Haya ndio maisha ya Alphonce Simbu mwanariadha wa marathon aliyetuwakilisha Brazil,anastahili pongez

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,825
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg


PENGINE isingekuwa rahisi kufikiria kwamba kuna kijana Mtanzania kutoka Mkoa wa Singida angeweza kuiletea heshima nchi ya Tanzania katika michezo ya Olimpiki mwaka huu, iliyomalizika jijini Rio de Janeiro, Brazil, akimaliza mbio ndefu (marathon) na kushika nafasi ya tano.

Hii ni kwa kuwa Watanzania wameshazoea kuona washiriki wengi wakitoka katika mashindano makubwa, wanarudi mikono mitupu na mkebe wa visingizio, hivyo kukata tamaa kuwafuatilia.

Alphonce Felix Simbu (24), aliyerudi nyumbani kwa ndege ya Shirika la ndege la South Africa Airways(SAA), amewashtua watu ambao walikata tamaa, si tu wanamichezo, bali pia na ambao si wanamichezo, hasa majirani wa mwanariadha huyo, mkazi wa Sakina kwa Iddi, jijini Arusha, nao pia wamejikuta wakipigwa na butwaa baada ya kusikia habari hizo nzuri.

Kutokana na nafasi hiyo aliyoipata Simbu, MTANZANIA lililazimika kufunga safari hadi nyumbani kwake, Sakina kwa Iddi na kufanya mazungumzo na mke wake, Rehema Daud (22).

Rehema, mama wa mtoto mmoja, Abednego, mwenye umri wa miezi nane, yeye na mumewe wanaishi katika nyumba ya kupanga eneo hilo la Sakina, wakiwa ndani ya chumba kimoja walichokigawanya kwa pazia ili kupata sebule na chumba cha kulala.

Akizungumzia maisha yao binafsi na mumewe, Rehema anasema anamshukuru Mungu kumkutanisha na mume mpole na mtulivu ambaye tangu wameoana mpaka sasa wana takribani mwaka mmoja na miezi mitatu.

“Mume wangu tulikutana hapa hapa Arusha eneo hili la Sakina, tulipendana na kuamua kuishi pamoja, Mungu ametujalia mtoto wa miezi nane sasa,” anasema Rehema, huku akiingia chumbani kwake kumchukua mwanawe, aliyekuwa akimvalisha kabla ya ujio wangu nyumbani hapo.

Huku akiwa amembeba mtoto wake, Rehema anaelezea maisha ya kawaida ya mume wake Simbu kuwa hana aina nyingine ya kazi inayomuingizia kipato, zaidi ya kujishughulisha na ukimbiaji (riadha) katika mashindano tofauti anayoalikwa kushiriki.

Anasema katika kushiriki huko ndipo hufanikiwa kupata riziki yake ya siku inayomwezesha kuendesha maisha yake, mkewe na mtoto wao mmoja, ikiwamo kulipia kodi ya chumba kimoja.

“Hana kazi nyingine zaidi ya kukimbia tu, kila siku huwa anafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye maeneo haya ya jirani na nyumbani na hasa maeneo ya milimani.

“Lakini pia sijui maeneo yake mengine ambayo anapenda kufanyia mazoezi,” anasema Rehema, huku akionyesha baadhi ya vikombe alivyowahi kushinda mumewe.

Rehema anamshukuru sana Mungu, kwa kumjalia mumewe ambaye ni mwenyeji wa Kijiji cha Mampandu, mkoani Singida, kushika nafasi hiyo ya tano kwenye mashindano hayo makubwa kabisa duniani.

Mbali na kutegemea kazi ya kufukuza upepo anayoifanya mumewe, Rehema anaweka wazi kwamba amefanikiwa kufungua saluni kwa ajili ya kutengeneza nywele za wanawake, hivyo kumsaidia mumewe katika baadhi ya majukumu ya kifamilia.

“Namshukuru sana Mungu, kwani mume wangu ndiye alinipa mtaji wa kufungua saluni hapo kwa Iddi. Lakini kwa sasa nimelazimika kuifunga ili nipate kumlea vizuri mtoto wangu,” anasema Rehema.

Akiwazungumzia wanariadha wengine nchini, Rehema anawaomba waendelee kufanya mazoezi na kujipa matumaini ya kufanya vizuri zaidi katika siku zijazo badala ya kukata tamaa mapema.

Wakati Simbu akifanikiwa kuandika historia ya mchezo wa riadha kwa hapa nchini kwa kuingia tano bora, majirani zao wameonyesha kushangazwa zaidi na ushindi huo.

Said Msuya (32), mkazi wa eneo hilo la Kwa Iddi, anasema kwa muda mrefu sasa amekuwa akimuona Simbu akifanya mazoezi ya kukimbia kila siku, lakini hakuwa anamuelewa.

Unajua nini broo, huyu chalii (kijana) Simbu kwanza sijaamini kama ndiye yeye aliyeonekana huko Brazil akikimbia mbio, hebu angalia hapa nyumbani kwake anaishi maisha ya kawaida kabisa kwenye nyumba ya kupanga.

“Huwezi tegemea, kwanza mimi binafsi sikujua kabisa yuko wapi mpaka juzi kati hivi mtaani kwetu walipoanza kusema yule chalii mwanariadha ameshinda riadha Brazil,” alisema Msuya.


Simbu akiwa nchini Brazil alifanikiwa kukimbia kwa kutumia saa 2:11:15, sekunde 11 nyuma ya mshindi wa nne, Ghirmay Ghebreslassie.

Katika mbio hizo, Mkenya Eliud Kipchoge aliibuka mshindi na kunyakua medali ya dhahabu katika mbio za marathoni upande wa wanaume.

Feyisa Lilesa wa Ethiopia alimaliza wa pili akiwa nyuma ya Kipchoge kwa sekunde 70 na kushinda medali ya fedha, huku Mmarekani Galen Rupp akimaliza wa tatu na kujishindia medali ya shaba.
Simbu anahitaji pongezi kubwa sana sana,kwa sababu amekimbia na watu wenye mazoezi na mafanikio makubwa sana ktk ulimwengu wa riadha.Wakati Simbu akijitegemea ktk mazoezi na aina ya chakula cha kula wakati wa kujiandaa na mazoezi,Kipchonge alikuwa chini ya uangalizi mkubwa wa wafadhili/wadhamini wake,wakiwemo Kenya Airways,Nike,Kampuni za Bia,DsTv,KCB,Nakumat nk.

Mshindi wa kwanza mpaka wa nne ni watu wenye maisha ya juu,matajili na waliojiandaa kisasa kwa muda mrefu.Huku Simbu akiwa anaishi ndani ya chumba kimoja Arusha,akiamka asubuhi na kuanza mazoezi,wenzake walikuwa katika maisha ya juu na mazoezi ya kisasa.Tumtie moyo Simbu,Serikali iwekeze kwa Simbu ili Tokyo2020 aweze kushiriki akiwa na maisha mazuri na hali nzuri kiafya.


Kwa mfano kwa sasa Rais wa Shirikisho la Raidha Tanzania ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Huyu hana historia yoyote au record ktk ulimwengu wa riadha,nafasi hiyo anaitumia tu kisiasa na kujipatia umaarufu.Rais kama huyu ktk riadha ni ngumu kujuwa matatizo ya riadha na wanariadha.Aina hii ya uongozi ni jipu kwa sbb wapo kwa maslahi ya kisiasa.

Kamati ya Olympic chini ya F-Bayi ijitathmini upya.Inatosha kwa Bayi kuongoza kamati hiyo na atoe nafasi kwa vijana.Hakuna ulazima wa yeye kuzeekea kwenye kiti kama Mugabe.Tunahitaji kwenda Tokyo2020 tukiwa na team ya ushindi itakayotuleta medali.

Kwangu mimi Simbu ndio bingwa wa Marathon,kwa maisha anayoishi....Hakika ameshinda medali ya dhahabu toka ktk mioyo ya WatanzNia wapenda michezo....Hongera sana Mtanzania mwenzetu.
 
Pongezi za nini wakati ajarudi na medali hakuna lolote pongezi kwa samata siyo hao watalii wa brazil
 
Duh. Miaka 24........chumba kimoja cha kupanga . na tayari ana mke mwenye miaka 22 na mtoto. Haya hongera zake
 
Pongezi za nini wakati ajarudi na medali hakuna lolote pongezi kwa samata siyo hao watalii wa brazil
Pongezi za nini wakati ajarudi na medali hakuna lolote pongezi kwa samata siyo hao watalii wa brazil
Wew umeleta medali gani?Hata kwa familia yako umeleta tuzo gani?Kuwa wa tano kati ya wanariadha 268 unadhani ni kitu kidogo??
 
Duh. Miaka 24........chumba kimoja cha kimoja. na tayari ana mke na mtoto. Haya hongera zake
Maisha tunatofautina....Hustling ya maisha ni mtu na mtu!Vijana waliokulia kota experience hii huwezi elewa!!Unashangaa mtu kuanza maisha na room moja?Huyu ni mtu toka Singida vijijini huko ambako mpaka leo hata simu haijafika....Kwake ni mafanikio
 
Kwa hiyo lifestyle,next Olympics is very uncertain.............Awezeshwe,apate kwenda next level.
 
Kabla ya Mtaka kuwa rais wa hilo shirikisho nani alikuwa President?

Je tulitwaa medali ngapi kabla ya Mtaka?

Kina Kipchoge hawakupata wadhamini just from nowhere,walianza kama Simbu tu baada ya uwezo wao kuonekana ndo watu wakaweka pesa zao.

Kijana akaze tu kwani Filbert Bayi alitoboa vipi?

Kama kaamua kuishi kwa kutegemea michezo asitegemee serikali kumgharamia maisha yake yote ili yeye awe anashinda anafanya mazoezi tu.

Sana sana serikali ataiona atakapoitwa kupiga kambi kwa ajili ya mashindano.
 
Duh. Miaka 24........chumba kimoja cha kupanga . na tayari ana mke mwenye miaka 22 na mtoto. Haya hongera zake
Hongera zako wewe ulietengenezewa maisha Na wazazi wako, mwenzio kila kitu ni juhudi zake.

Hana pa kujishikia zaidi ya kipaji chake Na juhudi binafsi...anaamka asubuhi anafanya mazoezi hakuna anaemjali anakula nini, analala wapi wala kiujumla maisha yake yakoje.

Wewe Mwenye kila kitu katika umri huo hakuna anaekujali wala kukupa heshima ndani ya Taifa....

Leo ameshika nafasi ya tano kati ya wanariadha 268 Duniani kote tena wengi wao walioandaliwa vya kutosha.

Mpe heshima yake...Mungu amsaidie apate wadhamini kuelekea 2020 Japan naamini anaweza kufanya maajabu.
 
Naona umeenda mbali sana na kudhani labda Nime hate. Mimi sija criticise ushindi wake......nimeupenda sana ushindi wake ila nimekuwa interested na life style yake. maana angekuwa kijijini sawa. Lakini ndani ya jiji la arusha kama wanavyoita wenyewe . 24 yrs tayari una mke na mtoto. Chumba kimoja cha kupanga.
 
Back
Top Bottom