Hii ni kwa wanaume wanao penda watoto wa shule tu

Haliali

JF-Expert Member
Oct 1, 2012
574
263
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mpanda imemuhukumu Kassim Lugendo (41) mkazi wa Kijiji cha Kambanga kifungo cha miaka 10 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumnyonya ulimi msichana mwenye umri wa miaka 13, mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Igalula bila ridhaa yake.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga Tengwa, alisema ametoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Alisema ushahidi wa upande wa mashitaka na utetezi, umethibitisha kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo.
Akitoa utetezi wake kabla ya hukumu hiyo, mshitakiwa aliiomba mahakama isimpe adhabu kwa kile alichodai ana familia ya watoto saba na wazazi wake wote wawili ni walemavu na wanamtegemea yeye.
Pamoja na utetezi huo, hakimu Chiganga alisema kitendo alichokifanya mshitakiwa ni cha hatari, kwani kinaweza kikamsababishia msichana huyo kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).
Awali, mwendesha mashitaka Ally Mbwijo alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi 30 mwaka jana, majira ya saa 6 mchana akiwa nyumbani kwake.
Alidai siku hiyo msichana huyo akitoka shuleni akielekea nyumbani kwao, mshitakiwa alimuita na kisha kumwingiza kwa nguvu ndani ya nyumba yake na kumnyonya ulimi pamoja na kumwingiza vidole vyake sehemu za siri.
Alielendelea kudai kuwa wakati akimfanyia vitendo hivyo, msichana huyo alipiga mayowe na ndipo majirani wafika na kumkuta akifanya kitendo hicho huku sehemu ya sketi ya msichana huyo ikiwa imefunuliwa.
 
Duh...
Sijui kwa nini serikali isihalalishe tu biashara ya ukahab...
 
Hata adhabu aliyopewa naona ni ndogo. Alishindwaje kuwanyonya ndimi watoto wake kama ameshindwa kwa mkewe?
Ningekuwa hakimu ningemhukumu miaka 50 jela, pamoja viboko 50 anaingia na vingine 50 akitoka.
 
Yaani huyo maaluni ana mke na watoto 7. Ukahaba si angefanya na mkewe ama wanae? Fedheha tupu sijui wanae wanapitaje barabarani!
Duh...
Sijui kwa nini serikali isihalalishe tu biashara ya ukahab...
 
Back
Top Bottom