Mr.Junior
JF-Expert Member
- Sep 8, 2013
- 11,797
- 10,003
Poleni kwa msiba. Huduma zinalipiwa kulingana na matumizi ya mteja husika. Pia laki 7 ni ndogo sana ukilinganisha na gharama halisi, ujue hiyo laki saba ni baada ya kulipiwa na ruzuku ya serikali, bila ruzuku mteja angedaiwa hata milioni kadhaa kwa shida aliyokuwa nayo na matumizi yake. Kifo ni mapenzi ya mungu hakihalalishi kuondolewa deni. Niulize swali hivi ukinunua sukari dukani wakati unapokea ikamwagika unamwambia muuzaji kuwa nipe sukari nyingine kwa malipo yaleyale? au unalipia tena. Kumbuka siku si nyingi Raisi wetu alilazimika kumlipia mama mmoja hapa Muhimbili shilingi milioni 5 ili achukue mwili wa mama yake. Huu ulikuwa ni mfano tosha kuwa nini kinastahili .Kwa maana hiyo basi ni haki kulipia huduma. Kumbuka usipozichangia huduma iko siku utazikosa kwani zitakuwa zimeisha
Huduma zikosekane serikali ikiwa wapi, watu kila siku wanalipa kodi.
..........Laki saba ni gharama ndogo? Hivi unajua kuna mtu hawezi hata kupata Milo mitatu kwa siku na akiumwa anatakiwa apate matibabu mtu wa aina hiyo ataweza kulipa laki saba kweli?