Hii la mahakama ya kadhi limekaaje?

Status
Not open for further replies.
Tulishaambiwa serikali haina dini hakuna cha kushangaa katiba kutozungumziwa mahakama ya kadhi kwenye nchi yenye mchanganyiko wa dini kama TZ
 
Mkuu Mkirua Hiyo ndio Kete aliyotumia Kikwete kupata kura zetu huku misikitini badala ya kutuhamasisha tujenge shule wanatudanganyia mahakama za kadhi wenzetu wakristo mnasonga mbele tuu
Wewe ni Mohamed Hussein Daima " Mmachinga" Yule striker bora kabisa wa Yanga aliyepata kutokea katika nchi hii katika kipindi cha mwaka 1995-2000?
 
  • Thanks
Reactions: mij
....kaka na dada zangu ktk imani ya kiislamu..! tumeshagawanyika mno! wanasiasa na viongozi wetu wameshatugawa mno! ukikaza jicho "usawa wa kati, mbele", utaona kuzungumzia mahakama ya kadhi ktk katiba ni fimbo ya kisiasa inayotumiwa na wanasiasa (naam!) na vibaraka wao waliojivika uimamu, na usheikh kuchapiana kwa sababu za kisiasa zaidi!...la msingi hapa ni moja tu!...TUNAIHITAJI KWA DHATI KABISA MAHAKAMA YA KADHI?...kama jibu ni: "Naam..tunaihitaji", basi na tuiunde wenyewe! hatuwezi shindwa!..lkn (1:LAKINI 2:LAKINI 3:LAKINI)...sisi wenyewe tunayoihitaji, tuwe na imani thabit ktk "emaan", na insha allah, ktk mahakama, na mahakimu wake na hukumu, na maamuzi yatakazokuwa yakitolewa katika mahakama hizo...kisha tuone...yule atakaedharahu......na sisi (KATIKA UMOJA WETU WA KIIMANI KTK HILI) tutamfanya mfano "KIMAKWELIKWELI"....
 
Hili la mahakama ya kadhi limekaaje mbona tulihamasishana sana lakini kwenye rasimu ya katiba limekwepwa


Ishu ni nani wa kugharamikia mahakama ya kadhi!
Mahakama ya kadhi kuwepo kwenye katiba siyo ishu sana. Tunaweza kuiendesha kwenye misikiti yetu

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
hili la mahakama ya ardhi mlilipigia kelele na nani! mlishambiwa ruksa kulianzisha but lisitegemee mkono wa serikali, coz ni mambo ya kiislamu hayo!

mkuu mbona mahakama ya ardhi ipo toka kitambo hapa nchi? au umechanganya pilau na mlenda.
 
...wanasiasa na masheikh na maimamu wanaoshupalia kuifanya mahakama ya kadhi kuwa jambo la kuamuliwa na katiba, wote wako katika siasa ileile!(kuwagandamiza waislamu)....! waislam tunaihitaji mahakama ya kadhi! uwezo wa kuiunda tunao!na uwezo wa kuigharamia kulingana na uwezo wetu tunao! uwezo wa kulinda utekelezaji wa hukumu na maamuzi ya mahakama zetu hizo tunao ktk kiwango cha kuwatisha mpaka maadaui wa imani yetu!!!!...tunasubiri nini sisi waislam wa eneo hili la mama afrika? serikali? au msaada wa waarabu? hatuwezi kufanya kama kaka zetu wa "nation of islam", katika amerika, au PAGAD ktk cape town walivyofanya ?
 
Suala la mahakama ya Kadhi ni suala jepesi kama Wahusika wenyewe wakiwa na nia ya dhati na mahakama hii.Kwanza idea ni kwamba mahakama itakuwa inashughulikia usuluhishi, upatanishi, Mirathi, na ndoa .Sasa baada ya kuruhusiwa kwamba waislam waanzishe mahakama yao katika misingi yao wenyewe nje ya mfumo wa serikali mimi nadhani hii ingekuwa ni golden chance. Hii ilikuwa ni bahati ya kipekee kwa kuwa kwa kipindi chote lawama zimekuwa zikijitokeza kwamba bakwata imeundwa na serikali na sasa badala ya kuwasaidia waislam inawadumaza.(kwa kawaida anayelipa mishahara ndio huwapangia wafanyakazi cha kufanya).Sasa mimi naona suala hapa ni kuanzisha mahakama kwenye mifumo ya ndani ya dini yenyewe na serikali isihusike kwa kuwa serikali ni ya kisecular inayohudumia watu wengi wa aina tofauti tofauti. Mimi sidhani kama waislam wakiji organize wakafungua mahakama yao watu wakiwa na migogoro katika ndoa yao wakafika pale wakasuluhishwa wakaendelea na maisha, mimi sioni kama kutakuwa na tabu yeyote.Kadhalika na madhebu mengine yanaweza kufanya hivyo.Hebu tuiacheni serikali iwe neutral kwenye masuala ya kujihusisha na dini.Kutaka serikali kuingilia kwa namna yeyote ile kwenye masuala ya dini za watu, ni kutaka migogoro isiyo na sababu.
 
Tatizo mnaomba mahakama ya kadhi bila ya imani, ndio maana mnaikosa, ongezeni imani kidogo na muswali kwa bidii mungu atawasikia na kuwapa mahakama hayo
 
Si mlishaambiwa kwamba mahakama ya kadhi RUKSA lakini undeni wenyewe nje ya mfumo wa serikali.

Serikali iliwaundia BAKWATA hadi leo mnalalamika, sasa tena mnataka SERIKALI iwaundie tena MAHAKAMA YA KADHI, hivi nyinyi watu mnafahamu mnachokitaka?!
Mkuu ngoja nitafute kitufe cha LIKE..Mgogoro unafukuta kwa sasa kati ya serekali na baadhi ya waislam ni kuhusu Bakwata,sasa inakuaje watake serekali iwaundie mahakama ya kadhi wakati Wanataka serekali ijitoe Bakwata..
 
Si mlishaambiwa kwamba mahakama ya kadhi RUKSA lakini undeni wenyewe nje ya mfumo wa serikali.

Serikali iliwaundia BAKWATA hadi leo mnalalamika, sasa tena mnataka SERIKALI iwaundie tena MAHAKAMA YA KADHI, hivi nyinyi watu mnafahamu mnachokitaka?!

hawa ni viumbe wa ajabu sana!
 
Hili la mahakama ya kadhi limekaaje mbona tulihamasishana sana lakini kwenye rasimu ya katiba limekwepwa


Mnalalamika kitu gani, si tayari Kadhi alikwisha teuliwa, inamaana tokea ateuliwe bado hajapata ofisi? Hata mmeshindwa kujichangisha mkajenja Mahakama, pia Kikwete alishawambia kuwa Serkali haitajihusisha na Mahakama ya Kadhi. Jichangishe changishe muendeshe wenyewe Mahakama yenu.
 
Huo ndiyo uhuni wa ccm,kwenye kampeniya urais walituahidi litashughulikiwa lakini wametuona sisi kama watu wasio na akili,wametufanya ngazi ya kufanikiwa malengo yao ya kisiasa.
Hapo sasa inabidi tubadilike habari ya kutumiwa kama ngazi na wanasiasa kwa malengo ya vyama vyao sasa iwe mwisho.

na nyie mmezidi, nchi ni moja mahakama ya kadhi undeni huko misikitini kwenu!!
 
Waislamu walishiriki katika kutoa maoni kuhusu kurejeshwa Mahakama ya Kadhi lakini hakuna aliyetegemea kuwa Warioba atatupa Mahakama ya Kadhi!

Ninachotaka kusema ni kuwa hakuna jipya! ilitegemewa na Waislamu kuwa suala la Mahakama ya Kadhi litatupwa, lakini kama wasemavyo wazungu There is always plan B.

tangia lini makafiri wawaundieni mahakama ya kadhi? NYERERE aliwaoneeni huruma akawaunganisha na bakwata lakini hakuna shukrani.
 
Katika nchi isiyotawaliwa na dini Kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi
katika mambo ya imani ya dini aipendayo na anao uhuru pia wa kubadilisha dini,
imani yake au kutokuwa na imani na dini.
Serikali ipo katika kuwasimamia watu na kuwaelekeza katika njia sahihi jinsi ya kuishi bila migogoro na kufikia malengo mbalimbali ya maisha. Kutokana na serikali kutokuwa na dini haipo katika kupiga kam,peni mambo ya dini.Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ili mradi asivunje sheria za nchi.
Kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii ya watanzania na chi kwa ujumla serikali itasimamia kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria za nchi yaani katiba jinsi ya kuenenda.
 
Huo ndiyo uhuni wa ccm,kwenye kampeniya urais walituahidi litashughulikiwa lakini wametuona sisi kama watu wasio na akili,wametufanya ngazi ya kufanikiwa malengo yao ya kisiasa.
Hapo sasa inabidi tubadilike habari ya kutumiwa kama ngazi na wanasiasa kwa malengo ya vyama vyao sasa iwe mwisho.
...kaka wanasiasa pia wana mawakala wao miongoni mwetu ambao ni wengi katika maimamu na masheikh wetu...! lazima tuwaambie mbele ya nyuso zao kwamba "sisi waislam tunataka siasa ya kiislamu, na si uislam wa kisiasa"...!....ktk nchi yetu, waislam kwa umoja wetu, hatutakuwa na matatizo na serikali wala wenzetu wasiokuw waislam kama tu, tutasimama katika siasa ya kiislam, na kuachana na uislam wa kisiasa ambao tunaushuhudia miongoni mwa "wanasiasa na vibaraka wao ktk misiki yetu".....!
 
...wanasiasa na masheikh na maimamu wanaoshupalia kuifanya mahakama ya kadhi kuwa jambo la kuamuliwa na katiba, wote wako katika siasa ileile!(kuwagandamiza waislamu)....! Waislam tunaihitaji mahakama ya kadhi! Uwezo wa kuiunda tunao!na uwezo wa kuigharamia kulingana na uwezo wetu tunao! Uwezo wa kulinda utekelezaji wa hukumu na maamuzi ya mahakama zetu hizo tunao ktk kiwango cha kuwatisha mpaka maadaui wa imani yetu!!!!...tunasubiri nini sisi waislam wa eneo hili la mama afrika? Serikali? Au msaada wa waarabu? Hatuwezi kufanya kama kaka zetu wa "nation of islam", katika amerika, au pagad ktk cape town walivyofanya ?


hivi waislam mna maadui wa imani yenu? Hilo nalo jipya.
 
Si mlishaambiwa kwamba mahakama ya kadhi RUKSA lakini undeni wenyewe nje ya mfumo wa serikali.

Serikali iliwaundia BAKWATA hadi leo mnalalamika, sasa tena mnataka SERIKALI iwaundie tena MAHAKAMA YA KADHI, hivi nyinyi watu mnafahamu mnachokitaka?!

binafsi sidhani kama wanajua,na sijui wanambwela nini kufanya yao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom