Hii imekaaje?

Hivi kwa ndg zetu waislam mfungo una maana gani nyingine tofauti na kujinyima na toba?
Nasema hivi kwa vile nimeshangazwa na tukio la leo hotelini pale Iringa, tuliposhuka kwenye basi kwajili ya chakula na kuchimba dawa.
Nilishangaa kusikia tangazo kupitia vipaza sauti vya pale hotelini likisisitiza na kutoa onyo kwa vijana wanaouza maziwa mtindi/yogurt za kampuni ya Asas. Tangazo lilisisitiza watakaokamatwa wakiuza yogurt kwa abiria ktk kipindi hiki cha ramadhan wasije kulaumu...nilishangaa sana!
Ikumbukwe, watengenezaji wa maziwa hayo ni matajiri wakiarabu, ASAS Diary Group wenye 'base' yao hapo Iringa.

Sasa nikajiuliza na naendelea kujiuliza, ina maana wateja wenye haki ya kutumia hayo maziwa ni Waislam peke yao? Je, wateja wa imani tofauti na uislam hawaruhusiwi pia kutumia maziwa hayo ktk kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhan?

Sheria ya dini inasemaje kuhusu wachuuzi wadogo wanaoishi kwa kutegemea biashara hiyo ya kuuza hayo maziwa? Wanapewa posho ya kujikimu na kampuni kupisha mfungo?

Vipi kuhusu wagonjwa ambao wanatakiwa kunywa au kuendelea kula kwasababu za kitababu? Ni dhambi pia kuwauzia maziwa?

Kwa kweli nimewaza mengi na kujikuta nikihitimisha ukweli wa msemo usemao, Religion is the opium of mind! It might be a crude conclusion, but it's what it is!
Dini ya Uislam imejawa na chuki na unafiki tupu, haifai kwa jamii
 
Kwa sababu umeuliza kuhusu sheria ya dini inasemaje kwenye jambo hilo ngoja tukupe majibu na wengine wajifunze hapa...

Mwezi wa ramadhani ni lazima kufunga kwa kila aliye mwislamu isipokuwa watu hawa tu
A.mtoto mdogo (aliye chini ya miaka 7)
B.majnuni/punguani/chizi/taahira/kichaa/punguani/mwendawazimu
C.mgonjwa/mzee kikongwe/mjamzito/aliye kwenye hedhi/anayenyonyesha (ambaye hali yake inafanya ashindwe kufunga)
D.msafiri (aliyeko safarini)


Hivyo basi Mtu mwingine yeyote asiye na kimoja katika hivyo haruhusiwi kupewa huduma ya chakula mchana wa mwezi wa ramadhani kwa hiyo kama ulisikia tangazo hilo uelewe kwamba hakukusudiwa Wewe wala uliyepanda naye basi

Kinachotokea ni kwamba sheria hainitumi na wala siyo sharti kuwauliza wateja kwamba wamefunga au hawajafunga, au kutaka kujua wana udhuru wa kisheria au laa. Vijana nao ndiyo hivyo wanachotaka ni faida tu hawaangalii masharti waliyowekewa hivyo mtu mwingine kwa kuhofia mkanganyiko anaamua kujizuia kabisa kufanya biashara ya vyakula na vinywaji mchana wa ramadhani.

Nakumbuka jamaa mmoja aliwaambia vijana gari yake wasibebe pombe wakawa wanabeba akawashtukia akawafukuza akaleta wengine mambo ni yaleyale akaihamisha na gari yenyewe (yote ni namna ya kuepuka shubuhaat au mikanganyiko)

Ni ngumu kujua kama mtu ananunua kitu (chakula) kwa ajili ya mtoto au mgonjwa, au ananunua kwa ajili ya kula baada ya kuingia magharibi. Vilevile ni ngumu kutofautisha wasafiri na wasio wasafiri miongoni mwa wateja wako.

Hatahivyo uislamu haulazimishi asiye muislamu kufunga biashara yake ya vyakula kwa hiyo kuna watu lazima wataponea njaa huko (na hii ndiyo nature ya uislamu)
Jambo moja la kuzingatia ni kwamba kutokuwa mwislamu hakukupi uhalali wa kuuziwa chakula au vinywaji na mwislamu mchana wa ramadhani

Najua umepata maswali mengi sana baada ya kusoma hivi kwa mfano utajiuliza


Majibu ya maswali hayo ni kwamba MAMBO YAO WAACHIE WENYEWE . Waislamu wenyewe wanajua kwamba"ukiacha jambo kwa ajili ya mola basi utapewa lililo bora kabisa kuzidi hilo uliloliacha" kinachotushinda ni imani tu!

Kuhusu wewe kufika mji wa waislamu tupu na ukakosa hata mgahawa wa kula mwezi huu wa ramadhani, jambo hili ni hypothetical halafu mimi siwezi kuliongelea ila kuna wataalamu wana uwezo mkubwa kunizidi watalifafanua inshaallaah!
Asante kwa ufafanuzi mzuri. Nilichoelewa ni kuwa mambo ya imani hayapaswi kuchanganywa na logic.
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri. Nilichoelewa ni kuwa mambo ya imani hayapaswi kuchanganywa na logic.
Yeah, kwa mfano imani ya kiislamu inakataza kamari na riba lakini ukiangalia kwa logic riba inatajirisha watu!
 
Mimi mwenyewe nimeshangaa juzi eti naingia mgahawa wa Bahkresa pale kariakoo naomba niuziwe maji ninywe dawa zangu za Typhoid ninazo kabsa mkononi eti nanyimwa huduma na kuambiwa maji hayauzwi yan hakuna chochote kiuzwacho licha ya kuwaonesha dawa sasa sijui hata hyo toba wenzetu wanayoifanya mwezi huu wa Ramadhan pamoja ya kua na huruma kwa wagonjwa cjui ni ipi nlichoka Yan haya yamenikuta juzi Ijumaa
 
Back
Top Bottom