hii ni kwa washabiki wezangu wa barca tu

chebi

JF-Expert Member
Nov 10, 2012
1,737
761
jamani mimi mwenzenu usingizi siupata usiku huu yaani nashindwa kuamini tumekula 4-0 dah kweli mpira unadunda kwa wale wezangu hebu nipeni moyo gem ya marejeo tuna tamaa ya kushinda 5-0 iyo ndio ile tamaa ya fisi kumuona mtu anakwenda na anatamaa mkono utaanguka aah!! mimi nasema ndio soka ila barca tuna tatizo la beki washabiki wezangu mtanisamehe kama kuna kitu kimewachoma hapo
 
hii imekaaje fcb.PNG
 
Sikia chebi, kil kitu kina wakati wake au katika mipira ya wenzetu kuna kitu kinaitwa cycle. Utakuta timu inatamba kwa kipindi fulani halafu inapotea kabisaaaaaa. Nikupe mfano: Miaka ya 50 kulikuwa na Real Madrid, 60 Benfica ya Ureno chini ya Eusebio, 70 kulikuwa na Liverpool pamoja na Ajax. Miaka ya 70 mwishoni na mwanzoni ya 80 kulikuwa na timu za Uingereza (Nottingham Forrest, Aston Villa, Liverpool), katikati ya miaka ya 80 na 90 timu za Italia haswa AC Milan. Miaka hii ya karibuni ni Barca imechukua kombe mara tatu, Man Utd. imechukua kombe mara moja na imefika fainali mara tatu. Kila kitu kina mwisho wake, na Barca waliponea chupuchupu tu kwani ilibidi watolewe na AC Milan kwenye robo fainali, ila basi tu.
 
Last edited by a moderator:
Chebi

Mliifunga AC Milan mabao 4.
Kama mliweza kufunga nne. mtaweza kufunga tano.

Mtakapoweza kufunga tano na kulinda lango lenu kwa ukuta wa zege ni wazi kitakapopulizwa kipenga cha dakika 90, wachezaji wenu watakuwa wametoa ulimi kama wa mbwa aliyekimbizwa na wakorea kwa ajili ya mboga!
 
Sikia chebi, kil kitu kina wakati wake au katika mipira ya wenzetu kuna kitu kinaitwa cycle. Utakuta timu inatamba kwa kipindi fulani halafu inapotea kabisaaaaaa. Nikupe mfano: Miaka ya 50 kulikuwa na Real Madrid, 60 Benfica ya Ureno chini ya Eusebio, 70 kulikuwa na Liverpool pamoja na Ajax. Miaka ya 70 mwishoni na mwanzoni ya 80 kulikuwa na timu za Uingereza (Nottingham Forrest, Aston Villa, Liverpool), katikati ya miaka ya 80 na 90 timu za Italia haswa AC Milan. Miaka hii ya karibuni ni Barca imechukua kombe mara tatu, Man Utd. imechukua kombe mara moja na imefika fainali mara tatu. Kila kitu kina mwisho wake, na Barca waliponea chupuchupu tu kwani ilibidi watolewe na AC Milan kwenye robo fainali, ila basi tu.
Upotoshaji si kitu kizuri. Ukweli ni kwamba Manchester United imetwaa ubingwa wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE mara tatu na sio mara moja. Tafuta data ambazo ni credible and authentic kabla ya kuandika.
 
Last edited by a moderator:
ungewewka na waale magorikipa wa baca ingependeza

Hawa washazoea kubebwa! Hakuna tatizo katika magoli yalofungwa. Ilo la kwanza ndo kabisaaa wabataka kumsingizia eti kampandia mwenzake wakati jamaa ame fanya sawasawa, mpira wa kona hauna offside.... Na jamaa kapewa ubavu... Tatizo wachezaji wa spain wanakula tambi tu ukimgusa kidogo wanataka foul! Tena swaiba barca ilikuwa na magoalkeeper watatu, lakini wapiiii, wale wawili jamaa hajaeka picha zao mana aibu eti
 
tafiki huyu mtu tungemuuliza kwanini hao wala tambi kila wakifungwa goli wanamfata refa
 
Hawa washazoea kubebwa! Hakuna tatizo katika magoli yalofungwa. Ilo la kwanza ndo kabisaaa wabataka kumsingizia eti kampandia mwenzake wakati jamaa ame fanya sawasawa, mpira wa kona hauna offside.... Na jamaa kapewa ubavu... Tatizo wachezaji wa spain wanakula tambi tu ukimgusa kidogo wanataka foul! Tena swaiba barca ilikuwa na magoalkeeper watatu, lakini wapiiii, wale wawili jamaa hajaeka picha zao mana aibu eti

Wala tambi wakiwa barcelona au spain?! Kama ni spain sahau labda kama ni barceleona na kama ni barcelona logically you are very wrong!!
 
Upotoshaji si kitu kizuri. Ukweli ni kwamba Manchester United imetwaa ubingwa wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE mara tatu na sio mara moja. Tafuta data ambazo ni credible and authentic kabla ya kuandika.

Mkuu MNYISANZU umelewa? Usipende kuropoka ama kutokwa na povu kujibu watu wakati haulewi point. Nimesema mipira ya wenzetu ina kitu kinaitwa cycle ama mzunguko kwa lugha ya kwetu. Na nikasema kwa miaka hii ya karibuni Barca imechukua kombe mara tatu na Man Utd mara moja na imefika fainali mara tatu. Kumbuka nimezungumzia cycle ya hivi karibuni na si mwaka 1968, na 1999 wakati Man Utd. imechukua ubingwa wa Ulaya. Je, bado haujaelewa? Ebu rudia kusoma point yangu tena.
 
Last edited by a moderator:
Ah! Hiyo ni ajali kazini tu. Mwakani tutarudi strong as ever baada ya kufanya marekebisho sehemu stahili. Si unakumbuka mwaka tunapigwa na Inter Milan ya Mou? Kilichotokea mwaka uliofuata sote tunakijua.
 
Upotoshaji si kitu kizuri. Ukweli ni kwamba Manchester United imetwaa ubingwa wa UEFA CHAMPIONS LEAGUE mara tatu na sio mara moja. Tafuta data ambazo ni credible and authentic kabla ya kuandika.

Jamaa kasema miaka ya hivi karibuni kwa hesabu za haraka haraka jamaa anamaanisha tangu 1999 hadi 2013. Nadhani yuko sahihi
 
Barca ili ifuzu kwa fainali nadhani little Mesi anatakiwa angalau apige bao 3 peke yake la sivyo wasahau. Ila kwa miaka takribani 14 hivi kama sijakosea timu zinazoingia fainali ya klabu bingwa ya ulaya na kuluzi au kushinda fainali zinakawaida ya kuingia fainali tena msimu unaofuata au hata kuishia nusu fainali. Maoni yangu nadhani wazee wa munich ni zamu yao kunyanyua hiki kikombe 2013
 
Back
Top Bottom