Hii ni kweli au imani tu??

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,702
Eti inasemekana mtoto wakati wa kukatwa kitovu kikiangukia katikati ya mapaja basi kama ni mvulana akikuwa atakuwa shosti, na msichana atakosa uzazi?
 
Duuu.... mkuuu hizi nyingine ni imani tu kwa waliombali kiimani na muumba wao!!!:tea:
 
Hata mimi nimesikia hizo, ila mimi lilinikuta la tofauti, mke wangu alisema kitovu huwa lazima kitupwe/fukiwa na mama mkwe au ndugu yoyote wa kike wa upande wa kiume, ilinipa shida sana kwani mimi si muamini sana wa hizi mila na pia tunatoka makabila tofauti.
Tulikuwa tunaishi Mkoa wa mbali na DSM na ndugu Mhusika alikuwa yupo DSM, yaani ilinibidi nigharimike aende huko kwa ndugu yangu kwa ajili hiyo.
 
Sasa ni kwa nini kitovu kinachukuliwa kwa umakini sana. Huenda kuna reason behind hizi imani kuhusiana na kitovu! Kwani ulipewa sababu gani za kitovu kufukiwa na ndugu wa ukweni?
 
Mkuu, Imani ni kitu kikubwa sana..., mfano kama jamii inaamini kitovu kisiangukie kwenye mapaja kikaangukia, malezi ya yule mtoto yanaweza yakapelekea hata yeye akajihisi ndivyo sivyo, na malezi / environment ndio zinazotufanya tuwe jinsi tulivyo..,

Kwahiyo hizi imani nyingine (ambazo hazina madhara) hata kama sio za kweli, ila kuwaridhisha wazazi na mababu inabidi tuzifate tu...,
 
Kwa nini tuzifuate tu ili tuwaridhishe? Kama hakuna madhara yoyote inabidi kuziacha na kuwaelewesha!!
 
Mkuu unaweza kumwelewesha bibi au babu yako ?, hapo utaambiwa hauna adabu na unaweza ukapewa laana bure.., na kama bibi anaamini hivyo alafu usifanye, je akianza kumuangalia mjuu wake kwamba hajakamilika?

Kwahiyo naona ni bora kama mila haina madhara, basi twende nayo hivyohivyo
 
Wanakatwa, wengine wanakihifadhi hadi kinakauka halafu wanakichimbia ardhini.
 
Mkuu unaweza kumwelewesha bibi au babu yako ?, hapo utaambiwa hauna adabu na unaweza ukapewa laana bure

Kwamba utapewa Laana nayo si ni imani potofu mkuu?
Au unaamini kuwa hilo suala huwa lipo kweli?
Mi siamini, labda mtu ajaribu kunilaani hapa ili nione....
 
Mkuu mimi binafsi haya mambo siyaamini..., lakini power of mind ni kubwa na kama jamii nzima itaamini kwamba wewe hauna adabu, na unabishana na babu na bibi zako, lile shinikizo la kwamba umekosa hata mambo yakienda kombo utaanza kurelate na makosa uliyofanya, bila kujijua unaweza ukakuta mambo hayakunyokei na confidence inakwisha

Hata kwenye michezo watu wana imani kuwa kitu fulani wakifanya itasaidia wao kufanya vizuri, mfano kina Fernando Alonso, Michael Jordan, n.k. unakuta wana kitu good luck charm siku wakikosa hicho kitu unakuta hawachezi vizuri sababu akili inawaambia kwamba kitu fulani hakiko sawa.

Kwahiyo hizi imani potofu (kama hazina madhara ) na ni utamaduni bora tuendelee kuzifanya iwapo zitawafanya wazazi wetu wawe happy, muda unavyozidi kwenda basi tutabadilika..,
 
Sasa ni kwa nini kitovu kinachukuliwa kwa umakini sana. Huenda kuna reason behind hizi imani kuhusiana na kitovu! Kwani ulipewa sababu gani za kitovu kufukiwa na ndugu wa ukweni?

Ya nini ndugu yangu sikutaka kuumiza kichwa changu kwa kutaka sababu, nilibisha bisha kidogo lakini nakaona isiwe taabu nikaacha afanye anavyotaka. Tunatoka makabila tofauti.
 
Kila kabila lina iman yake kuhusu kitovu. ni iman tu hakuna madhara yoyote me kaka yangu alidondokewa yupo hadi leo na kaoa ana familia. Wengine wakitahiriwa kile walichokatwa kinarudi home kwa babu.
 
Duh hii kali sasa, ila hizi imani zetu si bure kuna kitu nyuma yake ambacho bado hatujafanikiwa kukijua na sisi tunayachukulia haya mambo juu juu tu! Kuna haja ya kufanya utafiti zaidi
 
we ilijuaje kuwa kakayako aliangukiwa?, na kama kweli aliangukiwa unajuaje kuwa hakupewa tiba?, nasikiaga mtoto akiangukiwa nakitovu inabidi aingize ka bamia kwenye kitumbua cha mama.....................
 
Mkuu unaweza kumwelewesha bibi au babu yako ?, hapo utaambiwa hauna adabu na unaweza ukapewa laana bure.., na kama bibi anaamini hivyo alafu usifanye, je akianza kumuangalia mjuu wake kwamba hajakamilika?

Kwahiyo naona ni bora kama mila haina madhara, basi twende nayo hivyohivyo
Twende nazo hivyohivyo inawezekana kuna ukweli ndani yake.
 
Duh hii kali sasa, ila hizi imani zetu si bure kuna kitu nyuma yake ambacho bado hatujafanikiwa kukijua na sisi tunayachukulia haya mambo juu juu tu! Kuna haja ya kufanya utafiti zaidi
Kweli kabisa huenda kuna kitu na ukweli wa hizi imani, ujuaji tu unatupa kiburi....
 
Kwamba utapewa Laana nayo si ni imani potofu mkuu?
Au unaamini kuwa hilo suala huwa lipo kweli?
Mi siamini, labda mtu ajaribu kunilaani hapa ili nione....

Laana zipo ndugu............ahaaaaaaaaaah unataka ulaaniwe hapa, kwa kosa gani ulilofanya?????
 
we ilijuaje kuwa kakayako aliangukiwa?, na kama kweli aliangukiwa unajuaje kuwa hakupewa tiba?, nasikiaga mtoto akiangukiwa nakitovu inabidi aingize ka bamia kwenye kitumbua cha mama.....................

Du!!!!!
 
Back
Top Bottom