Hivi ile tume ya mishahara (salaries and remunerations commission) ipo kwenye rasimu ya katiba?

msemakweli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,627
880
Nakumbuka mchango wa Mhe. Mbowe akipendekeza kuwepo tume ya mishahara itakayosimama ulipwaji wa mishahara kwa wafanyakazi wa bunge, serikali na mahakama, wakiwemo viongozi (wabunge, majaji nk) kama ya Kenya. Alisema tuachane na huu mfumo wa watu, haswa wabunge, kuwa na nguvu za kujiamulia mishahara watakaolipwa wao.
Nililiona ni wazo zuri sana.
Wanaojua naomba mnifahamishe hivi hiyo tume ilipita au la? Hii rasim ya katiba wanasema inatuwezesha sisi wananchi kiuchumi, lakini kwa kweli haijatuwezesha kisiasa! Viongozi wamejilinda sana na kuijiwekea masharti ya kujifavor sana!
 
Yaani unataka watu wakusomee Rasimu kisha wakupe majibu? Yaani wana-UKAWA mnachekesha sana!
 
Kwenye Katiba iliyopendekezwa na Chenge usitegemee kukuta kitu hicho! Hata mahakama ya Katiba nasikia ineondolewa.
 
Yaani unataka watu wakusomee Rasimu kisha wakupe majibu? Yaani wana-UKAWA mnachekesha sana!

BUCHANAN NIMEKUSOMA KILA KONA NIENDAYO,HUNA MASHIKO YA HOJA,HUNA UWEZO wa kutafakari kwa kina ndo maana unamuattack mtu badala ya hoja;any way mdau kauliza swali suala la ukawa linakujaje? kwa taarifa yako yey ni mwanachama mwenzako.usilewe chama
 
Yaani unataka watu wakusomee Rasimu kisha wakupe majibu? Yaani wana-UKAWA mnachekesha sana!

Kuna wakati nilikuwa nakuheshimu sana. Baada ya kufuatilia posts zako sehemu kadhaa nimekuona huna lolotr. Bila aibu nitakubali kwamba naunga mkono sera nyingi ambazo kwa bahati zinasimamiwa na vyama vya upinzani. Hii katiba Mungu atuepushie mbali!
 
me naona uvivu hata kuipitia kwani yoote niliyopendekeza yametiwa kapuni, nasubiri kupiga kura ya hapana! daah yaani mbunge ajue kusoma na kuandika halafu ndo asimamie serikali? haya twendeni!
 
me naona uvivu hata kuipitia kwani yoote niliyopendekeza yametiwa kapuni, nasubiri kupiga kura ya hapana! daah yaani mbunge ajue kusoma na kuandika halafu ndo asimamie serikali? haya twendeni!

Wakati hata kuomba udereva serikalini wanasema uwe na cheti cha form four....sasa sijui kwa nini wanakataa kwa wabunge?!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom