Hekaya za wamakonde wale walio chanjwa usoni na ndonya mdomoni

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
12,695
31,499
Wakati tunaendelea kuchakata DP World,

Hawa wamakonde OG walikua wengi sana Dar es Salaam, wakati huo mji umejaa mikorosho na haukua na heka heka.

Hawa watu kila waendako walikua wanabadili majina na walikua wanajipa jina lolote litakalo kuwa mbele yao, mathalani: Konokono, Fiat, Train n.k

Kibaya zaidi, kila waendapo kama ni wakristu, i mean wakatoliki, walikua wanabatizwa upya baada ya mafundisho kama wakatekumeni (wakatoliki wataelewa).

Usiku mmoja wa mkesha wa pasaka wakati nikiwa mdogo, padri alikua anambatiza mmakonde mmoja mbaba mtu mzima, akamuuliza unataka uitwe nani, jamaa akamwambia, Yuda Iscariot, padri akakataa, jamaa akamwabia basi Shetani, pardi akakataa, jamaa akamwambia basi Bikira Maria, aisee watu walicheka sana.

Sijui hawa watu wamepotelea wapi siku hizi, walikua burdani sana.
 
Wamehamia Kigamboni ndani ndani huko

Kuna wakati ukifika kigamboni, unakuta wana cheza zile ngoma zao za kumtoa mwali...

Japo wamemezwa na winginwa watu mjini

Ila bado wapo
 
Back
Top Bottom