Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Wote wanaoonekana kwenye picha ni wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
Samahani kwa lugha hii lakini ina maana nikisema pole zake kwa "nyani asiyeweza kuona manyoya yaliyvonyonyoka makalioni mwake." Binafsi huwa nasikia aibu kubisha hodi kila siku nyumbani kwa mtu, wengine kama akina kikwete haya zimewatoka.
Kuchokwa ndio huko ambapo unaona hata tu gavana wa jimbo haendi kumpokea ila analakiwa na watanzania. Uzururuaji mwingine ni aibu na atakapomaliza muda wake tutasikia mengi kwa hawa wamarekani. Wamarekani si wa kudeka nao ipo siku watayaanika madudu yake kama walivyomwanika kuhongwa suti huko Uingereza.
Sina shaka kama Kikwete passport yake anahitaji kubadilishiwa kila mwaka maana inajaa haraka kwani makazi yake ni kuzunguka zaidi duniani badala ya kuwatumikia watanzania. FaizaFoxy anajua maana ndiye anayemwandalia masurufu ya safarini.