Hivi hizi parking za taxi mjini ni nani anatoa vibali?

Mapondela

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
454
83
Wana JF kwa kweli ni muda mrefu nimekuwa nakerwa na parking za taxi katika mji wa Dar es Salaam haswa City centre. Katika kila sehemu ambayo majengo muhimu yapo utakuta taxi zimeandika kituo cha taxi. Ukiweka gari lako tu wanakuvamia kwa ukali hata kama unasimama kumsubiri mtu.

Mimi nina mashaka kama kweli huwa wamepewa hawa madereva wa taxi. Kama wamepewa na wanalipia basi kuna tatizo huko ofisi za jiji kwa sababu wametoa vibali vingi kiasi kwamba watu wenye magari tunataabika kweli na hawa madereva wa taxi na vituo vyao.
 
Back
Top Bottom