HII IMEZIDI SASA.... kivukoni

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,603
29,748
Tangu mwanzo wa mwezi huu serikali imebadili utaratibu wa usimamizi wa kuruhusu abiria kuingia kwenye kivuko pale ferry. utaratibu huu wanasema kuwa wanakusanya takwimu zao fulani. Sasa angalia walivyofanya:-

  1. Abiria wooote wanashurutishwa kupitia lango moja kuingia ktk kivuko, tena wanalazimishwa kurundikwa kwenye banda la kusubiria ambalo halina uwezo wa kuacomodate watu wengi ikichukuliwa kuna maradi ya kuambukiza kwa hewa au ngozi. Hata akina mama, watoto, wagonjwa wanarundikwa humo kwa usimamizi mkali wa wanajeshi na polisi (siyo walinzi waliokodiwa na wizara)
  2. SERIKALI inatumia JWT (Tena Military Police) kusimama mlangoni kukagua tiketi. Hii ni unyanyasaji mwingine na udhalilishaji wa vyombo vyetu vya ULINZI. kazi hii ingefaa sana mgambo ambao ndio wako kwenye levo ya kusimamia bylaws na shughuli ndogondogo za manispaa.
  3. WALINZI wa vivuko hawaheshimu au hawajafundwa kuhusu haki za binadamu kwani wanajua wazi kwamba baada ya magari kuingia kwenye kivuko wanapaswa kuruhusu abiria wapande ndipo baskeli na pikipiki, lakini wao huruhusu pikipiki na baiskeli kuziba milango ya kivuko kisha ndipo hufungulia abiria kutoka VIFUNGONI wakajiju na matahira waendesha vyombo vya matairi mawili.
  4. Ndani ya pantoni sheria na utaratibu haufatiliwi kabisa kwani hivyo viboya vya kujiokoa vimerundikwa mahala pamoja na vimepigwa KUFULI kana kwamba ikitokea dharura kuna crew mwenye roho ya malaika atavifungua na kuwagawia abiria wasiojua namna ya kuvitumia. Wehu wa wizara ni kwamba hata hizo life-jackets hazina user manual. au kama ilivyo kwenye vyombo vya usafiri hakuna maelekezo kutoka hata kwa rubani on how to use them.
  5. Muda wa kivuko kushusha na kupakia abiria unazidi dakika hamsini ukijumlisha na interval ya route moja yaani dakika sita za kusafiri.
  6. upande wa kigamboni hao wanajeshi, polisi na walinzi wanajaza magari kwenye open yard ya gati na kuacha nafasi FIIIINYU ya kupita msongamano wa abiria na magari yanayoshuka kwenye kivuko. Kuna siku itatokea ajali ndipo watajua kwamba physics haikuzingatiwa na kuanza kulaumiana.
  7. TUNAOMBA wizara iwaeleze wakazi wa kigamboni kwa nini walipe kuingia ktk pantoni ilihali PANTONI ni sehemu ya barabara? ni haki kwa vyombo vya usafiri kulipia lakini si watu ambao wengine wanakosa hata hizo shs mia (ambayo wizara imepanga kuongeza baada ya uchaguzi).
Wadau mnaofahamu na kutumia kivuko cha kigamboni mnayo mnayoyafahamu ktk hili?
Jamani natoa hoja ifike kunakohusika ili ufafanuzi na marekebisho yafanyike kungali mwachweo
 
Ndugu watu wametajirika sn kwa kuuza tikets mara mbili au tatu, ss nadhani wamestuka lkn too late
 
Bahati mbaya hao majeshi hawajali wazee wala wasiojiweza.
Kwani wanashindwa kutumia teknolojia kufanya tahmini? mbona serikali yetu hii analogy sana?
 
Back
Top Bottom