Hii tabia ya trafiki kubambika makosa ya barabarani inaumiza

Mwee

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
240
602
Moja kwa moja kwenye kero yangu. Kumekuwa na mtindo wa askari wa usalama barabarani kusimamisha gari hata kama huna kosa halafu wanainakiri namba ya gari na kuiandikia fine. Binafsi nimekumbana na hali hii mara mbili sasa.

Mara ya Kwanza nilisimamishwa na askari kama kawaida akaomba leseni nikampa na akawa anatazama kama ina deni kisha akanirudishia. Kwa kuwa sikuwa na kosa lolote akaniruhusu niendelee na safari Mambo yakawa fresh. Siku zikasonga nikiendelea na mishe zangu na hapakuwa na deni lolote kwenye mfumo.

Sasa baada ya miezi mitatu nikasimamishwa mahali na askari wengine wakaja juu sana wakifoka kuwa nimelimbikiza deni kwa miezi mitatu hivyo natakiwa nilipe fine elfu sitini on the spot la sivyo sitaruhusiwa kuendelea na safari yangu. Nikauliza kulikoni, nikaambiwa ulipigwa fine kutokana kwenda spidi Zaidi ya 50 mahali nikatajiwa. Kuja kuvuta kumbukumbu ni pale yule askari aliyechukua leseni yangu na kujifanya anacheki deni.

Sikutaka niendelee na mabishano nikailipa. Sasa kero kubwa zaidi mpaka Nimelazimika kuandika hapa ni hivi wiki iliyopita tu nikiwa nimepaki gari yangu mahali nikiwa naendelea na mishe mishe zangu narudi nakuta plate number za gari zimefunguliwa na hazipo. Nikiwa nimetaharuki mashuhuda wakaniambia wamechukua askari. Kwenda kituoni baada ya kusota sana nikaja kuambiwa wiki tatu nyuma nilipigwa fine eti niliovertake mahali ambapo hairuhusiwi. Mtindo ule ule kama wa kwanza.

Sheria ya usalama barabarani inasema wazi kuwa kama ni fine askari atakuandikia pale pale na kukupa control namba ya kulipia. Lakini huu mtindo wa kubambikiza ni maagizo au kuna siri gani. Wengi wamelalamikia hili suala na hakika linaleta kero kubwa sana.
 
Back
Top Bottom