Hii ni kawaida kwenye mapenzi au?

Apollo

JF-Expert Member
May 26, 2011
4,920
3,221
Mimi ninajiuliza sana, kwanini kuna watu wakiwa wanaanza mahusiano wanakuwa na jitihada na juhudi nyingi kunogesha mapenzi mfano kukupigia simu, kukupa kadi na zawadi na kuonyesha upendo alafu baada ya muda wanachoka. Yaani wanapunguza upendo sijui niseme wanachoka. Unakuta anapunguza muda wa kukupigia simu au ukimpigia anajifanya busy. Tena unakuta mwingine hana mpenzi pembeni wala hatoki nje ila anakuwa anapunguza upendo. Why? Ni kawaida kuwa mapenzi yananoga then yanapoa au ni mtu tu na tabia yake au hisia zake? Mbona kuna wengine wamedumu kwa miaka mingi ilia hawachokani? Msaada please!

NA SOLUTION YAKE NI NINI?
 
Mara nyingi wapenzi wakiishi au kuwa katika mahusiano ya muda mrefu wanasahau vitu vidogo vidogo ambavyo in real sense vinadumisha mapenzi... But si kwamba mapenzi yanapungua.. Kwa mwenye busara akishagundua mapungufu atafanya jitihada za kurudisha that "sparkle" between them kwa asieona umuhimu ndio hivyo wanaishia kuachana wote wakiwa na conception kwamba mwenzie amemchoka!
 
Yes, na hicho ndio nilipenda kujua, kumbe ni kawaida? Maana wengi huwa wanaona kama mmechokana. Tena kwa visingizio vidogo tu.
 
Si kawaida,from no where mtu kupunguza mawasiliano na mpenz wake bila hata ya kuwa na mtu nje,lazima kunatatizo.Jaribun kulitatua..hakunaga kuchokana kwa wapenzi..

Kaeni nyote wawili mtatue tatizo hilo la ukimnya.There must be wrong somewhere.
 
mwanzoni mambo moto moto bana na pia wajua hii ni kutofahamu wat relationships are. unampa unrealistic expectations mwenzio maana kwenye mapenzi hamtapigiana simu kila leo au kutoka out kila mara. cha msingi nikumtendea mwenzi yale mambo ambayo kweli kabisa utaweza kuendelea kumtendea ata baada ya kuwa kwenye uhusiano miaka kadha.
 
kumbe ni uchumba kpnd ambacho hamkua na majukumu ata yakumfulia na kumvsha mtoto nakupanga maendeleo mengne, maisha c maigzo!
 
watu wengi huanza mahusiano kwa mbwembwe hizo za simu kadi etc mwezekana ukawa wewe ndo unavilazimisha ndo maana huyo atavifuata kwa muda. maana ni maigizo havitoki moyoni na hasa mkikwaruzana kidogo ndo kabisa vinapotea
 
kipya kinyemi ndugu, mapenzi mapya huwa moto moto but mkishazoeana yan baada ya kukaa muda mrefu lazima ile kasi ya mapenzi itapungua tu, mnakuwa hamna jipya tena kila mtu nw anaishi real mauongo ya mtu kupretend yamewekwa kwando.
well ni kawaida tuu.
 
Nawashukuru sana kwa michango yenu. Nathani watu wa siku hizi wanaiga na wanataka kuwa na mapenzi ya kinamarichui au ya kifilipino. Nimejifunza mengi kutoka kwenu.
 
Ila nilishawahi kuwa na mwanamke mmoja hivi, eti kuna kipindi nikimpiga (nilikuwa nampigia simu kila siku night ili nimjulie hali) eti ananiambia ''mbona unanipigia sana? Mi sitaki unipigie simu kila saa'' ni mwanamke ambaye nilimgundua anachoka mahusiano sana. Tena nikifikiria kuwa alioachana nao wengi walimwacha kwa sababu hii. Mtu kama huyu utaishi naye vipi?
 
Mimi ninajiuliza sana, kwanini kuna watu wakiwa wanaanza mahusiano wanakuwa na jitihada na juhudi nyingi kunogesha mapenzi mfano kukupigia simu, kukupa kadi na zawadi na kuonyesha upendo alafu baada ya muda wanachoka. Yaani wanapunguza upendo sijui niseme wanachoka. Unakuta anapunguza muda wa kukupigia simu au ukimpigia anajifanya busy. Tena unakuta mwingine hana mpenzi pembeni wala hatoki nje ila anakuwa anapunguza upendo. Why? Ni kawaida kuwa mapenzi yananoga then yanapoa au ni mtu tu na tabia yake au hisia zake? Mbona kuna wengine wamedumu kwa miaka mingi ilia hawachokani? Msaada please!

NA SOLUTION YAKE NI NINI?

hapo ndugu tatizo laweza kuwa ni wewe mwenyewe, unaweza ukawa umeanza wewe kumpotezea nae anaamua kupotezea taratibu... usilopenda kutendewa usimtendee mwenzio
 
Mara nyingi msingi wa mapenzi hayo yalianza kwa kasi, unapoanza kwa kasi ni lazima utachoka ni bora kuanza taratibu kwani mvua ya nguvu ikikata imekata ila mvua ile ndogo hunyesha kwa muda mrefu
 
hii hutokea mara nyingi kwa msichana labda alipenda sana mwishon akaja kuumizwa,hata akipata mwingine anajua ataumia tu.hivyo huogopa kuingia katika mahusiano ya uharaka,nenda nae taratibu,ata change tu.Hata kwa mwanaume ni kitu kile kile.
 
Majukumu yanachangia sana. Mfano mkiwa bf na gf mnakuwa nyie wawili tu, mkiwa kwenye ndoa mtakuwa na mtoto au watoto, mashemeji na mipango mingine ya maendeleo, hivyo vitu vingine vinakuwa very minor.

Lakini pia kuna mambo mengine ambayo yanachangia, huenda bado ni gf na bf, kila weekend unataka mwende out wakati mwenzio hali si shwari, yupo anayeweza kukuambia na kama wewe ni mwelewa itakuwa poa, kama si mwelewa basi atajifanya yupo busy
 
inaweza ukawa sahihi, but mbona kuna wanawake wengine siwezi kuwachoka wala kupunguza upendo kwao?
 
Mara nyingi msingi wa mapenzi hayo yalianza kwa kasi, unapoanza kwa kasi ni lazima utachoka ni bora kuanza taratibu kwani mvua ya nguvu ikikata imekata ila mvua ile ndogo hunyesha kwa muda mrefu

true, mvua ndogo hunyesha kwa muda mrefu.
 
hii hutokea mara nyingi kwa msichana labda alipenda sana mwishon akaja kuumizwa,hata akipata mwingine anajua ataumia tu.hivyo huogopa kuingia katika mahusiano ya uharaka,nenda nae taratibu,ata change tu.Hata kwa mwanaume ni kitu kile kile.

ulijuaje? Maana kuna msichana mmoja ninamjua, aliumizwa na anawasiwasi wa kuumizwa tena mpaka leo.
 
Majukumu yanachangia sana. Mfano mkiwa bf na gf mnakuwa nyie wawili tu, mkiwa kwenye ndoa mtakuwa na mtoto au watoto, mashemeji na mipango mingine ya maendeleo, hivyo vitu vingine vinakuwa very minor.

Lakini pia kuna mambo mengine ambayo yanachangia, huenda bado ni gf na bf, kila weekend unataka mwende out wakati mwenzio hali si shwari, yupo anayeweza kukuambia na kama wewe ni mwelewa itakuwa poa, kama si mwelewa basi atajifanya yupo busy

yes mkuu. Pia majukumu huchangia.
 
muda mwingine ni hisia tu utakuta wala hujachokwa ...inawezekana mlianza mapenzi mkiwa chuo/shule hapo muda huwa ni mwingi na majukumu huwa ni machache,,ukianza kazi mbaya zaidi unakaa dar ambapo inakulazimu uamke saa kumi kisha unarudi saa 4 usiku ,ukifika umechoka alafu stress za kazini na hali ya maisha ,lazima upunguze kufikilia mapenzi.
 
Back
Top Bottom