Hitilafu ktk bajeti

Mtumishi Mkuu

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
259
92
Hitilafu za Bajeti zaiangusha Wizara ya Afya Mei 29, 2011
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya mwaka 2010/2011 imejaa mipango isiyofaa na isiyozingatia kanuni, uhalisia na ufanisi hali inayoifanya ishindwe kufanya kazi zake ipasavyo.
Hayo yamebainika kwenye uchambuzi wa bajeti ya Wizara hiyo ya mwaka 2010/11 uliofanywa na Sikika, Shirika lisilo la Kiserikali la kufanya utetezi kwa ajili ya huduma bora za afya kwa Watanzania wote. Uchambuzi wa Bajeti ya sekta ya afya ni moja ya shughuli kubwa za Sikika katika kutetea mgao wa bajeti na matumizi yenye ufanisi. Ripoti ya uchambuzi imetolewa leo na pia inaweza kupatikana kwenye tovuti ya Sikika home page
Sikika imechambua mgao wa sekta ya afya na kujikita kwenye bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na za afya za mikoa na kugundua kwamba mipango iliyopo inakinzana kwa kiwango kikubwa na kukumbatia ufanyaji migao maradufu kwa shughuli moja. Pamoja na mabaya hayo, Sikika imetambua juhudi za wizara hiyo katika kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, ambapo wizara imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi hayo.
[/FONT]
[/FONT]Migao maradufu
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Imeonekana kuwa shughuli moja inaweza kupangiwa fedha kutoka kwenye vyanzo zaidi ya kimoja. Kwa mfano, wakati ni wajibu wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania kulipia safari za wabunge majimboni mwao, Kurugenzi ya Sera na Mipango ya Wizara ya Afya ilipanga kutumia milioni 75 kwa ajili ya safari za Waziri, Naibu Waziri na maafisa wanne kutembelea majimbo yao ya uchaguzi. Mgao huu wa fedha haukubaliki hasa ikizingatiwa kuwa kiasi hicho ni zaidi ya mara mbili ya fedha ambazo mikoa hupokea kutekeleza miradi ya VVU/UKIMWI au shughuli za kuzuia maambukizo ya VVU/UKIMWI. Mgao kwa ajili ya miradi hii kwenye Programu ya Sekta ya Afya ya Msingi ni sh milioni 30 kwa mkoa.
[/FONT]
[/FONT]Mipango isiyozingatia uhalisia
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Katika bajeti hiyo hiyo iliyochambuliwa, kifungu namba 1005, chini ya kipengele cha ‘Safari za Nje ya Nchi,’ Wizara imetenga shilingi laki moja tu kwa ajili ya safari lakini, katika hali halisi fedha hizo hazitoshi kwa ajili ya shughuli hiyo. Hii inaleta wasiwasi kwamba migao hii haikufanywa kwa umakini; ama sivyo hilo lisingejitokeza kwenye mipango hiyo.
[/FONT]
[/FONT]Mipango isiyofaa
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Mmoja wa mifano inayoonyesha mipango isiyofaa na isiyo na tija ni ule wa sherehe za kuadhimisha Siku ya Malaria Duniani mwaka huu ambapo sh milioni 62 zinatarajiwa kutumika. Ukweli ni kwamba matumizi hayo yangeweza kupunguzwa na kuelekezwa kwenye maeneo yenye tija kama vile ya ununuzi wa vyandarua hivyo kupunguza maambukizo ya malaria.
Mfano mwingine ni kwamba pamoja na kuongezeka kwa matukio ya saratani nchini, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road haikupata fedha yoyote iwe ya ndani au nje ya nchi kwenye bajeti hiyo. Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali pia haikuambulia chochote.
[/FONT]
[/FONT]Mipango isiyozingatia usawa
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Akiongelea uchambuzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Bw. Irenei Kiria, anasema "wakati matumizi zaidi ya shughuli za maendeleo kwa ajili ya kupambana na VVU/UKIMWI yanakaribishwa kwenye bajeti hii, fedha hizi zimegawanywa bila kuzingatia viwango vya maambukizo ya VVU/UKIMWI." Bw. Kiria anasema kuwa mikoa ambayo ina kiwango kikubwa cha maambukizo VVU/UKIMWI haijapewa kiwango kikubwa cha fedha za maendeleo kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo. Uchambuzi huo unaonyesha kuwa wakati Iringa ina kiwango kikubwa cha maambukizo kwa kuwa na asilimia16%, matumizi yake ya shughuli za maendeleo kwa VVU/UKIMWI ni sh 328 kwa kila mtu, wakati Arusha, ambayo ni miongoni mwa mikoa yenye kiwango kidogo cha maambukizo nchini (2%), inapata [/FONT][/FONT][FONT=Cambria,Cambria][FONT=Cambria,Cambria]sh 411 kwa kila mtu.
Mipango isiyofuata kanuni
[/FONT]
[/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Katika uchambuzi huo ilikuwa dhahiri kwamba ingawa mipango na bajeti katika sekta ya afya inaongozwa na sera na mikakati muhimu, mipango isiyofuata matakwa ya nyaraka hizo elekezi kwa wizara na isiyoendana na mipango ya Wizara imebainika.
Kwa mfano, wakati wa Programu ya Maendeleo ya Huduma ya Afya ya Msingi (PHSDP) inasema kwamba shilingi bilioni 59.8 zitatumika kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zinazohusiana na rasilimali watu katika sekta ya afya kwa mwaka huu wa fedha, Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya III unapanga kutumia sh bilioni 119.1 na Mpango Mkakati wa Afya wa Rasilimali Watu unaonyesha kupanga kutumia sh bilioni 90.3 kwa ajili ya shughuli hiyo hiyo.
[/FONT]
[/FONT]Mapendekezo
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][FONT=Times New Roman,Times New Roman]Sikika inapendekeza kwamba ili sekta ya afya iboreshe utendaji wake, inahitaji zaidi ya kuongeza tu rasilimali fedha. Sikika inaamini kwamba mgao na matumizi yenye ufanisi ya rasilimali unahitajika na siyo tu kuongeza fedha kwa ajili ya sekta hiyo kwani mwelekeo wa sasa wa mgao na matumizi hauashirii hali nzuri ya baadaye ya sekta hiyo.
Shirika inapendekeza kuwa katika mchakato wa mpango kwa bajeti ya 2011/12, mahitaji ya sekta ya afya yapewe kipaumbele kwa madhumuni ya kukabiliana na changamoto za sekta. Sera mbalimbali zinazoingoza sekta hiyo zioanishwe na kuzingatiwa kuhakikisha kuwa mgao unafanywa kwa mujibu wa vipaumbele vilivyowekwa.
Bajeti hii pia izingatie mahitaji ya watu kwani hali hiyo itasaidia kutatua matatizo yao na kusababisha maendeleo endelevu ya sekta ya afya nchini. Pia ni muhimu kwa serikali kuhakikisha kuwa mipango inalenga kutenga fedha za kukabiliana na vyanzo vya matatizo na siyo matokeo yake.
Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi info@sikika.or.tz
[/FONT]
[/FONT]
 
Back
Top Bottom