SoC02 Hisia za Mapenzi zinavyoteswa na ugumu wa maisha

Stories of Change - 2022 Competition
Aug 14, 2022
2
1
TAZAMA HISIA ZA MAPENZI ZINAVYOTESWA NA UGUMU WA MAISHA

Wanajukwaa hili pendwa kabisa napenda kuwaletea mambo kadhaa ambayo kwa namna moja au nyingine yamepelekea watu wengi kutofurahia mahusiano pengine pasipo wao kupenda .

 Ni dhahiri kabisa wanaume na wanawake wote kwa pamoja huathirika kimahusiano kwa sababu ya ugumu wa maisha au uchumi duni unaowakumba wahusika .

Pole dada yangu kwa kuamka usiku wa manane na kuanza kujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu halali na halisi kichwani mwako ,

1. unajiuliza nipate wapi pesa ya kununua pedy nasiku za hedhi zinakaribia?

2. Nimemaliza elimu yangu ya chuo kikuu ajira hakuna hata dalili ya kuajiriwa kwa kile nilichosomea haionekani kabisa nifanye kipi ili nipate kujikimu?

3. Wazazi wanaamini Mimi ni MTU mzima sipaswi kuwategemea wao tena kwa tamaduni zetu tulishazoea ukifikisha miaka kumi na nane wewe unapaswa kujitegemea sasa nitajitegemea kwa kipi nilichonacho?

4. Pengine Mimi ni mtoto wa kwanza wadogo zangu wananiomba pesa ndogo tu ya kununua daftari kwa kuamini Mimi ni dada yao naweza kuwasaidia ukweli ni kwamba sina hata senti mbovu nitawasaidiaje?

5. Wazazi Wangu waliamini kwa kiasi kikubwa sana kwamba Mimi ndio mkombozi wao wakajinyima nikasoma mpaka nikamailza elimu yangu sasa nitafanya nini ili watambue kwa kuaidika kwamba hawakupoteza pesa zao bure?

6. Wenye elimu ndogo wapo kwenye ajira na wenye elimu kubwa hawana ajira serikali imetumia mfumo gani huu?je ni mfumo wa haki?

7. Nimesoma kwa shida sana tukauza kila kitu kwa lengo kuu nitavirudisha vyote tulivyouza tena na zaidi pengine hata niliwaahidi wazazi na wadogo zangu vitarudi sasa mbona naonekana mfilisi wa familia?

8.Nilipata mchumba chuoni tukaanzisha mahusiano kwa kujali hisia za miili yetu pia tukaamini sisi ni watu wazima pia tukaamini tunaelekea kuhitimu masomo yetu na tunaenda kuajiriwa wote Mimi na mchumba Wangu tukajikuta mwaka wa mwisho ili penzi letu lisiingiliwe na mdudu tukaamua kuzaa kabisa sasa tuko mtaani kila mtu yupo kwao maisha magumu Mimi na mwanangu nipo kwetu nimeongeza ugumu wa maisha, Maana mpaka sasa mwanangu anahitaji huduma zinazonishinda sababu sina kitu niliiamini sana elimu.

 Daaah! kwanini umlaumu huyu dada kwa kudai kuwa haoneshi hisia za kimapenzi pale anapokuwa katika mahusiano?

Mzigo alionao kichwani ni mzigo mzito kupita mizigo yote iliyopo ulimwenguni atatua huu mzigo pale tu atakapokuwa na pesa zitakazokidhi mahitaji yake.

 Hisia katika mahusiano huchochewa na amani ya moyo na akili ikiwa katika utulivu .
Kaka kijana mwaminifu tena mwenye busara ila maisha magumu yamepelekea uonekane kijana au mwanaume usiejali, mlevi, msaliti wa ahadi zenu,huna utu,n.k

Ukweli ni kwamba wanaume wamekuwa katika changamoto kubwa sana labda kitamaduni zetu waafrika tumetwika kuwa kichwa cha familia .

Mengi umejaribu kufanya ili kutengeneza maisha bora lakini ndio kwanza kama ulikuwa unaharibu kwa makusudi ili uukaribishe umasikini.

Umesoma kwa bidii ili kuukimbiza ujinga na umaskini ,lakini umaskini umekita mizizi kwako maana elimu yako imekosa ajira.

Umeingia shambani kwa nguvu zako ndio ulime na uweze kuongeza kipato pengine upate na familia ndio kwanza masoko yanakosekana unauza kwa hasara hata mtaji wa kulimia hujauona.

Mke wako anakuomba pesa za mahitaji ya msingi kabisa katika familia unakosa pesa hiyo wakati huo huna kabisa anaamua kukusaliti ukapata taarifa unavurugwa na maisha unavurugwa na mapenzi basi akili inachoka kabisa unakata tamaa unakuwa hujijali unaonekana umekuwa mwehu kwa kutokujijali unadharaulika mazima wanakuhesabu katika kundi la vichaa waliopo mtaani pale.

Wadogo zako wanakuomba pesa kama kaka yao unawaeleza sina kitu kwa kuwa unajitahidi kujijali kimavazi wanaamini hutaki kuwasaidia wanaanza kukutenga katika familia unajikuta mpweke huna ndugu kisa ugumu wa maisha unashinda unawaza.

 Mwanamke uliempenda kwa dhati umeshindwa kumuoa kisa hali ngumu ya maisha uliyonayo wazazi wanataka mahari kubwa kwa kuamini binti yao wamemlea na kumsomesha kwa gharama kubwa sana hivyo wameona sehemu ya kurudisha gharama yao ni mahari nitakayolipa wakati huo hiyo pesa inayohitajika sijawahi hata kufikiria kuipata nimemkosa mke wa ndogo yangu nawaza kama nitaoa hatakuwa chaguo langu la kwanza.

Kwanini umlaumu mwanaume huyu kwa kuonekana hana nguvu za kiume au kutokuwa na hisia katika mapenzi wakati anateseka na mzigo mzigo akilini mwake?.

 Ukweli ni kwamba mapenzi bora hujengwa na afya bora ya akili na amani ya moyo.


Mambo machache yatakayoweza kutuondoa katika msongo wa mawazo uliosababishwa na uchumi mbovu.

1. Tuache kuamini elimu ni kwa ajili ya kuajiriwa .

2. Tuepuke kuchagua kazi za kujitafutia ridhiki kuanzia Leo pengine kutokana na elimu tulizonazo.kazi nyingi ni za hali ya chini lakini zinampatia kipato mhusika kwa kuamini asipokuwa makini atafilisika maxima hivyo kwa uoga huo hujikuta anakuza kipato chake.

3. Epuka kutegemea mafanikio makubwa kwa muda mfupi kwani hats wateja watakuja taratibu huku wakiongezeka kadri siku zinavyosogea kutokakana na huduma bora unayowapatia

4. Nidhamu ya pesa izingatiwe kwa kuwa na matumizi yanayolinda kipato chako tena tumia kwa kuogopa kiasi kwamba unaiba hali ya kuwa ni kipato chako.

5. Epuka starehe wakati wa utafutaji pia utakapofanikiwa Epuka starehe za ufujaji ulichokipata kitadumu.

6. Watanzania tupeane fursa pia tubebane usifurahie mwenzako anatembea peku wewe upo kwenye gari kwani ukipata pancha mtembea peku atakusaidia kuziba pancha hivyo kumbe anauwezo wa kusaidia mpe maarifa huenda upeo wako ukamtajirisha nae akaja kutajirisha wengine

SERIKALI IWAPOKEE KATIKA HILI
serikali inapaswa kuwapokea watu hawa kwa kuwasaidia mambo yafuatayo:
1. Kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa jinsia zote ili kuwasaidia katika kujishughulisha kama wajasiriamali wadogo.

2. Serikali kutengeneza miundo mbinu mizuri itakayopelekea wajasiriamali hao kusafirisha bidhaa au kupokea bidhaa zao kwa gharama nafuu.

3. Serikali kutengeneza masoko yatayosaidia wajasiriamali kukutana na kufanya biashara zao kwa urahisi pia kwa pamoja ambapo soko husababisha wateja kupata huduma zao bila kuhangaika hivyo kupelekea nafuu kwa mjasiriamali.

4. Elimu ya ujasiriamali itolewe kwa wajasiriamali kuepuka kupotea kwa mikopo yao na kuwapelekea hasara.

5. Serikali kuwaondolea kodi kabisa wajasiriamali wadogo ili wakuze mitaji yao

6. Serikali kama inaona baadhi ya taaluma hazina uhitaji kwa sasa itoe tamko ili kuepuka watu kusomea taaluma ambayo atatumia pesa zake kusoma halafu anakosa ajira bora pesa hiyo angewekeza katika ujasiriamali huenda angekuwa tajiri au serikali iande mitaala mingine itayofundishwa na yenye kuendana na uhitaji wa maisha ya sasa.

Wanajukwaa hili Mimi ninawaaga kwa hayo ninachowaomba tuyazingatie yote ili tuweze kuvuka kipindi hiki cha kuishi duniani.

"Binti wa kike ndio mtu pekee mwenye mtihani mkubwa wa kumtambua mchumba wa kweli yupi katika maisha yake, aliyemdharau kumbe alikuwa ni Mme wa maisha ya furaha katika maisha yake,alimtegemea kumbe amekuwa Mme wa kumkosesha usingizi kila siku".
 
Ujumbe bora ukufaao maishani usiwaze saaaana wewe ridhiki yako imepangwa na mungu na itakuja kwa wakati wake cha msingi jibidishe kilichopo mbele yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom