D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,160
- 3,259
Habari wanajamvi,
Siku ya juzi tarehe 19 september 2023 tumeletewa notisi ya malipo ya kodi ya ardhi (nimeambatanisha) ikiamrisha tulipe kodi ya ardhi jumla ya shilingi 244,700/=tshs
Kodi ya mwaka huu ni 7,500/=tshs
Baada ya kuulizia afisa mtendaji yeye anadai jumla ya hilo deni ni tangu mwaka 1996.
UTATA ULIPO (na ndipo nahitaji msaada wa wanasheria na wataalamu)
1: hili eneo marehemu baba yangu alinunua pagale na kulikarabati na kuwa nyumba kamili ya kuishi mwaka 2005 lakini jina la kwenye hii notisi sio la marehemu baba yangu aliyekuwa mmiliki wa eneo hili wala sio la mtu aliyemuuzia(baba yangu aliuziwa hili eneo) yaani jina silitambui
2: Karatasi ya kuandikishana mauziano ya hilo pagale nayo kwa bahati kwa bahati mbaya ilipotea.
3: Kuhusu kodi ya jengo tushalipia sana tu ila kwa sasa wanakata kwenye umeme(japo hata risiti za zamani pia hamna )
4: Gharama walizoandika NI :-
TOZO YA MWAKA 2023/2024 7,500/=
MALIMBIKIZO 150,210/=
TOZO 144,450/=
hapo kiuhalisia jumla ni 302,160/= Lakini wameandika Jumla ni 244,700/=
Wamefika wakamkabidhi mtoto mimi sikuwepo.
Je msaada wa wataalamu ni upi hapo maana nimechanganyikiwa na sina hata pa kutoa hizo fedha kwa sasa pili sielewi kama hicho kiwanja ni hiki kweli au vipi kutokana na majina kutoyatambua
Msaada wa haraka tafadhali