Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 4,160
- 11,483
Yaani nchi hii imejaa viongozi ambao ni wezi, majambazi, na vibaka wakubwa! Hawa watu kwa sheria za China adhabu yao ni kunyongwa! Dp world ndani yake ni mtiririko wa viongozi wetu tuliowaamini ndo wamegeuka kuungana na mabeberu kuuza rasilimali za nchi! Hivi unaweza kuamini kauli ya Nazir Kalamagi aliyewahi kuwa Waziri? Tena kuendesha bandari kwa mkataba wa miaka 15, akaomba aongezewe muda serikali ikamwongezea 5 kuwa jumla miaka 20 ndo akanyanganywa na ndo akajitokeza mwarabu wa Dp world? Hivi Nazir kalamagi kweli anaweza kushangilia mzawa kunyanganywa na kupewa mgeni? Sasa naelewa DP WORLD ndani ya pazia kuna utitili wa viongozi wanaofurahia nchi yetu kunyonywa na kuwa fukara wa kutupwa wakati wao na watoto wao wakifurahia maisha. Je! Nazir Kalamagi anafurahia kwa kufuata itikadi za kidini au nini? Mbona mtu mwenye akili timamu hawezi kumwelewa huyu jamaa! Lakini wakumbuke hata kama ni itikadi za kidini wakumbuke Gadafi wa Libya aligeukwa na wananchi wa dini yake. Naomba hizi itikadi za dini tuziweke pembeni tunapoongelea maslahi ya taifa! Tanzania ni yetu wote bila kujali dini! Angalia mtaani maisha yalivyo magumu! Unga, maaragwe, mchele, mafuta ya kula, petrol ️ na diesel ️ havikamitiki na nauli zinapanda kila kukicha! Watoto wa shule za umma darasa moja wanajazana wanafunzi 200, mahospitali wagonjwa wanalala mzungu wa nne. N.k, haya yoote hayachagui mkristo, muislam au mpagani! Tukipigika tunapigika woote!