Historia ya maisha yangu

INTROVERT MAN

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
993
1,337
HI THERE, MAISHA YANGU
Mahusiano, Muziki, Depression, hustles, & Happiness.

Habari wakuu wa jamiiforums,
Heshima kwenu.

Kuna msemo mmoja wa Kiingereza unasema " if a street performer make you stop walking, you owe him a buck"
Basi kupitia hadithi za ukweli nilizozisoma humu basi nami ninawiwa kuileta yangu kwani uhalisia wa maisha waliyopitia baadhi ya walioleta story zao humu kama mzee Akili Sina , Analyse, UMUGHAKA na wengineo wameni inspire na mimi nilete story yangu. Sababu kuu ya kuandika ni kwamba napenda kuandika sana na hao wanaJF wananidai coz nimejifunza vitu vingi toka kwao.

Nikisema nimepitia labda maisha magumu nitakuwa nakufuru. Nimepitia mambo ya kawaida ila natoa maangalizo mapema lakini binafsi nimepitia mitihani iliyokuwa migumu kulingana na umri wangu na pia issue ya kuhandle kitu ambacho ndio unaface kwa mara ya kwanza katika life. Hii ni kwa kila mtu hapa duniani. Kinachokuja ku matter hapa ni kwamba kiwango cha maumivu experienced by brain ni sawa hata kama ni mapito ni tofauti.. Nasema hivi mapema kwani isije ikafika huko kwenye comment yakaanza mashindano ya shida oh wewe umepata tabu gani? sisi ndio tumeptia shida. Ok kama mimi kula andazi moja asubuhi kwangu ni tabu afu kwako ni bless haina noma kumbuka kuna wengine breakfast ni draft za madikodiko.
Classes zipo hadi mbinguni so duniani tu haziepukiki. Kuna malaika wakuu na malaika wa kawaida. Kuna malaika wako jehanamu wanageuza watu waungue vizuri. . Kuna wengine wanazunguka katika kiti cha enzi.
Hivyo tu.

Msitishwe na nilivoandika heading hapo kuna neno muziki mkajua mimi ni mwanamuziki hapana. Me ni napenda muziki kuusikiliza sana. Hata hii stori nimeweza kuandika vizuri kutokana na kupata nostalgic memories kutokana na nyimbo fulani fulani hivi.

UZI HUU NIMEANDIKA KWA NOTE BOOK YA SIMU SO MSIJARI NI UMEKAMILIKA FROM A TO Z. YOU HAVE NOT TO WORRY. NITAKUWA NA PANDISHA KIPANDE KILA JIONI. ni mwendo wa kupaste tu. Au mods mnasemaje??.


TAFADHALI KAMA UTAUNGANISHA DOTS NA UKANIJUA BASI FANYA UVUNGE KIMYA KIMYA KAMA UMEKUTANA NA JESHI LA VIBWENGO. UVUNGE KABISA.

Here we go.

1. BAADA YA KUMALIZA FORM FOUR NA KWENDA ADVANCE.
Nilivomaliza form four basi nilirejea nyumbani kwa mama angu ambae anaishi nje kiasi chake toka kwenye mji fulani. Sababu ya kurudi kule ni kwamba kulikuwa na fursa ya kazi kwa kijana mdogo kama mimi kufanya manual labour kwenye mashamba ya zao fulani la kibiashara.
Nilirudi kwa mama tokea shule iliyokuwa mjini. Nilirudi kilazima japo sikupenda kurudi kule nilitamani kukaa kwa ndugu yangu mjini.

Kilichofanya nirudi kule ni msiba wa bamdogo aliyefariki 26/December so tulivozika wanafamilia wakanipiga pin nisirudi. Aiseee nilichukia sana. Lakini nashukuru Mungu ni kwamba kurudi kule kijijini ni ilikuwa baraka kubwa sana kwangu. Kulifanya nikakua kiakili kiasi chake.

Basi msiba ukaisha. Basi mama ambaye ni mjane na anaishi peke ake kutokana na kuwa watoto wote tumetawanyika kusaka maisha na sisi huku wa mwishoni ndio tunasoma basi alishukuru me kuwepo pale kama mtoto wa kiume kusaidia majukumu mengine ya home hata kumuondolea upweke.

Mama akasisitiza nikaombe kazi kwenye kampuni kubwa ya kilimo ambayo iko karibu na kijiji. Kishingo upande nikakubali. Nikaomba msaada wa watu jinsi ya kujiandaa na vitu gani yaani passport na kitambulisho chochote. Mama alinipa elfu tano kwa ajili ya kupiga paspoti size. (Kijijini ni gharama kubwa).

Baada ya kujiandaa basi Jumatatu huyo ya mguu safari ya km mbili mpaka katika ofisi ya hiyo kampuni.
Mdogo mdogo huyo asubuhi mama aliniandalia chai. Nikanywa vizuri nikaondoka. Kipindi hicho nilikuwa namiliki kisimu fulani hivi nokia navigation cha button. Kilikuwa na Internet kupitia opera mini na storage kiasi chake. Hako kasimu kalinisave sana. Basi huku nikitembea nilikuwa nasikiliza wimbo wa post to be wa marion ambao mwaka ule ulikuwa hot sana bila kusahau wa Kid ink show me ft chris brown



Basi nikafika ofisini wakaniandikisha kazi. Uzuri ni ulikuwa msimu wa kuajiri. Niliripoti tarehe 7 mwezi wa kwanza. Wakanipa number yangu kuwa kesho nifike nayo kwa head man katika division niliyopangiwa. Kumbuka kampuni ina division kibao zenye maekari ya kutosha.
Kazi yenyewe ni uvunaji na me sina experience sana dah nikaona hii hatari. Lakini nikakumbuka ya kuwa kuna shamba jipya linatengenezwa yaani ndani ya virgin forest umefumuliwa so wanataka kupanda miche mipya.

Huko ndiko vijana wengi wanapenda na ni kazi ya kulipwa kwa siku yaani 5,400/= ila mshahara kutoka mwisho wa mwezi. Wazee na watu wazima hawapendi huko ila wao wanapenda uvunaji. So kwa kuwa kule kuna vijana afu kuna wanangu wengi wa kijijini kwetu na waliomaliza form four wapo kule basi nikaona hapa ndio penyewe.
Na uzuri ni kuwa hilo shamba jipya ni pua na mdomo na kijijini kwetu kuliko huko division nilikopangiwa na nikikumbuka uvunaji ndio siwezi.

Nikatoka ofisini nikaamua nipitie shamba jipya siku ile ile. Kumbe headman wa shamba jipya ni brother fulani kasoma na sister angu afu ni mwana balaa. Akanisalimia chapu akaniuliza kwa kilugha dogo na wewe kazi utaweza nikasema sana. Nikamuambia nimetoka ofisini ila uvunaji siwezi ndio maana nimekuja huku.
( Kiukweli mimi jembe ninapiga sana hata shule nilikuwa nalima na pia nilikokuwa nakaa mjini tuna mashamba na vinyungu so kulima nilikuwa napiga hatari mpaka leo hii ninaweza).

Basi nikampa namba akairudisha akasema dogo usiogope we njoo nayo kesho usisahau jembe. Nikasema sawa usijari imeisha hiyo '' in Kidagaa voice "

Kesho asubuhi saa kumi na mbili nikaamka nakuta mama kajihimu kanipikia bonge la ubwabwa . Nikawahi mno kazini aka shambani niliwahi kuliko inavyotakiwa. Nikapeleka namba pale wakanisajili. Tukapangiwa ukubwa kila mtu mahali pa kupiga hallow.

Kwenye hilo shamba jipya ni kuwa makatapila na magrader yalikuwa yamefumua na kulima so sisi kazi yetu na majembe ilikuwa ni kupigasha na kusawazisha na kutoa mizizi na vijigogo. Ilikuwa kazi easy sana na mwisho ni saa tano au sita.
Siku ya kwanza nilitoka jasho balaa ila wana wakanisaidia. Uzuri asilimia kubwa ya jamaa zangu wa pale kijijini nao walikuwa wanafanya kazi pia.
Nilipangiwa pagumu wakanisave. Tumbo lilifanya kazi iwe ngumu basi nikajikuta napata tabu. Kumbe nikajua haitakiwi me niwe nakula asbh.

Maisha ya kule shambani yalikuwa vizuri sana tena sana nayamisi kwa kweli. Sikuwa muongeaji sana na kama kawaida yangu. Mama aliniambia huko kazini kuna mengi ukiwa muongeaji manyapara hawapendi kabisa.
Na kampuni inaendeshwa kikoloni kwa sababu ipo hata kabla ya uhuru so kuna kuendeshana fulani hivi.

Kipindi hiko nilikuwa katika mahusiano na mwanamke wangu wa toka shule. Tulikutana shuleni yeye akiwa mgeni pale. Alihamia tukiwa form two nikawa nae kuanzia form three so kwao ilikuwa Dar afu me mkoani. Hata baada ya kumaliza shule tulikuwa tunawasiliana vyema kabisa. She loved me for real aisee. Kinokia changu kilikuwa kinatuunganisha.

Mshahara tulikuwa tunapokea tarehe 7 au week ya mwanzo wa mwezi. Tena dirishani ofisini ila ulinzi unakuwepo mkubwa tu.
Mwezi wa pili tarehe 7 nikapokea dirishani pesa yangu kubwa. Toka nikue ndio pesa ndefu niiyopokea. Ilikuwa shilingi 79,860/=. Ndio shilingi sabini na tisa mia nane na sitini!!!
What a smile. What the first pay. Nakiri ilikuwa ni pesa nyingi kwangu kwani licha ya kupiga vijikazi mjini sikuwahi kumake zaidi ya elfu tano kwa mara moja. So i was so damn happy.

Siku za mishahara basi huwa kuna kuwa na minada. Wanauza kila kitu.
Nami nikaenda mnadani. Nikanunua nyanya lita moja za buku nikasepa home bila kutazama Nyuma. Njiani nikapata lift. I was so happy Jamani. Nikafika home nikampa mama nyanya zake na pesa zote. Nikasema anipe tu elfu tano tu kwa mwezi inanitosha sana. Matumizi ni sadaka na vocha tu. Miaka kadhaa hapo mabundle yalikuwa rahisi tu.

Kazini kulikuwa njema. Headman alinipenda ila alikuwa anani treat kama msomi sijui kutokana na family status.

Yeah, sijisifu ika family yetu pale kijiji ilikuwa ya kipekee sana. Marehemu baba alikuwa strict sana. Na mama ndio kabisa.

***********
 
MAISHA YANGU

SEHEMU YA PILI.
inaendelea

............ Yaani wale ni walikutana wakatuzaa sisi. Headman wa shambani alikuwa hanijui coz sijakulia kule ila baada ya kuambiwa huyu dogo ni wa nyumba fulani basi alinikubali mazima. Akaniuliza ndio wasubiri matokeo? Nikasema ndio. Alinipenda sana mpaka leo kuna siku alinambia dogo isingekuwa matokeo yako kuwa mazuri na unaenda advance basi dogo tungekutafutia kacheo uwe nyampara . Sijui nyota. Nilikuwa nateleleza yaliyomo kwenye kitabu cha 48 laws of power hasa ile law say less than necessary. Hahahahah sikuwa najua kwa sababu hicho kitabu nilikuja kukijua baadaye.

February basi matokeo yalitoka basi broo alieniachia ziwa alikuwa chuo so akanipigia simu dogo matokeo nasikia yametoka. Duh me tumbo joto na ukijumliasha sina smartphone kuchekia. Akanitoa hofu kuwa atanichekia afu atanipiagia. Dah sikuwa na wasiwasi mkubwa coz mtihani nilikuwa najua siwezi feli. Ndio nilifanya mwenyewe so nilikuw najua hapa kuna kupata sio kukosa. Ila presha kawaida. Jioni bro akanipigia na siku hiyo mvua ni imepiga balaa akaniambia nimtajie namba ya shule na yangu. Dah akaanza akanambia shule yenu mlikuwa 218 eh nikasema ndio. Akasema waliofaulu ni 20 tu ila na wewe UMEPIGA aisee nilifurahi hovyooo hatari..

Wakati ananipigia sikuwepo home. Nikarudi kumpa taarifa mama. Alikuwa shamba nje nyumbani anachimba viazi. Alifurahi basi kujipongeza. Nikaenda nunua nyama tukapiga na viazi .

Kipindi hicho nilikuwa nikitoka kazini shambani basi nilikuwa nashinda kwenye kilibrary cha rafiki ake bro so nilikuwa najifunza utundu utundu mwingi. Nilikuwa napenda sana kujifunza programu, games kurusha nyimbo ufundi simu na mambo kama hayo. Nakumbuka siku hiyo ya matokeo nilivokuwa pale library nilikuwa na ma vibe sana nikajibless kwa ngoma hili linaitwa feeling the nikka la D banj ft akon " feeling the nikka"


Kumbe bhna shemeji yenu matokeo yake hayakuwa mazuri. Nikamtafuta jioni hiyo akawa harespond kabisa, na me sikubadilika chchte kile. Nikawa namtext sms nzuri za kumbembeleza akawa hajibu ila zinadeliver. Inaonesha hakuwa vzr kisaikolijia kutokana na matokeo yake mabovu.

Dah sikuwa najisikia kwa kweli. Sikumbadilikia kitu. Kufaulu kwangu hakukufanya nipunguze upendo kwake. Sikuipa ego nafasi ila nikashangaa hajibu. Basi week ya kwanza ya pili nikaamua na me nikae kimya kama kuna lingine atanitafuta. Nikawa na mawazo ya kitoto au atakuwa kafariki, . Utoto huu dah
Basi nikaamua kukaa kimya nikaona labda pia kanuna kisa nimefaulu afu yeye ndio hivyo. Dah nakumbuka Februari 27" ndio birthday yake basi ilikuwa j mos nikasema asbh na mapema ninamtext kum wish afu ninakaa kimya mazima. Nilidhamiria kwa kweli nakupenda afu kisa nimefaulu afu nakubembeleza unaninunia. Kwendaaa huko.
Nilimtext nakumbuka akanijibu "ahsante my friend"

Dah nilichoka leo nimekuwa friend. Au kisa huu umbali jamani dah niliumia ila sikujibu kitu nikasema powa..
Wana jf hii ndio heartbreak ya kwanza maishani mwangu dah niliumia kimyakimya hasira zikawa nimehamishia shambani kuwa nipige kazi nisave my f*kng money then niende advance.


Nikamsahau dakika tu me huyo kazi, church na kufanya home chores basi. Basi ndio life style mpya inabidi niishi.

Kazini kulikuwa safi. Nilikuwa nasave 95% ya mshahara. Wote anakaa nao mama. Ishu ikaja home hatuna umeme. Na sisi kule kwetu hakuna huu umeme wa tanesco wala Rea. Kule kuna umeme wameutega huko mpakani na Morogoro. So haukuwa bei sana. Basi sister alipropose tutoe pesa. Mama alitoa na me nikatoa kwenye akiba na sister pia. Basi home pakawa panawaka napo. Am so proud kufanya endeleo linaloonekana kwa mara ya kwanza.

Ah kuna siku napalilia hivi naona text kucheki ni yule mwanamke wangu. Hapo nimeanza kumsahau nikasema ananitafutia nini akati nishamsahau. Sms yake ilikuwa ni kunisalimia. Sikujibu nikaendelea zangu kupalilia.
Jioni akanitafuta tena dah mapenz haya akaniomba msamaha sijui nini. Sikumruhusu aongee sana sipendagi nilijua lbda matokeo ua shule ndio sababu. Basi akasema ananipenda. Basi yakaisha.

Yule mdada nilimpendaga nisiwe muongo.
Tukaw powa tu maudhi ya kawaida yapo. Ila tulikuwa powa kabsa japo ni ile distant relationship.

2.KWENDA ADVANCE
Post za shule zikatoka. First selection kabisa. Shule iko mpakani mwa nchi. I was so excited. Nilikuwa napenda nikutane na new people na ile kitete cha kwenda nje ya mkoa. Brooo come on .
Huyo maandalizi chap nikaenda shule ya olevel kuchukua result sleep.
Hapo nishaaga home kwa mama then nipitie shule then mpaka town ili nifanye maandalizi niwahi shule.
Nakumbuka safari ile kwenye gari ilipgwa ngoma ya Wycliffe Jean ft Lil Wayne "Dollar Bill" aka sweetest girl.

Ilikuwa ni zile noah za Bush.
Maandalizi yakawa powa bro ndio alikuwa karudi likizo so alinisave pakubwa.
Huyo nikakwea shule. Nililala mkoani kwenyewe then kesho safar ya kuelekea wilayani. Basi nikawa nawaza dah maisha. Mengine pia lakini sio mbaya tv na speaker za basi zilikuwa zinapiga nyimbo fulani hivi hasahasa ile ya diamond kashirikishwa na Akothee inaitwa sweetlove basi ilinogesha safari yangu nikawa namkumbuka mchumba.

Nikiwa njiani mchumba akanijulisha kuwa aliapply chuo kusomea issue za IT so ndio kafurahi mwenyewe. Nikasema sawa ila nikajiambia mh kaenda chuo nina changu kweli?? Ila yeye alikuwa anasisitiza mawasiliano ndio kila kitu. Hukupita muda nikawasili shuleni kwenyewe.


Ahhh
Ile shule ni tofauti na nilivoitegemea. Nakumbuka ilikuwa tarehe 23/7 nilivoripoti.
Picha linaanza tukaambiwa tukabidhi simu zetu. Dah nilikuwa nimeenda na kanokia kangu nikikokatengeneza kwa kujnganisha spear kipindi kile nashinda kwenye library ya best ake bro. Dah nilikuwa choko kweli badala ya kuficha nikakabidhi basi mawasiliano na mtoto yakakata. Dah poor me.
Shule ilikuwa na mikazo sijawah ona. Ukiwa na kosa dogo tu kwenu. Mazingira hayakuwa friendly kwangu. Kwanza huko hakuna umeme kuna solar tu. Ah Nikataka kuhama ndugu hata hawanielewi
. Dah kunywa uji wa mahindi ilikuwa jau. O level tulikuwa tunapiga chai. Ule uji ukipiga tu ukirudi class lazima ulale aisee. Dah hatari.

-KUNUSURIKA KIFO CHA MAJI.
Nikiwa nina week moja yaani tarehe 30/7 basi tukiwa ziwani kumbuka hii shule iko mwambao wa ziwa moja hivi basi shughuli zote ni ziwani iwe kufua, maji ya kuoga na kupikia ni ziwani. Tulikuwa tunaogelea sana aisee ila mimi nilikuwa sijui.
Siku hiyo ilikuwa ni Jumapili mida ya saa nane
hivi. Pale beach palikuwa na jahazi limetia nanga. Jahazi la uvuvi. So kuna jamaa alilegeza kama ya nyuma ya jahazi then akapanda mbele kabisa ua mashua akawa anavuta kamba ya nanga. So akivuta ile kamba jahazi linasonga mbele. Likiwa linasonga sisi tunajishikilia pembeni mwa jahazi kwa nje kama vile wadada wasiojuaga kuogelea wanavijishikizaga kwenye swimming pool vile.

So jahazi likifika mahali kwenye kina jamaa anaachia kamba then sisi tunajiachia kwenye maji. Jahazi linarudishwa na upepo beach then mchezo unajirudia .

Basi kuna round nyingi tulipiga mambo yakawa fresh tu. Ila kuna raundi hii yenye kisanga. Jamaa alivuta ile kamba kuliko awamu zote zile. So chombo kilienda mbali kuliko kawaida. So jamaa akaachia kamba na sisi tukajiachia.
Paap nimejiachia ahh cheki hivi chini naona miguu haifikii chini. Cheki juu mikono imepotelea. Dah nikajua hapa nimemezwa na maji. Kumbe jahazi lilifikia kwenye kina kirefu.

Jagi la kwanza, nikarudi juu, mamaaa nikarudi chini, jagi la pili, nikarudi juu nikanyoosha mikono " nakufaaaa jam" nikarudi chini ile naanza kupiga jagi jingine nikashangaa navutwa. Dah kuna jamaa wawili wanafunzi wenzangu waliokuwa wanajua kuogelea. Wakaniokoa bhana. Ndio ningekufa ndugu zangu. Basi hapo ndio ikawa tiketi ya mimi kujua kuogelea.

Maisha ya shule yalikuwa tight sana. Joto kali, msosi mbaya hatari. Unga waliokuwa wanatupikia ulikuwa ni umevunda hatari. Kiasi kwamba hata ukimpatia kuku hadonoi. Ndio hadonoi cause kulikuwa na kuku wa walimu walikuwa wanaingia dining walikuwa wanakula tu maharage babaake.

Uzuri wa shule ilikuwa ni uwepo wa beach safi, kucheza beach soccer,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom