Hii ndiyo siku niliyotambua kuwa wanawake ni wauaji na wanaweza kukusababishia kifo usipokuwa makini

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,732
Nakumbuka nikiwa mgeni ndani ya mji wa morogoro/mji kasoro bahari nilipata mchumba(mwanamke) mtaani nilipokuwa naishi, panaitwa Mafiga. Yule manzi alikuwa anakuja geto, sometimes analala lakini kimazingira alikuwa anaishi kwao kwa wazazi wake, inapotokea wazazi hawapo alikuwa anaibuka kwangu tunajiachia, kiukweli nilimpenda/nilifurahia.

Background ya huyo mtoto wa kike kipindi namtongoza ili NALIA NGWENA nipate kumpata awe ananifariji moyo, aliniambia kuwa alikuwa na boyfriend wake wakaachana kwa kuwa jamaa hamjali kabisa.

Mwamba nilikaza nilimuahidi kuwa sitomtenda wala kumfanyia alichokuwa anafanyiwa na jamaa yake kiufupi alinielewa tukawa wapenzi.

Kuna siku moja mishale ya saa tatu usiku tukiwa tumesima kwenye mti karibu na kwao nikiongea nae mazungumzo ya kawaida, walitokea jamaa wawili, mmoja alisema, "Kumbe pamoja na huduma zote ninazokupa kumbe unanichanganya na huyu boya, leo utanitambua na huyu jamaa yako!"

Nikiwa katika hali ya mshangao, nilishangaa yule msichana kapigwa bonge la kofi, alipiga ukelele mkubwa wa maramoja.

Nilipoona hivyo nikamuuliza jamaa vipi? Hakutaka majadiliano akanigeukia, kaja mkuku mkuku kichwa ndipo nilipoona hakuna amani tena. Nilimtuliza na punch moja ya mbavu akadondoka. Ikawa vita sasa, yule mwenzake naye akaja kama kalewa nikamgusa shingoni kama nachinja, haja kaa sawa nikapiga mtama akadondoka chini.

Yule mwanamke alipoona fujo zinaendeleea alikimbiana kutokomea nyumbani kwao. Kelele ziliwashitua watu wakamwamsha Mwenyekiti wa Serikali za mtaa alikuja speed sana vijana wake kadhaa wa sungusungu/police jamii, alipofika maeneo yetu alipiga filimbi nakusema mpo chini ya ulinzi.

Mjumba nilitii filimbi nikaachana na maugomvi, Mwenyekiti alipofika pale alitutambua wote na kusema vijana wangu mbona mnaleta fujo, kesho mje ofisini.

Kesho yake nilienda ofisini, nikiwa nimekaa pale nilimuona jamaa anakuja na yule dada. Kiufupi yule mwanamke alikuwa anatuchanganya na jamaa nae alikuwa anagharamika sana kwa huyo mtoto wa kike na chakushangaza yule mwanamke alipofika pale kwa Mwenyekiti alinikataa katakata na kusema nilikuwa namtongoza na kumuomba namba, hanijui na wala hajawahi kuniona kabisa na ile siku usiku ilikuwa ndiyo mara ya kwanza!

Sikutaka mambo yawe mengi, nilimpa mkono wa kwa heri Mwenyekiti na kuondoka zangu. Ila nilipata funzo, wanawake asilimia kubwa siyo watu wa kuwaamini kabisa katika ulimwengu huu.
 
FB_IMG_16812767897677396.jpg
 
Pole sana mkuu hawa viumbe wana undugu wa damu na shetani.

Mkuu Mungu alikwisha tuambia tuishi nao kwa akili. Nina uhakika huyo demu kama ungelikutana nae tena chemba angelikurudia na kukuomba msamaha tena hawa viumbe si mayuda hawa...!?
 
Pole sana mkuu hawa viumbe wana undugu wa damu na shetani.

Mkuu Mungu alikwisha tuambia tuishi nao kwa akili. Nina uhakika huyo demu kama ungelikutana nae tena chemba angelikurudia na kukuomba msamaha tena hawa viumbe si mayuda hawa...!?
Mzee aliniruka futi Mia mluguru Yule
 
Back
Top Bottom