Historia ya Kura Tatu: Dua ya Mnyanjani Tanga Hadi Hotuba ya Julius Nyerere Ndani ya Parish Hall (Ukumbi wa Kanisa Katoliki) Tabora 1958

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
HISTORIA YA KURA TATU: DUA YA MNYANJANI TANGA HADI HOTUBA YA JULIUS NYERERE PARISH HALL (UKUMBI WA KANISA KATOLIKI) TABORA 1958

Laiti kama si Sheikh Abdallah Rashid Sembe wa Tanga kukubali kuzungumza na mimi historia ya Kura Tatu isingejulikana kwa ukamilidu wake.

Waliokuwa wanaojua mkutano wa siri uliofanyika Tanga walikuwa wao viongozi wa Tanga, Mwalimu Nyerere na Amos Kisenge peke yao.

Bahati mbaya Mwalimu Nyerere hakupenda kueleza historia yake katika mengi yaliyofanywa na viongozi wenzake wa TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia hii muhimu sana katika kjupigania uhuru wa Tanganyika ingepotea na ikawa inajulikana kijuujuu kama ilivyokuwa historia ya chama cha TANU chenyewe.

Historia ya Kura Tatu nimeieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes (1998) na kwa ushawishi wa mchapa vitabu mmoja kutoka Kenya akaniomba nimpatie mswada wa kitabu cha historia hii achape kitabu makhsusi kwa kaudhimisha miaka 50 ya Azimio la Busara mwaka wa 2008.

Kazi hii niliifanya na ilikuwa mapendekezo ya mchapaji huyu kitabu hiki kiandikiwe utangulizi na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Jinsi alivyothamini historia hii mchapaji huyu alikuwa amepanga kuchapa nakala chache maalum kwa ajili ya viongozi wa nchi.

Kitabu kilichapwa lakini bila ya kuandikiwa utangulizi.
Kwa ajili hii nakala zile maalum kwa watu maalum hazikuchapwa.

Kitabu hiki kikafa kabla ya kuzaliwa lakini kilipotoka chote kilinunuliwa kwa haraka sana na sasa ni katika vitabu vinavyoitwa, ‘’out of print,’’ yaani vimekwisha sokoni havipatikani hadi vichapwe upya.

Kitabu hiki ni cha pili katika vitabu vyangu viwili vilivyochapwa na na ''publishers'' wa Kenya vinavyohusu historia ya uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya sana vitabu hivi vyote viwili havikupata mafanikio Tanzania.

Havikupendwa.

Nimepokea picha ya Parish Hall Tabora palipofanyika Mkutano wa TANU wa Mwaka wa 1958, mkutano uliokuja kufahamika kama Mkutano wa Kura Tatu kwa kuwa TANU ilikuwa inajadili agenda nyeti sana ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza kuchagua wajumbe watakaoingia katika Baraza la Kutunga Sheria (LEGCO).

Nikiwa naiangalia picha hii fikra nyingi zilipita kichwani kwangu.

Nilikuwa nawaza nchi hii ilikotoka na historia yake ya umoja wa wananchi wake na jinsi historia ilivyopotoea ikawa haijulikani.

Nachelea kuifanya makala hay kuwa ndefu sana kwa hiyo nitaeleza jambo hili ninalokusudia kwa kifupi.

Mwalimu Nyerere na Amos Kisenge walikwenda Tanga kuonana na uongozi wa TANU kutafuta kuungwa mkono kwa agenda ya TANU kuridhia kushiriki katika Kura Tatu jambo ambalo wanachama walikuwa wanapinga kiasi kuja na kauli mbiu, ''Kuingia Kura Tatu ni Sawa na Mtu Kujipaka Kinyesi Chake.''

Sababu ya upinzani huu ni yale masharti ya kupiga kura na masharti ya mpigiwa kura.

Mpiga kura alitakiwa awe na elimu ya darasa la 12 (wakashudha hadi darasa la 10), awe na kipato cha Pound za Kiingereza 400 kwa mwaka, awe na kazi ya ‘’kueleweka’’ na ampigie kura Mzungu, Muasia na Mwafrika.

Wanachama wengi wa TANU walikuwa Waislam na ukoloni uliwanyima elimu kwa kuwa elimu ilikuwa ikitolewa na wamishionari kwa kushirikiana na serikali ya Kiingereza.

Masharti haya yaliwatoa katika kupiga kura na halikadhalika kupigiwa kura kuingia katika LEGCO.

Lakini hili halikuwa likisemwa bayana.

TANU ilikuwa na hofu kubwa na hisia za dini ndani ya chama kwa kuchelea kuwagawa wananchi.

Hukumu yake kwa mwanachama atakaekiuka sharti hili ni kufukuzwa chama.
Wanachama wa TANU waliweka msimamo wao tu kuwa hawatashiriki katika uchaguzi wa Kura Tatu bila ya kueleza hayo.

Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU akawa kiongozi wa kupinga TANU kuingia katika Kura Tatu.

Katibu Mkuu wa TANU Zuberi Mtemvu ns yeye pia alikuwa katika wapinzani wa Kura Tatu.

Majimboni kote Dodoma, Lindi, Tabora, Tanga, Kanda ya Ziwa hali ilikuwa ni hivyo.

Rais wa TANU Mwalimu Nyerere kuona hali hii ndiyo akaamua kwenda Tanga kuzungumza na uongozi wa TANU wa akina Mwalimu Kihere, Abdallah Rashid Sembe, Hamisi Heri, Mohamed Kajembe kwa kuwataja wachache kutafuta msaada kuwezesha TANU kushiriki katika Kura Tatu.

Mkutano wa Tanga ulikuwa mzito sana lakini hatimae walikubaliana kuwa lazima TANU ishiriki na wakaweka mikakati ya ushindi ndani ya chama kuwashinda wapinzania wa Kura Tatu na nje ya chama kushinda hila za Waingereza na chama chao cha United Tanganyika Party (UTP).

Baada ya kumaliza kikao hiki viongozi wa TANU Tanga wakamwambia Nyerere kwa kuwa hili jambo ni kubwa lazima ifanyike dua kumuomba nusra ya Mwenyezi Mungu.

Leo ukieleza kuwa Qur'an ilikuwa ikitangulia kusomwa katika mikutano ya TANU hakuna atakaeamini.

Kulikuwa na hofu kubwa kuwa kama hawatakufikia muafaka Tabora TANU itameguka vipande viwili na kuna hatari Julius Nyerere akajikuta yuko peke yake kundi kubwa likabaki na Sheikh Suleiman Takadir na Zuberi Mtemvu na wengine.

Dua hii ilifanyika kijiji cha Mnyanjani nje kidogo ya Tanga na Mwalimu Nyerere na Amos Kisenge walishiriki.

Kisomo kilifanyika usiku na kumalizika alfajir.

Mwalimu na Kisenge wakarudi Dar es Salaam kisha wakaenda Tabora kwenye Mkutano Mkuu wa TANU wa 1958.

Katika mkutano wa Tabora Mwalimu akawahakikishia wanachama wa TANU kuwa TANU itaingia kwenye Kura Tatu na Wazungu wake na Waasia wake wote wanaunga mkono TANU.

Ilikuwa ndani ya Parish Hall ndipo Mwalimu Nyerere alipotoa hotuba iliyobadili mwelekeo wa wanachama wa TANU wa kugomea Uchaguzi wa Kura Tatu na kukubali kushiriki.

TANU ikaja na kauli mbiu mpya kututa ile kwa kwanza, ''Tuingie Kura Tatu Tuiondoe Kura Tatu.''

Sasa angalia waasisi wa nchi hii walivyokuwa na busara.

Bila ya kujali dini zao Mwalimu Nyerere na Amos Kisenge walishiriki dua Mnyanjani dua iliyoongozwa na kufanywa na masheikh kuiombea TANU ushindi.

Ukweli ni kuwa Mwalimu alikuwa mzoefu wa haya kwani kila alipokwenda alikutana na dua ndani ya TANU.

Wanachama wa TANU wakafanya mkutano Tabora ndani ya Ukumbi wa Kanisa Katoliki (Parish Hall) na hapakuwa na ukinzani kutoka kwa Waislam kwa nini mkutano huo muhimu ufanyike pale.

Leo tumefikaje katika hali hii ya chuki inayoonekana hivi sasa?

Ukisikia anatajwa Mwarabu ni uoga tu lakini aliyekusudiwa hapo ni Muislam.
CCM ina wajibu mkubwa sana wa kusomesha historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika.

Huenda hawa wasiojua wapi nchi hii ilikotoka wakabadilika.

Halikadhalika huenda ikatusaidia kuleta utangamano na kurejesha msingi wa mapenzi ulipobomolewa baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.

PICHA: Jengo la Parish Hall nje na ndani, Mnara wa Julius Nyerere wa Kumbukumbu ya Kura Tatu, picha ya Mwalimu Nyerere na Hemed Mashaka wakati wa Mkutano wa Kura Tatu.

1686491563222.png

1686490210798.png

1686491619885.png
1686491683794.png

1686491905852.png
 
Mzee Mohamed Said shikamooo!Nimesoma andiko lako Jana umewasikiliza wabunge wako lakini pia wewe ni mtu mzima wa TANU Kwa macho ya kawaida Kwa nini unataka tuzungumzie dini badala ya uzalendo wa nchi ?Sisi watanzania Kwa mujibu wa katiba yetu lazima tulinde nchi yetu ikiwemo mipaka yetu ,tulimfukuza mwarabu,tulimfukuza mreno,tulimfukuza mjerumani na hao wote hakuna aliyetawala zaidi ya miaka 50 ,lakini pia hao wote tuliwafukuza Kwa kuwa 1 walitunyanyasa,walituuza,walichukua Mali zetu,Sasa Leo mwarabu anapewa ardhi yote ya Tanzania Kwa kisingizio cha uwekezaji !!!!!Hatupingi uwekezaji lakini huo MKATABA unatuuza hadi chupi zetu fikiria mwarabu anapewa hadi anga letu,MOHAMED I SAID kuwa mzalendo,nisaidie kidogo Kwa nini chama chako kimetoka kwenye misingi ya chama Sasa nimeingia kwenye chamadola???
 
Mzee Mohamed Said shikamooo!Nimesoma andiko lako Jana umewasikiliza wabunge wako lakini pia wewe ni mtu mzima wa TANU Kwa macho ya kawaida Kwa nini unataka tuzungumzie dini badala ya uzalendo wa nchi ?Sisi watanzania Kwa mujibu wa katiba yetu lazima tulinde nchi yetu ikiwemo mipaka yetu ,tulimfukuza mwarabu,tulimfukuza mreno,tulimfukuza mjerumani na hao wote hakuna aliyetawala zaidi ya miaka 50 ,lakini pia hao wote tuliwafukuza Kwa kuwa 1 walitunyanyasa,walituuza,walichukua Mali zetu,Sasa Leo mwarabu anapewa ardhi yote ya Tanzania Kwa kisingizio cha uwekezaji !!!!!Hatupingi uwekezaji lakini huo MKATABA unatuuza hadi chupi zetu fikiria mwarabu anapewa hadi anga letu,MOHAMED I SAID kuwa mzalendo,nisaidie kidogo Kwa nini chama chako kimetoka kwenye misingi ya chama Sasa nimeingia kwenye chamadola???
Kimbe...
Dini ni muhimu kupita kiasi katika historia na siasa za Tanzania.

Anza na harakati za kudai uhuru na malizia na hali ya siasa hivi leo.

Kuna mambo utajifunza.

Jiulize kwa nini unatajwa Uarabu.

Umepata kusikia malalamiko yoyote yakitajwa mataifa ya Ulaya kwa makabila yao?

Hawa wana migodi ya dhahanu nchini kwa miaka mingi.

Ukiwa ni mgeni katika somo hili nifahamishe nikuelekeze vitabu vya kusoma.
 
Kimbe...
Dini ni muhimu kupita kiasi katika historia na siasa za Tanzania.

Anza na harakati za kudai uhuru na malizia na hali ya siasa hivi leo.

Kuna mambo utajifunza.

Jiulize kwa nini unatajwa Uarabu.

Umepata kusikia malalamiko yoyote yakitajwa mataifa ya Ulaya kwa makabila yao?

Hawa wana migodi ya dhahanu nchini kwa miaka mingi.

Ukiwa ni mgeni katika somo hili nifahamishe nikuelekeze vitabu vya kusoma.
Je magufuli alipokiwaita wazungu mabeberu na wanyonyaji wewe ulikuwa unafurahi?
 
naendelea katibu wa wizara ni mzanzibar,waziri wa wizara mzanzibar, Rais anatokea makunduchi hivi hapo Kwa macho yako Nani atakuamini kwamba wewe unania njema na nchi?
Sasa hapa tatizo ni Uislamu au Uzanzibari?

Mi naona Tatizo ni uzanzibari ndio maana bandari ya Zanzibar hajapewa Mwarabu... Kama kweli mwarabu yuko vizuri na nia ni njema, Bandari ya Zanzibar ambayo iko Tanzania angepewa pia mwarabu...
 
Sasa hapa tatizo ni Uislamu au Uzanzibari?

Mi naona Tatizo ni uzanzibari ndio maana bandari ya Zanzibar hajapewa Mwarabu... Kama kweli mwarabu yuko vizuri na nia ni njema, Bandari ya Zanzibar ambayo iko Tanzania angepewa pia mwarabu...
Aspirin,
Nadhani kuna kitu labda umeghafilika kukisema kuwa hao Wazanzibari wote uliowataja ni Waislam na bandari wamepewa Waislam.

Mwarabu chembelecho hana "nia nzuri."

Tufahamishe nani mwenye nia nzuri anaestahili kupewa bandari?

Dr. Slaa na Dr. Kitime viongozi wa juu katika Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Tanzania Episcopal Conference wamepinga bandari kupewa Waarabu.

Fanya uchunguzi kidogo kubaini wanaopinga bandari kupewa Dubai.

Wote wqna rangi moja.
Hii inaashiria nini?

Ikiwa kutakuwa na viongozi wanaowajengea Watanzania hisia za kuendesha nchi kwa misingi hii ya ubaguzi kuna mengi yatahojiwa na kuombwa kutolewa maelezo.

Nina hakika serikali itataabika sana na kusababisha uadui.

Kuna mambo ningeweza kuyaeleza hapa lakini kwa ule uzito na unyeti wake nashindwa.

Najiuliza swali moja tu.

Tumefikaje hapa na ni nani aliyetufikisha hapa?
 
Nani kakuambia nimeghadhibika? Nimekuambia mbona haukukemea wakati wazungu wanaitwa majina mabaya na ya kashfa?
Mna...
Ikiwa hujakasirika na unaandika hivyo kuniijumuisha kama ulivyonitaja, "Waarabu wenzio," liko tatizo kwako labda hulitambui.

Mimi si Muarabu.
 
Back
Top Bottom