Hivi hii ni kweli kwa wanawake?

Katufu

JF-Expert Member
May 8, 2012
523
308
Leo mida ya saa 11 kasoro nilikuwa kwenye daladala kutoka Mwenge kuja Posta. Katika mazungumzo ya hapa na pale alikuwepo askari wa JWTZ akadai kwamba wanawake na wanaume wako sawa. Ila kuna mambo mawili mpaka sasa katika historia yamewashinda wanawake:
1. Mwanamke hajawahi kuendesha KIFARU akaweza, akasema nchi zote kuanzia Wayahudi (Israel) mpaka Marekani wamejitahidi majike dume wote lakini so far wamechemsha.
2. Mwanamke hajawahi kuwa katika kikosi cha kufyatua MIZINGA ya kivita na akaweza. Akatolea mfano kwamba walikuwa Afrika Kusini jike dume mmoja likabisha na unaambiwa huyo mama alikuwa strong si mchezo. Lakini unaambiwa baada ya kufyatuliwa mizinga miwili alianguka na kuzirai mpaka akalazwa hospitali.
Akasisitiza kwamba hizi habari ni za kweli yaani hakuna documented evidence kwa wanawake kufanya mambo hayo mawili wakaweza.
Haya magreat thinkers hebu tulidadavue na kulipekuapekua ili kujua ukweli wake.

Nawasilisha.
 
Roho zinawauma kwamba Bomu hilo linapotua kina Mama, Watoto, Wazee wasio na Hati wanakufa bila Hatia.
 
"P Square" wameimba 'What a man can do,a woman can do ....! Inabidi warudie utafiti wao,waje na single nyingine!
 
Kwa "uzoefu" wangu kweli sijawahi kuona wanawake wakiendesha tanks na pia najua kuna sehemu nyingi tu hawaruhusiwi jeshini haswa special ops. Ila kazi nyingine kibao hatuziwezi ni kwa wanawake tu! Kwahiyo ni mgawanyo wa majukumu tu
 
Back
Top Bottom