Hii ni Haki kweli???

Jimmy Romio

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
367
278
Leo mida ya saa moja na nusu nilikuwa napita barabara ya New Bagamoyo pale mitaa ya Lugalo, kulikuwa na kifoleni cha kiaina. Basi km kawaida watu wa pikipiki wakawa wanatanua, kufika hapo lugalo hamadi!!!!! wanajeshi hawa hapa.....! wanasimamisha pikipiki na bajaji zinazotanua. Jamaa mmoja wa pikipiki(akiwa anatoka mwenge) alivyowaona tu akawa anarudi kati kwa ghafla, mara akajaa kwenye salon ya mama mmoja hivi puuuu! chini..! Huyu mama alikuwa anaelekea mwenge. Wanajeshi walifika pale fasta, hakuna cha kutoa pole wakaanza kumshambulia kwa buti zao..., makofi... ngumi.. mitama n.k. Sasa nikawa najiuliza wanajeshi walukuwa sahihi kweli? Ndio jamaa ana kosa, lakini si wangemkamata wampeleke kunakohusika? Au wao kujichukulia sheria mkononi ni sawa? ILA JAMAA ALIKULA KIPONDO CHA UHAKIKA! DUH!
 
Sio sahihi. Ni uonevu. Uvunjaji wa haki za binadamu.
 
Bora hiko kichapo kitakua kilimpunguzia hasira huyo mama, japo km mkoko umeharibika lazima atengeneze maana boda boda kumlipa kazi itakua kwa gari........ Wanakeraga sana madereva wa piki piki. Wanajeshi hawako sahihi, piki piki hawako sahihi......
 
Back
Top Bottom