwake ni hiyo aliyonipa kumbe hiyo e-mail ambayo alinificha ndiyo hiyo ambayo anaitumia facebook. Sasa leo baada ya kugundua hilo nilipomuuliza kwa nini alinidanganya kipindi kile alikana kabisa kuwa hakusema hivyo.

Kwa jinsi nilivyo kasirika na kuumia moyoni nimeamua kuchana naye ingawa kiukweli nilimpenda sana msichana huyu, nilimpa kitu kitu alichohitaji, nilimpa mapenzi yangu yote, nilimpa hata vile visivyohadithika lakini bado mtoto wa kike haonyeshi kuridhika kila mwanaume anataka awe wake. kama nilivyosema hapo mimi nimeamua kuchana na nimeshamtakia wazi ila yeye bado ananiomba msamaha anasema eti hawezi kuishi bila mimi. Nifanyeje jamani?

aiseee! mkuu we ni balaa,nipm basi maujuzi yako ya kuhack facebook accounts na e-mails.
 
Kijana jambo la muhimu ni kuacha kuwachanganya wanawake wote na huyo wako. Si unajuwa kila binaadamu ana tabia yake? Huyo wako ana tabia ya kutokuwa na mapenzi ya ukweli tabia ambayo hata sisi wanaume baadhi yetu tunayo.
Usife moyo na unastahili pongezi kuwa umekuwa katika right track ya mapenzi kwa kuamuwa kuondoka na kwenda mbele pale rafiki ulienaye hatimizi matarajio yako.
Si alikwambia kuwa alikuwa na mpenzi kabla (pengine wapenzi)? Inaonyesha hawakutimiza au hakutimiza matarajio ya mapenzi, basi nawe nenda hatuwa nyengine ukiwa mwerevu zaidi usije ukaangukia katika mitego kama uliyoipata kwa huyo msichana. Safari ya Mapenzi ni sawasawa na safari nyengine lazima ufike ulipopatakla ndio utulie!
 
yaani kuflirt na wanaume wengine ndio kisa cha kumuacha?
mie hata nikiolewa sitaacha kuflirt,unless umenikuta kitandani na mtu tunafanya mapenzi ndio nitakuelewa ukisema unaniacha sio upuuzi wa kusoma messages...............................

unahack vipi account facebook embu nifundishe nataka kuhack account ya mtu lol,am serious lol
Dada Neema nini hasa faida ya kuflirt na mwanamume wakati ukiwa na rafiki? Je Rafiki yako akiruka ruka na kimwana hapo mtaani na kutangaza uchumba utafurahi?
 
Mambo mengine ni kujitakia presha kama siyo BP..achana na email mimi hata simu ya mpenzi wangu imekaa hapo pembeni siigusi na yes ana marafiki wa kike, ma-X sijui Y na kadhalika..sasa nikianza kufuatilia kila kitu nitakuwa ana amani kweli ya roho? na yeye vivyo hivyo kwangu, ni kuwa na imani mtu anakupenda na kuheshimiana.

Pole kwa uliyoyakuta..kama umeamua kumuacha basi usiumie roho mana ni uamuzi uliodhamiria.

Nafikiri kuna kasababu cha kumwachia afanye anavyotaka. Kuwa muwazi dada angu aidha unaogopa kumuuzi au unaogopa asije akakuingilia kwenye mchezo wako. Hakuna kitu gentlmen agreement katika ndowa isipokuwa kuna kajambo kati.
 
Ukitaka kuachana na mpenzio/mumeo we anza kupekenyua simu na sijui e-mail na madudu gani sijui. Wengi wanaofanyaga hivyo huwa wameshachoka kuishi na wapenzi wao na hivyo wanatafuta chanzo cha kulianzisha ili kieleweke. N kweli ndugu umekipata ulichokuwa ukikitafuta.

Kama wewe ni mtaalamu wa mapenzi kiasi cha kumwachia mpenzi wako afanye hayo madudu huku ukijuwa hasa kuwa anayafanya basi ni wa kubarikiwa. Bahati mbaya kijana ni mgeni wa mapenzi na akihisi kuwa mapenzi maana yake kuachana na wengine kabisa! Ndio maana alipoambiwa mwanzo kuhusu mpenzi wa mwanzo kwa uanagenzi wake aliona kuwa yaliisha, kumbe Sivyo!
 
Nyie wote wala hamtofautiani!mwanaume yoyote anaejiamin hawezi kurist mahusiano yake kwa kufatilia maupuuzi ya huko fb,na mwanamke makini hawezi kuendekeza kuchati na vivulana vya huko fb!mkikua mtaacha!katafute mpya ila ujiandae kukumbana na vituko vyake ambavyo huvijui!

Naona usitusemee! Kijana yuko sawa kabisa kwani mmoja anapodanganya maana yake ipo kasoro na kasoro ina maana jambo sio sawa .
 
Hasira hasara mkuu! Jipe muda kwanza wa kutafakari na yeye mwenyewe akupe some more details, usichukulie kitu haraka namna hiyo....tuliza akili ndugu uamue kwa uhakika!!

Inaonyesha tangu mwanzo alibeba mzigo si kadiri yake. Ametambuwa usimrejeshe nyuma utamvunja shingo!
 
Kijana jambo la muhimu ni kuacha kuwachanganya wanawake wote na huyo wako. Si unajuwa kila binaadamu ana tabia yake? Huyo wako ana tabia ya kutokuwa na mapenzi ya ukweli tabia ambayo hata sisi wanaume baadhi yetu tunayo.
Usife moyo na unastahili pongezi kuwa umekuwa katika right track ya mapenzi kwa kuamuwa kuondoka na kwenda mbele pale rafiki ulienaye hatimizi matarajio yako.
Si alikwambia kuwa alikuwa na mpenzi kabla (pengine wapenzi)? Inaonyesha hawakutimiza au hakutimiza matarajio ya mapenzi, basi nawe nenda hatuwa nyengine ukiwa mwerevu zaidi usije ukaangukia katika mitego kama uliyoipata kwa huyo msichana. Safari ya Mapenzi ni sawasawa na safari nyengine lazima ufike ulipopatakla ndio utulie!

asante kwa ushauri wako mkuu.
 
Nafikiri huyo ni cha mtoto, angehack za wengine angepata stroke na coma juu....maneno tu hakuna hata matendo....lol

Msamehe huyo dada na wapo wanawake wengi wamekata tamaa ya kupata wanaume waaminifu na matokeo yake hadi akuamini sana ndo atatuliza moyo,akili,mwili na roho yake kwako.....utaacha wengi kwa mwendo huo wa ku-hack!

Nomba unielewe dada yangu, mimi sikuwa na lengo la kuhack e-mail yake kama asingenidanganya tokea mwanzo. kunidanganya kwake ndio kulipekea kuhisi kuwa kuna kitu ambacho anakifanya nyuma yangu ambacho mimi sikifahamu ndio maana nikaamua kuchunguza ili kujua nini kinaendelea na ndipo nilipochukua hatua ya kwanza ya kuhack account yake ya facebook nakuchunguza kinachoendelea huko. Na hiyo ilikuwa ni step ya kwanza tu. nilikuwa na mpango wa kutrack hadi simu yake ili nijue kila anachofanya katika simu yake. Ila namshukuru Mungu nimeujua ukweli kabla sijaumia zaidi maana kama ningetrack simu yake sasa hivi ningekuwa nimelazwa muhimbili.
 
kwani mimi ndo nimesema hivyo?
Nimesema alipize?
No,no,no....Hapana,nimeandika kutokana na ulivyouliza;'kwani wanaume wana mapenzi ya kweli?',nilimaanisha kama mtu atakataa kuing'arisha tabia yake eti kisa ya mwenzie haing'ai si busara.Wanawake msiangalie upotofu wa waume zenu halafu na nyinyi pia mkaamua kupotoka.
 
Usemayo ni kweli kabisa mkuu
 
Jamani wana JF nimekuja hapa kwenu kuwaeleza hili swala na pia kuomba ushauri wenu kutokana na hili sakata lililonikuta la kusalitiwa na mpenzi wangu.

Jana usiku wakati nikiwa nafanya kazi zangu mbali mbali niliamua kuingia katika mtandao wa facebook na kuhack account ya facebook ya mpenzi wangu ili kujua kama kweli ananipenda au napoteza mda wangu tu kumpenda mtu ambaye hapendeki. Niliamua kufanya hivyo baada ya kudanganywa password ya e-mail yake kipindi cha nyuma kwa kisingizio eti aliogopa kunipa e-mail yake kwa sababu eti aliwahi kumpa mpenzi wake wa nyuma e-mail yake na matokeo yake mpenzi wake akawa anaitumia e-mail yake kwa kumtuhumu makosa ambayo hajayatenda kwa hiyo aliogopa pengine na mimi ningemfanyia hivyo. Kwa jinsi nilivyompenda niliamua kumsamehe na kuendelea na uhusiano wetu kama kawaida.

Sasa baada ya kufanikiwa kuhack katika account yake ya facebook nilianza moja kwa moja kwa kukagua profile yake, kutizama picha zake na mwishoni niliingia katika inbox yake na kuanza kusoma message zake. Jamani message nilizozikuta huko sitaki hata kusema. I wish kama ningekuwa na uwezo ningewawekea hapa ili na nyinyi mzione. Nilipomueleza na kumtaka aniambie ni kwa nini ameamu kunifanyia hivyo na kuamua kunisaliti na wanaume wengine tena wa facebook akanijibu na kuniambia kuwa eti alifanya vile kwa sababu eti wanaume wote wapo kuumiza tu ila hakumaanisha kila alichokuwa anasema katika message za facebook pia akaniambia kuwa japo aliumizwa ila alipokutana na mimi alinipa moyo wake wote cuz alinipenda sana na aliamini kuwa niko tofauti na wanaume wengine ila kiukweli hana mwanaume mwingine zaidi yangu.

Kitu kingine nilichogundua ni kuwa huyo mpenzi wangu ana e-mail address ila mimi aliniambia e-mail address yake mmoja tu. Mimi nilihisi kuwa anazo mbili na baada ya kugundua hivyo nilimuuliza kuwa e-mail address ........ ni ya kwako??? akaniambia hapana na ya kwake ni hiyo aliyonipa kumbe hiyo e-mail ambayo alinificha ndiyo hiyo ambayo anaitumia facebook. Sasa leo baada ya kugundua hilo nilipomuuliza kwa nini alinidanganya kipindi kile alikana kabisa kuwa hakusema hivyo.

Kwa jinsi nilivyo kasirika na kuumia moyoni nimeamua kuchana naye ingawa kiukweli nilimpenda sana msichana huyu, nilimpa kitu kitu alichohitaji, nilimpa mapenzi yangu yote, nilimpa hata vile visivyohadithika lakini bado mtoto wa kike haonyeshi kuridhika kila mwanaume anataka awe wake. kama nilivyosema hapo mimi nimeamua kuchana na nimeshamtakia wazi ila yeye bado ananiomba msamaha anasema eti hawezi kuishi bila mimi. Nifanyeje jamani?
kak ukimchunguza sana kuku huwezi ukamla.
 
facebook ni kupata marafiki wa aina zote, wakimapenzi, wakimasomo,wakikazi, wakimaombi, wakibiashara,na mengineyo sasa wewe mkuu unategeme mke wako ajiunge na facebook awe salama wakati facebook kunawawindaji hatari ,cha msingi wewe usicomplicate, kama hujamfumania au kumuoana na mwanaume tofauti na wewe ,basi muache ale starehe ya facebook
 
Aisee wewe kweli haufai
 
Back
Top Bottom