Hili la Uongozi wa Chawa wa Mama ni la kweli?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,252
113,647
IMG_4581.jpeg


Hivi hili jambo ni la kweli au ni utani tu wa kwenye mtandao?

Natamani lisiwe la kweli. Natamani liwe ni vijimambo tu vya kwenye mtandao.

Hayo ndo matamanio yangu.

Lakini kwa niwajuavyo Watanzania, jambo kama hili lawezekana kabisa!

Tuna idadi kubwa sana ya watu walio wajinga [rejea maana halisi ya neno] na walio wapumbavu.

Mimi ni muumini madhubuti wa haki za binadamu.

Haki ya kuwa mjinga na mpumbavu nayo ni haki ya kibinadamu.

Hivyo, kama ni kweli, hao walioamua kuwa chawa wa mama wanayo haki ya kuwa wajinga na wapumbavu.

Nami ninayo haki ya kuwa shangaa kwa ujinga na upumbavu wao.

Tanzania huenda ikawa ni nchi yenye idadi kubwa sana ya watu walio wajinga na wapumbavu.

We have a profoundly stupid populace.

Shameful.
 
Sikuamini macho yangu siku ile niliyoona maandamano asubuhi na bango kubwa mbele yao limeandikwa "CHAWA WA MAMA" Hivi kweli mama anakubali kuwa na chawa. Hongera ndg kwa kuwa muumini madhubuti wa haki za binadamu.
 
Yes, na huyo mama yao anautambua uwepo wao, na hiyo taasisi ilikuwa inatafuta kusajiliwa rasmi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom