Hifadhi ya Ngorongoro ecology lazima izingatie UHAI na USTAWI wa BINADAMU juu ya viumbe wengine

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Assalamualaikum wana JF!

Naenda moja kwa moja kwenye mada yangu hapo juu:

Kwa mujibu wa taarifa toka Serikalini ongezeko la idadi ya binadamu (Wamaasai) na ujenzi wa makazi yao katika Hifadhi ya Ngorongoro linahatarisha ecologia ya hifadhi hiyo. Na kwamba uamuzi wa kupunguza idadi ya watu kwa kuwahamishia Handeni ndiyo njia pekee ya kuokoa ecosystem ya Ngorongoro.

Napenda kutofautiana kidogo na uamuzi huo wa Serikali kwasababu zifuatazo:

1. Lengo la kwanza na msingi wa sera za mazingira ni kulinda na kuboresha uhai wa binadamu hapa duniani. Mwanamazingira wa kweli hawezi kukiuka msingi huu wa sera au elimu ya mazingira.

Vitabu vitakatifu vinasema kwamba baada ya kuumba dunia, Mwenyezi Mungu alimuumba binadamu (Adam na Hawa) na kumkabidhi bustani ya Eden ili aimiliki na kuitumia kwa mahitaji yake.

Vitabu vitakatifu vinasema pia kwamba Mwenyezi Mungu aliwaumba binadamu (Adam na Hawa) ili wazaane na kuijaza dunia! (Ingawa hatujui nini kitatokea tukishaijaza dunia, vitabu havijasema).

2. Athari za ongezeko la idadi ya binadamu katika dunia ni pamoja na kupungua kwa ardhi na resources za kuendeleza uhai wa binadamu na uhai wa viumbe wengine.

Kwahiyo kama Serikali na wadau husika wanakubaliana kwamba Wamaasai ni sehemu ya ecosystem ya Ngorongoro na kwamba (kibinadamu), haiwezekani kuwaondoa wote katika makazi yao ya asili; mambo muhimu yafuatayo yalipaswa kuzingatiwa:

1. Kwasababu tangu huko nyuma hakukuwa na mipango endelevu au hatua sahihi kitaifa na locally, za kuiendeleza jamii ya Wamaasai bila kuathiri ecosystem ya Ngorongoro; matokeo yake ni kuibuka kwa divergent local and national interests kama tunavyoona leo!

Maana yake ni kwamba kitaifa kuna makundi kadhaa yenye mitizamo tofauti kuhusu Ngorongoro.

A. Kuna kundi linaloliona eneo lote la Ngorongoro kuwa ni 'Hifadhi ya Ngorongoro'; kwamba ni kivutio cha watalii. Kundi hili kwa upande mmoja linaonekana kuthamini utalii zaidi, labda kuliko uhalali wa makazi ya asili ya Wamaasai.

B. Kuna kundi jingine linaloiona Ngorongoro kama makazi ya asili ya Wamaasai na wanyama. Kundi hili kwa upande wao linaonekana kuthamini makazi ya asili ya Wamaasai, labda kuliko utalii.

C. Lakini vile vile kuna kundi la tatu ambalo linathamini utalii na makazi ya asili ya Wamaasai.

2. Idadi ya binadamu na wanyama katika Ngorongoro ecosystem lazima itaendelea kuongezeka kila mwaka hata kama baadhi yao watu au wanyama leo watahamishiwa Handeni au Unguja nk.

Mpaka sasa kinachosikika toka Serikalini ni mpango wa kuwahamisha baadhi ya wanadamu kutoka makazi yao ya asili ya Ngorongoro kwenda Handeni katika mazingira tofauti, ingawa wanajengewa nyumba mpya za "kisasa".

Kwa bahati mbaya inaonekana kwamba kuna kasoro kadhaa kuhusu mpango huu wa kuwahamisha baadhi ya Wamaasai kama ifuatavyo:

1. Kutokana na hoja mbalimbali za wakosoaji wa mradi/mpango huu hasa mitamdaoni; inaonekana kwamba mtizamo wa wadau muhimu (wawekezaji wa secta ya utalii na Serikali na imeegemea zaidi katika kundi A. hapa juu ambalo linathamini utalii zaidi labda kuliko uhalali wa makazi ya asili ya Wamaasai. Na hii ni kutokana na masuala kadhaa, kwamfano mtiririko wa taarifa kuhusu uchambuzi wa athari HASI za kimazingira na jinsi ya kuzipunguza, ushirikishwaji wa wadau na maamuzi hatua kwa hatua kabla ya kufikia utekelezaji wa uhamisho wa watu kutoka makazi yao ya asili kwenda makazi mapya.

Pengine Serikali ingeweka wazi taarifa za aina nilizotaja hapo juu, na ingeshirikisha kikamilifu jamii husika kufikia maamuzi kabla ya utekelezaji wa mradi hatua kwa hatua, baadhi ya malalamiko na vurugu zingeepukika.

Kwahiyo kwa vile mradi huu ulianza miaka kadha iliyopita nadhani awamu ya 4 kama sikosei, umma ungekuwa una taarifa kuhusu mambo muhimu yafuatayo:

* Ripoti kuhusu idadi za binadamu na wanyama katika Ngorongoro ecosystem, za sasa na vipindi kadhaa mbele.

* Ripoti ya uchambuzi wa athari HASI za kimazingira na jinsi ya kuzipunguza au kuzitatua.

* Ripoti za changamoto mbalimbali kwamfano makazi ya kudumu, huduma za jamii, miundombinu, uchumi nk.

*Gharama za utekelezaji na uendeshaji na vyanzo vya fedha.

Hayo ni baadhi ya masuala mengi yanayopaswa kuwekwa wazi kwa umma wa Watanzania katika kitu kinachoitwa "full disclosure" kuanzia mwanzo kabisa!

Pili, kama nilivyosema hapa juu msingi wa sera za Serikali na wadau katika miradi ya ecosystems lazima iwe kulinda uhai na kuboresha maisha ya binadamu, juu ya viumbe wengine.

Kwa lugha ya kimazingira "overriding interest" ya Serikali katika suala la ku-preserve ecosystem ya Ngorongoro lazima iwe kwanza kabisa, kulinda na kuboresha maisha ya binadamu katika makazi yao ya asili.

Miaka kadha iliyopita kuliibuka suala la 'Vyura wa Kihansi' ambao walisemekana kuwa hatarini kutoweka baada ya mradi wa hydropower kujengwa. Baadhi ya wanamazingira wetu walitaka kusimamisha mradi ili kulinda uhai wa viumbe hao!

Mwisho wa siku vyura hao walihamishiwa USA ili Watanzania wapate umeme.

Maana yake ni kwamba ikijatokea umma wa Watanzania hawana chakula, tutaaacha wafe njaa au tutaruhusu wale nyumbu, nyati na mbogo wa Ngorongoro?
 
Kuwahamisha wakazi wa Ngorongoro ni jambo sahihi katika ktunza asili ya hifadhi hiyo na kuboresha utalii ktk eneo hilo kwa vizazi vijavyo.

Serikali imeweka mpango mzuri sana wa kuwalinda wakaazi na mazingira.
ila tatizo kubwa lipo kwenye upotoshaji wa maksudi unao fanywa na watu wenye nia ovu dhidi ya Serikali.

Watu wenye nia ovu wanataka kuwaaminisha umma kuwa zoezi linalo fanywa na serikali ni la kibabe na lina vunja Haki za binaadamu!! kumbe sivyo ilivyo.

Naunga mkono zoezi linalo fanywa na Serikali kwa masilahi ya kizazi kijacho.
wakazi wa Ngorongoro waendelee kutii zoezi hili halali na waepuke upotoshwaji na wachochezi ambao hawana nia njema.
 
Kumbuka binadamu amepewa akili tofauti na wanyama. Binadamu atahama kijijini na kuhamia maghorofani mjini na ataishi maisha mazuri tu, lakini wanyama hawawezi. Ni lazima tutumie akili kuwalinda wanyama na sii kuwaangamiza. Ikibidi binadamu ahamishwe ili kutokuangamiza wanyama na uoto mwingine wa asili.
 
Assalamualaikum wana JF!

Naenda moja kwa moja kwenye mada yangu hapo juu:

Kwa mujibu wa taarifa toka Serikalini ongezeko la idadi ya binadamu (Wamaasai) na ujenzi wa makazi yao katika Hifadhi ya Ngorongoro linahatarisha ecologia ya hifadhi hiyo. Na kwamba uamuzi wa kupunguza idadi ya watu kwa kuwahamishia Handeni ndiyo njia pekee ya kuokoa ecosystem ya Ngorongoro.

Napenda kutofautiana kidogo na uamuzi huo wa Serikali kwasababu zifuatazo:

1. Lengo la kwanza na msingi wa sera za mazingira ni kulinda na kuboresha uhai wa binadamu hapa duniani. Mwanamazingira wa kweli hawezi kukiuka msingi huu wa sera au elimu ya mazingira.

Vitabu vitakatifu vinasema kwamba baada ya kuumba dunia, Mwenyezi Mungu alimuumba binadamu (Adam na Hawa) na kumkabidhi bustani ya Eden ili aimiliki na kuitumia kwa mahitaji yake.

Vitabu vitakatifu vinasema pia kwamba Mwenyezi Mungu aliwaumba binadamu (Adam na Hawa) ili wazaane na kuijaza dunia! (Ingawa hatujui nini kitatokea tukishaijaza dunia, vitabu havijasema).

2. Athari za ongezeko la idadi ya binadamu katika dunia ni pamoja na kupungua kwa ardhi na resources za kuendeleza uhai wa binadamu na uhai wa viumbe wengine.

Kwahiyo kama Serikali na wadau husika wanakubaliana kwamba Wamaasai ni sehemu ya ecosystem ya Ngorongoro na kwamba (kibinadamu), haiwezekani kuwaondoa wote katika makazi yao ya asili; mambo muhimu yafuatayo yalipaswa kuzingatiwa:

1. Kwasababu tangu huko nyuma hakukuwa na mipango endelevu au hatua sahihi kitaifa na locally, za kuiendeleza jamii ya Wamaasai bila kuathiri ecosystem ya Ngorongoro; matokeo yake ni kuibuka kwa divergent local and national interests kama tunavyoona leo!

Maana yake ni kwamba kitaifa kuna makundi kadhaa yenye mitizamo tofauti kuhusu Ngorongoro.

A. Kuna kundi linaloliona eneo lote la Ngorongoro kuwa ni 'Hifadhi ya Ngorongoro'; kwamba ni kivutio cha watalii. Kundi hili kwa upande mmoja linaonekana kuthamini utalii zaidi, labda kuliko uhalali wa makazi ya asili ya Wamaasai.

B. Kuna kundi jingine linaloiona Ngorongoro kama makazi ya asili ya Wamaasai na wanyama. Kundi hili kwa upande wao linaonekana kuthamini makazi ya asili ya Wamaasai, labda kuliko utalii.

C. Lakini vile vile kuna kundi la tatu ambalo linathamini utalii na makazi ya asili ya Wamaasai.

2. Idadi ya binadamu na wanyama katika Ngorongoro ecosystem lazima itaendelea kuongezeka kila mwaka hata kama baadhi yao watu au wanyama leo watahamishiwa Handeni au Unguja nk.

Mpaka sasa kinachosikika toka Serikalini ni mpango wa kuwahamisha baadhi ya wanadamu kutoka makazi yao ya asili ya Ngorongoro kwenda Handeni katika mazingira tofauti, ingawa wanajengewa nyumba mpya za "kisasa".

Kwa bahati mbaya inaonekana kwamba kuna kasoro kadhaa kuhusu mpango huu wa kuwahamisha baadhi ya Wamaasai kama ifuatavyo:

1. Kutokana na hoja mbalimbali za wakosoaji wa mradi/mpango huu hasa mitamdaoni; inaonekana kwamba mtizamo wa wadau muhimu (wawekezaji wa secta ya utalii na Serikali na imeegemea zaidi katika kundi A. hapa juu ambalo linathamini utalii zaidi labda kuliko uhalali wa makazi ya asili ya Wamaasai. Na hii ni kutokana na masuala kadhaa, kwamfano mtiririko wa taarifa kuhusu uchambuzi wa athari HASI za kimazingira na jinsi ya kuzipunguza, ushirikishwaji wa wadau na maamuzi hatua kwa hatua kabla ya kufikia utekelezaji wa uhamisho wa watu kutoka makazi yao ya asili kwenda makazi mapya.

Pengine Serikali ingeweka wazi taarifa za aina nilizotaja hapo juu, na ingeshirikisha kikamilifu jamii husika kufikia maamuzi kabla ya utekelezaji wa mradi hatua kwa hatua, baadhi ya malalamiko na vurugu zingeepukika.

Kwahiyo kwa vile mradi huu ulianza miaka kadha iliyopita nadhani awamu ya 4 kama sikosei, umma ungekuwa una taarifa kuhusu mambo muhimu yafuatayo:

* Ripoti kuhusu idadi za binadamu na wanyama katika Ngorongoro ecosystem, za sasa na vipindi kadhaa mbele.

* Ripoti ya uchambuzi wa athari HASI za kimazingira na jinsi ya kuzipunguza au kuzitatua.

* Ripoti za changamoto mbalimbali kwamfano makazi ya kudumu, huduma za jamii, miundombinu, uchumi nk.

*Gharama za utekelezaji na uendeshaji na vyanzo vya fedha.

Hayo ni baadhi ya masuala mengi yanayopaswa kuwekwa wazi kwa umma wa Watanzania katika kitu kinachoitwa "full disclosure" kuanzia mwanzo kabisa!

Pili, kama nilivyosema hapa juu msingi wa sera za Serikali na wadau katika miradi ya ecosystems lazima iwe kulinda uhai na kuboresha maisha ya binadamu, juu ya viumbe wengine.

Kwa lugha ya kimazingira "overriding interest" ya Serikali katika suala la ku-preserve ecosystem ya Ngorongoro lazima iwe kwanza kabisa, kulinda na kuboresha maisha ya binadamu katika makazi yao ya asili.

Miaka kadha iliyopita kuliibuka suala la 'Vyura wa Kihansi' ambao walisemekana kuwa hatarini kutoweka baada ya mradi wa hydropower kujengwa. Baadhi ya wanamazingira wetu walitaka kusimamisha mradi ili kulinda uhai wa viumbe hao!

Mwisho wa siku vyura hao walihamishiwa USA ili Watanzania wapate umeme.

Maana yake ni kwamba ikijatokea umma wa Watanzania hawana chakula, tutaaacha wafe njaa au tutaruhusu wale nyumbu, nyati na mbogo wa Ngorongoro?
Ni Ngorongoro tu ndio inakumbwa na athari za ongezeko la watu na shughuli zao? Wamasai hawataki hizo nyumba zao. Kwani Wazanzibar wote wana nyumba?
 
Kumbuka binadamu amepewa akili tofauti na wanyama. Binadamu atahama kijijini na kuhamia maghorofani mjini na ataishi maisha mazuri tu, lakini wanyama hawawezi. Ni lazima tutumie akili kuwalinda wanyama na sii kuwaangamiza. Ikibidi binadamu ahamishwe ili kutokuangamiza wanyama na uoto mwingine wa asili.
Wanyama hawajui kuhama?
 
Mwarabu anavyotua na midege mikubwa yenye uzito wa kubeba zaidi ya tani 30 za wanyama ndio anaharibu ecology....istoshe mwarabu sio mwekezaji yeye anachukua wanyama kama wake hajaweka mtaji zaidi ya kuhonga watawala ccm
 
Back
Top Bottom