Nimekuja kupata wazo kwamba huenda baadhi ya vyeo vya kiutendaji serikalini huwa si muhimu sana.Maana mpaka sasa mkoa wa Dar es Salaam unakaimiwa baada ya aliyekuwa RC William Lukuvi kuukwaa uwaziri. Si DSM pekee bali pia kuna baadhi ya wilaya zinakaimiwa kitambo sasa na mambo yanaenda, hivyo kupelekea niamini kuwa na utitiri wa watendaji katika ngazi za mikoa,wilaya nk si kuleta tija ila mzigo tu kwa walipa kodi.