Haya ni kijijini kwetu, je kwenu?

acheni kuongea kilugha mnatuharibia thread.
SALAMU YETU UREWEDI.soon nakuja kuwapa mambo ya kijijini kwetu dengelua ikiwa included.
u know, tunapokutana huku mijini, kwenye makabila mchanganyiko tunasahau kabisa lugha za nyumbani, at least once per yr kukumbushia lugha sio dhambi plz!!!!!
 
kijijini kwetu siku hizi ukimwi umeingia!hapafai tena

ni kweli Geoff vijiji vyetu sasa si kama zamani Ukimwi unateketeza wanakijiji na bado wanakuwa wakiamini wamelogwa
Kijiji chako nadhani ndio kijiji changu;)
 
nyani<abiziani>; huyajui maisha ya kijijini wewe???:D

mi niko porini bana, ila kiukweli inaweza ikawa kweli .si unajua vijiji vingine hata ukifaulu kwenda form4 unalogwa.teh teh. wanajua umeshatoka kwa hiyo wanakupiga kabali aka stop.
kumbe hawajui kuna kufeli f.2 na f.4. D:
 
NGULI,

nimekupa. Maendeleo unayoyasifia kijijini kwenu ambayo ukiangalia kwa mamakini ni tofauti na katika maeneo mengine, hayo ni matokeo ya mfumo usio sawa (imbalance system) wa kugawa pato la taifa, kwa maana kwamba maeneo fulani fulani hasa maeneo unakotoka wamekuwa wakijipendelea sana kuliko maeneo mengine.Angalia unazungumzia bara bara za lami kijijini, nyumba za kifahari na umeme mapaka umewekwa kwenye miti, wakati mikoa kama Kigoma hakuna umeme wa grid, barabara ya lami ni moja iliyopo mjini tena mbovu sana imejaa mashimo, hakuna wenye uwezo wa kujenga nyumba zisizotumika vijijini. Hapa tunaona matokeo ya akina Basil Mramba, Waziri Mkuu wa zamani Msuya kupendelea mikoa wanayotoka na kusahau kabisa mikoa mingine kwa sasa ninyi mlioendelea mnaiita mikoa ya pembezoni.

Kulikokujisifia namna hiyo ebu piga kelele na mikoa mingine ipewe mgawo uliosawa na huo unaopelekwa kwenue ili wote kwa pamoja tusifie vijiji vyetu kama ulivyosifia vya kwenue. MUNGU IBARIKI MIKOA YA PEMBEZONI NAYO IKUMBUKWE KIMAENDELEO

Fugwe,
Maendeleo hayaletwi na serikali ila inasaidia tu. Kama wanakijiji wana averaji ya ng'ombe 50 kila kaya na hawawezi kujitolea kila mmoja ng'ombe wawili kwa ajili ya kuchangia kuchimba kisima, hata serikali ingeleta maji hayawezi kuwa endelevu kwa sababu hamjaona haja ya kuwa nayo.

Kama mtoto wa hapo kijijini kwenu akishasoma akapata kazi hasubutu kurudi kijijini kwa kuhofia horogwa, hamtakaa mpate maendeleo hata serikali ingefanyaje.

Kama wasomi wenu na wafanyabiashara wakishaoa mke wa mjini wanaona aibu kwenda kutembea nae kijijini kwenu hamuwezi kupata maendeleo kwa sababu mnapotelea mijini na kusahau kwenu.

Kama ukijenga nyumba ya bati kijijini kwenu unarogwa ufe, basi hakuwezi kuwa na majumba ya kifahari. Maendeleo mnayarudisha nyuma wenyewe na wanasiasa wanataka muendelee kuwa maskini ili wawatumie kupata kura za kununua.
 
Kijijini kwetu ni jirani na kwa Nguli, maji ya bomba yapo japo wakati mwingine yanakatika, umeme upo, bara bara lami bado ila ndo wako kwenye final stage.

Kijijini kwetu mambo yanaaza kubadilika, vijana wanakunywa gongo sana na inaathiri utendaji kazi wao. Wazee wanategemea zaidi vijana walioko mijini kuwasaidia kifedha hasa baada ya soko la kahawa kushuka.

Kijijini kwetu misiba inayotokea mijini ni mingi, hivyo shughli za mazishi kila kukicha.
 
Kijijini kwetu mchana nyumba mbavu za mbwa kwa nyasi.....usiku balaa mapaka Bilicanas inakuwepo...uchawi mtupu
 
jamani tusiandike kwa mate wakati wino upo,hebu tuwekeeni picha za huko vijijini kwenu.wengine tu Thomaso
 
Fugwe,
Maendeleo hayaletwi na serikali ila inasaidia tu. Kama wanakijiji wana averaji ya ng'ombe 50 kila kaya na hawawezi kujitolea kila mmoja ng'ombe wawili kwa ajili ya kuchangia kuchimba kisima, hata serikali ingeleta maji hayawezi kuwa endelevu kwa sababu hamjaona haja ya kuwa nayo.

Kama mtoto wa hapo kijijini kwenu akishasoma akapata kazi hasubutu kurudi kijijini kwa kuhofia horogwa, hamtakaa mpate maendeleo hata serikali ingefanyaje.

Kama wasomi wenu na wafanyabiashara wakishaoa mke wa mjini wanaona aibu kwenda kutembea nae kijijini kwenu hamuwezi kupata maendeleo kwa sababu mnapotelea mijini na kusahau kwenu.

Kama ukijenga nyumba ya bati kijijini kwenu unarogwa ufe, basi hakuwezi kuwa na majumba ya kifahari. Maendeleo mnayarudisha nyuma wenyewe na wanasiasa wanataka muendelee kuwa maskini ili wawatumie kupata kura za kununua.

Nashukuru kwa kumjibu Fungwe, nashangaa analalamika viongozi wa kanda yetu wanapendelea sana upande wetu na wameshika nyadha za waziri wa fedha na waziri mkuu ila na mimi naomba nimuulize swali mbona Rais na Shemeji yetu bwana na ndugu William Benjamin Mkapa kapakimbia na sasa yuko Tanga kwa nini hakurudi uko kupaendeleza??(Rejea maelezo ya Mchili)

Ngachihiyo baasi

Hata mimi pia.
 
Jamani hebu tusiandike kwa mate wakati wino ungalipo ,kila mtu atupe picha ya huko kijijini kwao .Wengine tu Thomaso
 
Kijijini kwetu maji kila nyumba kwa sasa na yanapatikana wakati wote..Suala la kulipa bill ndo lilitaka kuleta utata kwa wazee hawajazoea kulipia maji maishani kwao. wanaamini ni bidhaa ya bure toka kwa mungu.

Barabara inapitika hata wakati wa mvua na tetesi huenda ikatengenezwa kiwango cha lami kama tutachagua chama chenye dola...

Shule zimeongezeka na idadi ya vijana wanaosoma ni kubwa na kujiunga na vyuo vikuu nchini.

Wanywa pombe aina ya gongo wanaongezeka na vijana wengi kujihusisha na udokozi/wizi.

Mahudhurio ya kanisani kila jumapili bado ni makubwa pamoja na kanisa kuwa mbali na kutokuwa na kigangoo..

Tuliotoka Dar na maeneo mengine tukionekana weneyeji wanafurahi na kutuomba chochote hasa pombe aina ya mbege, beer na pesa.

Majadiliano ya kisiasa na mustakabali wa nchi yameshamiri na Zitto Kabwe ni miongoni mwa wanasiasa maarufuu akimfuatia MZEE WA KIRARACHAAA.
Nyie wachaga bana,mnapenda tudanganya cc haya tena hiyo lami mpaka mpakani imefika lini?
 
nimekupa.

Mazee hapa umenipa nini?

Maendeleo unayoyasifia kijijini kwenu ambayo ukiangalia kwa mamakini ni tofauti na katika maeneo mengine, hayo ni matokeo ya mfumo usio sawa (imbalance system) wa kugawa pato la taifa, kwa maana kwamba maeneo fulani fulani hasa maeneo unakotoka wamekuwa wakijipendelea sana kuliko maeneo mengine.
Msuya kupendelea mikoa wanayotoka na kusahau kabisa mikoa mingine kwa sasa ninyi mlioendelea mnaiita mikoa ya pembezoni.

Tunajipendelea na nini? soma historia ya nchi vizuri...kwa hio hata wakoloni walitupendelea?? na kama ndio kwa nini?? Je mikoa yenu haina viongozi? kama wapo kazi yao ni nini? mbona wasipendelee kama wetu unavyodai wanatupendelea?

Kulikokujisifia namna hiyo ebu piga kelele na mikoa mingine ipewe mgawo uliosawa na huo unaopelekwa kwenue ili wote kwa pamoja tusifie vijiji vyetu kama ulivyosifia vya kwenue.

Kwa taarifa yako kuna maeneo huku kijijini kwetu yamewekwa lami na watu binafsi na hawakuisubiri serikali.


MUNGU IBARIKI MIKOA YA PEMBEZONI NAYO IKUMBUKWE KIMAENDELEO

Mungu ameshabariki siku nyingi hapa nahisi anakushangaa na hio statement watu wafanye kazi kwa bidii watunze mazingira ..kwa mafano kijijini kwetu ni kosa kukata miti ila unaruhusiwa kupanda miti, kumegeuka msitu, ikifika jumamosi kuna kitu kinaitwa msarakambo lazma wote mwaamke saa 12 am mkasafishe vyanzo vya maji au kuchimba barabara na usiposhiriki wanakuja kuchukua mbuzi 1 wanauza wanamlipa kibarua anafanya ile kazi yako. Je kwenu hilo lipo??
heri umewatolea uvivu ndugu yangu, kazi hawataki, waharibifu wa mazingira niwao, walalamishi ni wao pia na maendeleo wanayataka! haiwezekani, rudini vijijini kwenu na muhimizane kufanya kazi kwa bidii maendeleo mtayaona na si kwa kupiga umbea na kulalamika kwa kila kitu.
 
mh jamani mi naogopa kuzungumzia kijiji chetu ,inawezekana raia wa kijiji changu wamo humu JF,lakini nitawanong'oneza.
kijiji chetu kimetia fora kwa uchawi,ukitaka kufanya sherehe lazima uombe ruksa kwa watu fulani,ukiwa na mtoto mchanga kama hujajipendekeza kwa watu fulani hapo utashika adabu yako mwenyewe utachukua room hospitali kwa vigonjwa visivyokuwa na kichwa wala miguu, kila wakati unatakiwa upige mizinga ili na wewe uonekane unashida la sivyo shughuli ipo.na ukienda kutembelea wazee siku ya kuondoka usiage majirani na kama wamekuona unawaambia siondoki bali naenda kulala kwa x hapo mbele la sivyo utasindikizwa na usivyoviona.
 
Back
Top Bottom