Hitaji muhimu juu ya elimu ya virusi vya homa ya ini

Jan 22, 2023
8
2
Nafikiri sasa wadau kushirikiana na serikali upo umuhimu zaidi kutoa elimu ya afya kuhusiana na homa ya ini.

Maana ili jambo kiukweli kwa sasa imekua ni hatari kubwa kwa afya za watu na takwimu nilizo nazo kulingana na utafiti wangu binafsi inaonyesha watu wengi bado atuna uelewa juu ya tatizo hili kwa utafiti wangu ni 65% ya watu bado awajui juu ya homa ya ini.

Hivyo serikali na sekta binafsi vyuo na mashule ikibidi kwa ngazi zote Ina bidi kushirikiana kutoa elimu juu ya uwepo wa homa ya ini kwa njia mbalimbali kupita vipeperushi vya maandishi na picha ikionyesha njia zinazo weza kuchangia maambukizi ya homa hiyo inavyo sambaa na namna ya kujiakinga na hata njia za kupata chanjo na matibabu kama yapo.

Kuliko kama ilivyo sasa nikupitia televisheni na smartphone pekee ndio unaweza kuona taharifa za homa hiyo kupita vipindi vya madaktitari au wale wauza madawa wanapotoa matangazo.

Changamoto inakua kwa wale wanao ishi nje ya televisheni na hawana smartphone ila kukiwa na vipeperushi na mabango ya matangazo juu ya homa hiyo naamini wananchi wengi watajua ukubwa wa tatizo hili.

Wadau wa afya na Serikali kupitia Wizara yake ya afya ifanye hivyo kama ilivyo kua kwa maradhi kama UKIMWI, Malaria, Kifua kikuu(TB) na janga la COVID- 19 ili watu waelewe kiurahisi.
 
Back
Top Bottom