Hii ndio Historia Kuntu ya Somalia

Wasomali ndiyo kabila pekee wanaopigana ndugu kwa ndugu bila maelewano takriban miaka 20 sasa.

Naona huu ni ujinga.

Wasomali pia ni maarafu kwa kuwashona mabinti kwenye papuchi zao na kuacha tundu la kukojoa kwa lengo la kuhifadhi ubikra. So inhuman
 
Mtoa mada alikuwa na lengo zuri la kutuhabarisha kuhusu historia ya Somalia ila amepotosha sana mambo mengi.. inaonyesha hakufanya utafiti mzuri kwenye mada yake..

Machache ambayo amekosea...

Hakukuwa na watu wanaoitwa wayahudi miaka ya 8400 BC.. na Pharaoh Khufu sio mwanzilishi wa dola ya Misri..
 
mmmmh somalia kwa kwelii mmmh siendi hata bureeeeeh, ila kitu ethiopia labda,, maana juzi kati nimekutana na mdada wa kiethiopia aiseeeeeeh, now naona nina dalili za 'ethiopian girl's disease' mbaya zaidi kwa maongezi yake matamu na kakifua flani hiv kama kavunja ungo jana hata contact sikukumbuka, naombeni mwenye rafiki aliyepo ethiopia aniunganishe nae nataka kufika huko
 
SOMALIA NA HISTORIA YAKE KUNTU

Na: Comred Mbwana Allyamtu.

Somalia ni moja ya nchi inayopatikana katika bara la Afrika. Katika bara la Afrika Somalia inapatikana upande wa kaskazini-mashariki mwa bara la Afrika. Nchi ya Somalia inapakana na Kenya kwa upande wa kusini-magharibi, upande wa magharibi inapakana na Ethiopia, upande wa mashariki inapakana na bahari ya Hindi, upande wa kaskazini-mgharibi inapakana nchi ya Djibouti na upande wa kaskazini inapakana na ghuba ya Adeni.

Mji mkuu wa Somalia ni Mogadishu. Nchi ya Somalia ina ukubwa wa maili za mraba 246,200 sawa na kilomita za mraba 637,658. Lugha rasmi katika nchi hii ni lugha ya Kisomalia ambayo ina lahaja zake zinazojitofautisha kimazingira.

Kuna kisomali kinachoongelewa magharibi na kuna kisomali kinachoonglewa mashariki. Kihistoria lugha ya kisomali haikuwa kwenye maandishi mpaka ilipofikia ya 1973, ndipo lugha hii ilianza kuandikwa. Ikiwa na maana kuwa kabla ya miaka hiyo lugha hiyo haikuwa na hati zake kama alama kwenye lugha hiyo. Kwa upande mwingine lugha ya kiarabu kinaongelewa sana hasa kwenye suala zima la dini ya kiislamu. Wakati huohuo lugha kama Kiswahili na kiingereza kinaongelewa kwa wale wachache wanajua, hasa wale wanopakana sana na Wakenya.


*HISTORIA YAKE YA MWANZO*


Somalia ni taifa yenye makabila ( ukoo) makubwa matatu na makabila hayo utambulika kama koo. Ambayo ni
1- Olumo.
2- Policano.
3- Polusa.

Historia ya koo hizi zimekuwa kwa maerefu ya miaka toka zama za mwanzo (6000 BC) pamoja na hiyo jamii ya asili ya Somalia ni Olumo( Mafarasha wa kiyahudi) waliofika Somalia miaka ya 8400 BCE na kuweka makazi yake hapo. Huku Koo ya Policano ni jamii ya NILOTIC (wa nailote wa mto Naili) waliotoka Misiri kwenye jamii ya wanubi na wameanza kuishi aridhi ya Somalia miaka ya 3700 BCE baada ya Dola ya kwanza kuundwa Misiri (Egypt) chini ya Pharao KHUFU. Hata vivyo Pia koo ya Polusa ni koo iliyofika somalia miaka ya 903 AD kutoke bala Arabu na hii koo ndio iliokuja na dini ya uislam ulioenea Somalia sasa karibu 98% ya wasomali wote ni waislam.( Rejea katika makala ya andiko langu no 0014/7 la tarehe 16/6/2016 lililohusu Dola kuu ya Mrima (Kilwa) barani Afrika karne 10 ) katika makala hile nilielezea kinagha ubaga namna koo hiyo ya Polisa ilivyo fika Somalia na kuwa sahemu ya makabila ya Somalia.

Lakini pia Historia kwa upande wa dini ipo hivi, kabla ya miaka ya 600.AD wasomalia walipata kuabudu dini zao za kijadi na kipindi cha Ukristo ulipoingia barani Afrika kupitia Misri na Ethiopia. Lakini kwenye miaka ya 600, Wasomalia walianza kuwa Waislamu na mpaka kufikia miaka ya 1100, karibia wasomalia wote walikuwa waislamu. Na kwa sasa ni nchi ambayo watu wake ni Waislamu(Wasuni).

Asili ya neno Somalia ni Wasomalia wenyewe, kutoka katika ukoo uliofahamika kama Samalo au samaal (sehemu ya ukoo wa Olumo) Na mpaka wanaakiolojia na antropolojia(wakitumia maaandiko ya Wagiriki na Waroma) waliwatambua watu hao kama Wasomalia na nchi yao ni Somalia.

*UKOLONI KATIKA SOMALIA*

SOMALIA kama zilivyo kuwa mataifa mengine Afrika ilipata kutawaliwa na mataifa ya kibeberu katika Somalia ukoloni ulikuwa wa katika pande mbili yani Somalia ya kaskazini ilitawaliwa na Uingereza na Somalia ya kusini ilikuwa chini ya Italy mpaka mwaka 1960 zilipoungana pamoja baada ya vuguvugu la ushindi wa vita ya ukombizo. Hata hivyo Somalia ya kusini baada ya vita ya pili ya DUNIA (WW II) ilipewa Uingereza chini ya umoja wa mataifa chini ya uangalizi kutokana na kile kilicho itwa " kama fidia ya kushindwa vita kwa waluoshindwa"

Ukoloni Somalia uligawanyika katika aina mabalimbali kutokana na mataifa mawili tofauti kuikali kiutawala, na hii ndio sababu ilioifanaya Somalia kukosa maandishi ya lugha yake mpaka mwaka 1973 maandishi ya lugha ya kisomali yalipo anza kutumika rasm.
1990 dikteta Siad Barre alipinduliwa halafu Mogadishu pamoja na nchi yote iliingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe. Wanajeshi wa Marekani walijaribu mwaka 1993 kurudisha hali ya usalama kwa niaba ya Umoja wa Mataifa lakini walikuta upinzani mkali kutoka kwa vikundi vya wanamgambo Wasomalia. Baada ya kupoteza askari Marekani iliondoka tena.

Hali ya vita imeendelea

*VUGUVUGU YA UKOMBOZI NCHINI SOMALIA*

vuguvugu hili lilianza mara tu baada ya vita ya pili ya dunia na hii ilitokana na sababu nyingi tu lakin kwa uchache ni kama hizii zifuatazo...

1- maasikali walioludi Somalia kutoka vitani huko Burma, India na wale walio kuwa Ethiopia kuisaidia Italy dhidi ya Ethiopia katika kile kilichojulikana "ushindi wa mfalme wa Italy Victor Emmanuel" kuanzia mwaka 1936

2- mivutano kati ya Uingereza na Italy wakati wa vita ya pili ya dunia kulitowa mianya ya ukombozi katika mataifa ya ukanda wa pembe ya Afrika.

3- Hamasa ya ushindi kutoka Ethiopia chini ya Haile Selasie mwaka 1941 kuliwapa moyo wa kuamini kumbe hata wao wangeweza kushinda wakoloni kama mwenzao Ethiopia alivyo shinda "vita ya uvamizi wa Ethiopia dhidi ya Italy".

4- Msukumo wa dhana ya kisosholist kutoka Muungano wa Kisovieti ambao ulimsapoti pakubwa chama cha Somali socialist People (SSP) cha Aden Abdullah Osman.

5- kuongezeka kwa vuguvugu la ukombozi la waarabu ( Arabu uprising) lilokuwa likiongozwa na Abdul Nasir Gamal mwanzon mwa miaka ya 1948-1958.

Pamoja na sababu zingine ambazo sijazitaja hapo zilichangia pakubwa chama cha SSP cha Aden Osman kuwa na nguvu na hii ilitokana na kiongozi mmoja wa SSP kuongoza vita ya ukombozi ambayo ulikuwa na changamoto nyingi za kikabila na kidini katika mapambano ya ukombozi yaliongozwa na Aden Osman kwa karibu miaka 10 toka mwaka 1949 mpaka mwaka 1959. Hata hivyo ilipo fika mwaka 1952 chama cha SSP kilibadilishwa jina na kuwa SYL (Somali Youth League) na Aden Osman kuchaguliwa kuwa katibu mkuu (general secretal) wa chama cha SYL na ilipofika mwaka 1956 Aden Osman alikuwa ameshakuwa na umaarufu mkubwa baada ya kushinfa uchaguzi wa gavana wa mji wa Mogadishu karibu mara nne (4) lakin Uingereza hawakumpa ushindi kitu kilicho chochea maasi na vurugu karibu nchi nzima ilipo fika mwaka 1957 chama cha SYL kiliamua kubadili mbinu za mapambano ndipo Aden Abdullah Osman Darr alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha SYL na kongeza vuguvugu la machafuko nchi nzima.

mwingereza ilimbidi alikubali matokeo baada ya kuongezeka kwa machafuko waliamua kuipa uhuru Somalia kwa kuitisha uchaguzi ndipo chama cha SYL kikaongoza dhidi ya chama cha SN (Somalia natinalism) kilicho kuwa kinaongozwa na Abdrashid All Sharmaker katika balaza la kutunga sheria kwa zaidi ya kura 87 dhidi ya 49 ya SN.
Na baadae alifanikiwa kushinda na kushawishi Somalia mbili kuungana na kufanikiwa kuunganisha pande hizo mbili na kuwa nchi moja yenye nguvu. Na kisha Somalia kupata uhuru wake mwaka 1960 chini ya chama cha SYL chini ya Raisi wa kwanza Aden Abdullah Osman Darr.

*SIASA YA SOMALIA BAADA YA UHURU*

Mara baada ya uhuru vyama vyote viwili yana SYL na SN viliungana baada ya kuungana kwa Somalia zote mbili na Abdrashid all Sharmaker kuwa makamu wa kwanza wa Rais chini ya serekari ya Aden Osman Darr. Somalia mala baada ya uhuru iliamua kufuata siasa za kijamaa na kuwa nchi ya kwanza Afrika kutangaza kuwa na mfumo wa kijamaa (Socialism) uliokuwa ukipigiwa chipuo na ile iliokuwa Dola na himaya ya Kisovieti (Urusi). Hali iliopelekea serekari ya ya Somalia kutoungwa mkono na mataifa ya magharibi (ulaya) pamoja na yote 1965 Somalia ilifanaya mabadiliko ya katiba yake na kuifanya kuwa taifa ya kidemokrasia yenye mlengo wa Kisovieti (Soviet brock pact nation) na kupelekea kufanyika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia Afrika mwaka 1967.
--UCHAGUZI WA KIDEMOKRASIA 1967.

uchaguzi wa mwaka 1967 ndio uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia kufanyika afrika katika uchaguzi huo Aden Abdullah Osman Darr alishidwa na mpinzani wake Abdrashid alli Sharmaker na Aden Osman Darr alikubali matokeo na kuwa Rais wa kwanza kuachia ngazi ya urais kwa njia ya amani Afrika. Pamoja na Aden Abdullah Osman Darr kuheshimu demokrasia amebaki kuwa na heshima kubwa afrika na duniani kote kwa kupewa heshima ya Baba wa demokrasia Afrika ( the father of African democracy) mpaka kifo chake kinamkuta nchini Kenya mwaka 2009 akiwa na miaka 91.

Serekali ya Abdrashid alli Sharmaker ilipinduriwa na kikundi cha waasi wa jeshi na yeye kuuwawa na mrinzi wake mwaka 1969. Ilikuwa tarehe 15/10/1969 asubuhu pale askari mrinzi wake alipo mfyatulia risasi na kumu-ua… baada ya kifo chake kuliibuka machafuko ya jeshi yaliopelekea wasomali wengi kukimbilia nje ya nchi kama wakimbizi hata hivyo Shekh Mukhatar Muhamed Hussen Alichaguliwa kushika nafasi ya uraisi lakina baada ya siku sita (6) alipinduliwa na aliekuwa mkuu wa majeshi Meja jenerali Mohamedi Said Barre alieitawala Somalia mpaka mwaka 1991 alipo kuja kupinduriwa na balaza la mapinduzi lilokuwa likiongozwa na Alli Mahd Muhammad.

Mara baada ya mapinduzi hali ya siasa Somalia imekuwa tete toka kipindi hicho mpaka sasa. Marekani ilijalibu kupeleka jeshi kujalibu kutuliza hali ya nchi mwaka 1997 lakini walikwama na kuludisha jeshi lao marekani kwa kushindwa.


VITA YA NDANI NA KUIBUKA KWA AL- SHABAB.


Baada ya mapinduzi ya mwaka 1991 selekari ya Alli mohamedi ilianza kupata migogoro ya ndani toka kwenye koo za ndani na kupelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe na kupelekea jimbo la Putland na Somaliland kujitenga na kujitangazia uhuru wao ambao aujakubaliwa kimataifa hata hivyo hali ya usalama ilizidi kuzolota na kupelekea kuibuka kwa kundi la kidini la Al-shabab.
Kundi la Al-shabab, kundi hili lilianza mwanzoni mwa mwaka 2000 na kuanza kupata nguvu mwaka 2004 lilipo kuja na misimamo ya "Jihadi Sarafu" juu ya kile kilichoitwa " Mahakama za dola la kiislam" ( Islam Court Union) vuguvugu hili liliongozwa na Ahmad Godan na Ayman Al-Zawahili 2006-2014 huku makao makuu ikiwa Kismayo. Mwaka 2006 jeshi la Al-shabab lilifanikiwa kuiteka nchi nzima ya Somalia na kuwa chini ya jeshi la utawala wa Al-shabab linalokadiliwa kuwa lilikuwa linafika askari 7000-9000. Mpaka pale lilipokuja kuondolewa mwaka 2009 na jeshi la AMISOM pamoja na uvamizi wa Kenya.

DIPROMASIA YA SOMALIA TOKA MWAKA 1960-2016

Somalia imekuwa na migogoro mara kwa mara toka uhuru wake mfano tu ni....

1- Mnamo miaka ya 1960, kulikuwa na mgogoro kati ya Kenya na Somalia. Kihistoria nchi ya Somalia kabla ya miaka ya 1960, ilikuwa imegawanyika yaani Somalia ya kusini na Somalia ya kaskazini. Na kwenye miaka 1961, kiongozi mmoja wa vita alifanikiwa kuunganisha pande hizo mbili na nchi moja yenye nguvu,

Pili pia
2-hawakuishia hapo, walitamani kufanya upanuzi kwa kutaka kuchukua maeneo kutoka Kenya na Ethiopia na hapo ndipo mgogoro ulipoanza. Na mwisho wa siku mgogoro uliisha kwani Ethiopia na Kenya kwenye miaka ya 1961/1962 waliunda umoja wa kijeshi kwa ajili ya kujilinda.
3- uvamizi wa kenya juu ya kile kilichoitwa vita ya Somalia na kikosi cha Al-shabab.
4- mgogoro wa Somalia dhidi ya Somaliland na Putland kimataifa.


UFAHARI WA SOMALIA KIMATAIFA.


Ushahidi kutoka kwa Wagiriki unasema kuwa watu wa kanza kupata kuishi Somalia ni wasomalia ambao wanatoka katika kundi la familia lugha ya Kushitic Wa Mashariki yani Waolumo na Walipata kufika hapo kabla ya milenia ya kwanza na jamii ya policano walifika hapo tokea Egypt tangu milenia ya kwanza wakimaanisha kuanzia mwaka 1-1000. Kwa kipindi chote hiko Wasomalia waliishi na ufalme wao ambao ulipata kuwapo maeneo ya Mogadishi. Miongoni mwa falme uliokuwepo ni Bazrangid kabla ya miaka ya 600.

Nakuanzia miaka ya 600, Waarabu walivamia ardhi ya Wasomalia na kusambaza Uislamu. Na kufikia miaka ya 1300, Waethiopia walijaribu kuvamia Somalia na kutokana na uwepo wa Waarabu ilishindikana. Kipindi cha ukoloni karne ya 19, Somalia ilikuwa imegawanyika, zipo sehemu zilizokuwa chini ya Italia, zipo sehemu zilikuwa chini ya Sultani. Na mpaka kufikia miaka 1940, yapo maeneo yalikuwa chi ya Sultani na mengine yalikuwa yakisimamiwa na Mwingereza. Na miaka ya 1960 kukawa na mchakato wa kuunganisha nchi hiyo. Raisi wa kwanza alikuwa Aden Abdullah Osman Daar(1908-2007). Na raisi wa sasa ni Raisi wa nane (8) ambaye ni Hassan Sheikh Mohamoud.

"Mungu bariki Afrika, mungu wabariki waafrika na fikra zao"

Daar Olya Karibuni Somalia, Somalia HAKUNA MTATA.

Ndimi
Comred Mbwana Allyamtu.

+255765026057
+255679555526
Mbwanaallyamtu990@gmail. ComView attachment 362268View attachment 362269
Hii historia ipo shallow sana. Hapo kuna figure nyingi huja zitaja na matukio kibao umeyapotezea. Kwamfano ni kitu gani kilisababisha Sied Barre kupinduliwa!? Vipi kuhusu rule ya koo katika maisha ya wasomali!? Na vipi pia kuhusu Vita ya Koo na pia kuhusu Mbabe wa Kivita MOHAMED FARRH IDEED!? Vipi kuhusu kabila la la wabantu lililo kuwepo Somalia na sasa wamehamia Handeni na wana zungumza lugha moja na wenyeji wa Handeni?
 
Back
Top Bottom